Global News

EU YAJADILI KUKATA MSAADA BURUNDI
Global News

MUUNGANO wa Ulaya EU umeanza kikao maalum kujadili uwezekano wa kukata msaada wake nchini Burundi na inakisiwa kuwa fedha kutoka muungano huo unafikia zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya Burundi ya kila mwaka.   Mkuu wa masuala ya mambo ya nje wa Muungano wa EU Federica Mogherini, ameelezea wasiwasi wake juu ya ghasia zilizototokea nchini humo kabla ya kufanyika  kwa uchaguzi wa rais, na ametilia shaka iwapo serikali itakayoundwa baada ya uchagzi huo itakuwa wakilishi ya taifa nzima. Uamuzi...

Like
183
0
Friday, 24 July 2015
MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KUTANGAZWA KESHO BURUNDI
Global News

MATOKEO katika  uchaguzi  wa  rais  uliofanyika  nchini Burundi  wiki  hii  yatatangazwa  kesho, ambapo  rais  aliye madarakani  Pierre Nkurunziza  anatarajiwa  kushinda kipindi  cha  tatu huku  wapinzani  wake  wakidai  kuwa  ni kinyume  na  katiba. Mkuu  wa  Tume  ya  uchaguzi  nchini  Burundi  Pierre-Claver  Ndayicariye  amesema  kiasi  cha  asilimia 72 hadi 80  ya  wapiga kura  wa  nchi  hiyo  wanaofikia  milioni  3.8 wamepiga  kura  siku  ya  Jumanne....

Like
164
0
Thursday, 23 July 2015
AU YATEKA NGOME YA MWISHO YA AL SHABAAB
Global News

IMEELEZWA  kuwa Mji muhimu wa mwisho uliokuwa mikononi mwa kundi la Al Shabaab kusini magharibi mwa Somalia wa Baardheere umechukuliwa tena na vikosi vya Muungano wa Afrika (AU) -miaka 7 baada ya wapiganaji hao wenye itikadi kali kuingia kwa mara ya kwanza katika mji huo . Wakazi wa mji huo wamesema vikosi vya Kenya na Somalia vikiwa na silaha nzito na usaidizi wa mashambulizi ya anga viliuvamia mji huo , ambao wapiganaji wa Al Shabaab waliutoroka usiku. Majeshi kutoka Kenya,...

Like
203
0
Thursday, 23 July 2015
LIBERIA: KAMPUNI YA MAWESE YASHUTUMIWA KUJINUFAISHA KUPITIA MLIPUKO WA EBOLA
Global News

SHIRIKA moja la kutetea haki za binadamu limeishutumu mojawepo ya kampuni kubwa zaidi duniani ya mauzo ya mawese iliyoko nchini Liberia kwa kutumia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kujinufaisha. Shirika hilo la Global Witness limesema kuwa wakati mlipukowa ugonjwa huo ulipoifikia Afrika Magharibi mwaka uliopita kampuni ya Golden Veroleum ilifyeka maelfu ya ekari kwa maandalizi ya kilimo cha zao la mawese wakati ambapo makundi ya misaada kwa jamii yalikuwa yanashughulika na kuokoa maisha ya watu kutokana na ugonjwa huo. Hata...

Like
259
0
Thursday, 23 July 2015
UGIRIKI YAKUBALI MASHARTI YA WADENI
Global News

WABUNGE wa Ugiriki wamepiga kura ya kuunga mkono mashariti mapya yaliyowekwa na wadeni wa taifa hilo lililo katika hatari ya kufilisika. Hatua hiyo inatoa nafasi ya kuanzishwa kwa mashauriano mapya kati ya taifa hilo pamoja na mataifa mbalimbali yanayotoa msaada wa kuokoa uchumi wa nchi hiyo kutoshuka. Hata hivyo Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras alishinda kura hiyo ya Bunge baada ya kura ya kuunga mkono kupigwa na vyama vingine vya upinzani juu ya suala...

Like
187
0
Thursday, 23 July 2015
KIONGOZI WA AL QAEDA AMEUAWA
Global News

JESHI la Marekani limesema kuwa mmoja viongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, ameuwaa katika shambulio la angani lililotekelezwa na ndege za kijeshi za Marekani Nchini Syria. Idara ya ulinzi ya Pentagon imesema kuwa Muhsin al-Fadhli, alikuwa kinara wa kundi la Khorasan, lililotumwa na al-Qaeda, kutoka Pakistan hadi nchini Syria. Mmoja wa wajumbe wa bunge la congress amesema kuawawa kwa mtu huyo Al Fahdli mwenye ufahamu na gaidi hatari ambaye amekuwa akijaribu kuiangamiza Marekani na washirika wake ni faraja...

Like
183
0
Wednesday, 22 July 2015
KURA ZAANZA KUHESABIWA BURUNDI
Global News

SHUGHULI ya kuhesabu Kura imeanza nchini Burundi kufuatia uchaguzi wa urais ambao umeshutumiwa na wengi nchini humo na hata kimataifa. Rais Pierre Nkurunzinza anatarajiwa kupata ushindi mkubwa kwa muhula wa tatu huku upinzani ukisusia kabisa kura hiyo. Huku hayo yakijiri Marekani na Uingereza wamekashifu kura hiyo wakisema kuwa haikuwa ya huru na haki. Marekani kwa upande wake imependekeza kugawana madaraka huku ikitishia kuchukua hatua dhidi ya Burundi iwapo muafaka...

Like
149
0
Wednesday, 22 July 2015
SENEGAL: KESI YA HABRE YAAHIRISHWA
Global News

KESI ya kihistoria dhidi ya Kiongozi wa zamani wa Chad Hissene Habre iliyokuwa imerejeshwa mahakamani leo nchini Senegal sasa imeahirishwa hadi mwezi Septemba mwaka huu. Mahakama imetoa muda huo kwa wakili wapya wa kiongozi huyo wa zamani wa kimila kujiandaa kwa kesi inayomkabili ya makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili na uhalifu wa kivita. Habre ambaye amekataa kuitambua mahakama hiyo alikataa kuzungumza mahakamani huku akiwashauri wakili wake wasimwakilishe mahakamani hatua iliyomlazimu hakimu kuingilia kati na kushurutisha apewe...

Like
163
0
Tuesday, 21 July 2015
BURUNDI WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS
Global News

BAADA ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa iliyopita hatimaye raia nchini Burundi sasa wamefika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao atakayewaongoza kwa muhula ujao. Taarifa zinasema kuwa watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura kufuatia vurugu zilizoambatana na gruneti pamoja na milio ya risasi. Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo huku viongozi wanne...

Like
191
0
Tuesday, 21 July 2015
UGIRIKI YAONYESHA MATUMAINI YA KUJINUSURU KUFILISIKA
Global News

SERIKALI ya Ugiriki imefanikiwa kuwasilisha sehemu ya malipo ya deni lake kwa Shirika la Fedha la Kimataifa –IMF– hali inayoashiria kutokuwepo tena kwenye hatari ya kufilisika. Msemaji wa –IMF– Gerry Rice amesema katika taarifa yake muda mfupi uliopita kwamba Ugiriki imelipa euro bilioni 2 jana ambapo Kamisheni ya Ulaya iliruhusu nchi hiyo kupatiwa mkopo wa euro bilioni 7 ili kuiwezesha serikali ya waziri Mkuu Alexis Tsipras kulipa sehemu ya madeni yake kwa Benki Kuu ya Ulaya na IMF. Msemaji wa...

Like
279
0
Tuesday, 21 July 2015
BRAZIL YAANZISHA UCHUNGUZI KUFUATIA MAUAJI YA WATU 35
Global News

MAMLAKA ya Ulinzi nchini Brazil katika mji wa Manaus imeanzisha uchunguzi kufuatia mauaji yaliyotokea na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 35 kati ya wiki iliyopita na siku ya jana asubuhi. Taarifa zinaeleza kwamba Mauaji hayo yalianza mara baada ya sajenti mmoja wa polisi kupigwa risasi nje ya Benki katika nji huo ambao ni mwenyeji wa michuano ya Olympic mwaka 2016. Hata hivyo Mauaji hayo yaliyoanza siku ya ijumaa usiku na kuendelea Siku ya jumatatu yamesababisha Vikosi vya usalama wa...

Like
193
0
Tuesday, 21 July 2015