Global News

NASA WAPATA TAARIFA ZA SAYARI YA PLUTO
Global News

WANASAYANSI wa NASA kutoka Marekani wanasema kuwa majaribio yao ya kurusha chombo kwenda katika sayari ya Pluto yamekuwa na mafanikio makubwa. Chombo hicho kimefanikiwa kutuma taarifa katika kituo cha utafiti huo cha Maryland zilizochukua takribani saa nne na nusu hadi kufika duniani na kupokelewa na antenna NASA. Saa chache zijazo wanasayansi hawa wa NASA wameeleza kuwa wanatarajia kupata mfululizo wa taariza zaidi na picha kutoka sayari hiyo ya Pluto ambazo zitatoa uhalisia wa undani wa sayari hiyo ya...

Like
381
0
Wednesday, 15 July 2015
MUSEVENI AENDELEA NA MAZUNGUMZO YA AMANI BURUNDI KWA SIKU YA PILI
Global News

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni leo ameingia siku yake ya pili ya mazungumzo ya amani nchini Burundi. Ikiwa imebaki siku chache tu kufanyika kwa uchaguzi wa Rais, inaonekana kuna nafasi ndogo ya Rais Museveni kuweza kushawishi lolote kuhusiana na msimamo wa Serikali ya Burundi kuhusiana na uchaguzi wa Burundi. Mara baada ya kuwasili nchini Burundi, rais Museveni amewakumbusha raia wa Burundi moja ya jambo baya lililowahi kutokea nchini humo na ambalo halipaswi kuwepo kwa sasa ambalo ni mgawanyiko wa kikabila...

Like
469
0
Wednesday, 15 July 2015
EBOLA: TAHADHARI YA MAAMBUKIZI ZAIDI YATOLEWA SIERRA LEONE
Global News

MAOFISA wa Afya nchini Sierra Leone wametahadharisha uwezekano wa kutokea kwa maambukizi zaidi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ikiwa ni mwaka mmoja tangu mgonjwa wa kwanza kubainika nchini humo. Wamesema kuwa hofu ya baadhi ya watu kukataliwa na kutengwa na jamii ni moja ya sababu inayochangia kuenea kwa maambukizi hayo kwani wengi hujificha wanapokumbwa na ugonjwa huo. Hata hivyo kumekuwa na kasi ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika siku za hivi karibuni ingawa katika makao makuu ya...

Like
172
0
Tuesday, 14 July 2015
NYUKLIA: IRAN YAKUBALIANA NA MATAIFA 6 MAKUBWA
Global News

MAZUNGUMZO kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yemeendelea hadi usiku wa kuamkia leo mjini Vienna kujaribu kufikia makubaliano yatakayoweza kuudhibiti mpango huo na kuizuia Iran kutengeneza silaha za atomiki. Msemaji wa ikulu ya Marekaani Josh Earnest amesema kuwa baadhi ya masuala muhimu yameshughulikiwa, lakini bado kuna masuala mengine yanayoendelea kuleta mzozo. Ikiwa kuna muafaka kuhusu vipengele vyote vya makubaliano hayo, wanadiplomasia wakuu kutoka baadhi ya mataifa makubwa ikiwemo Iran, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani...

Like
183
0
Tuesday, 14 July 2015
WAZIRI MKUU UGIRIKI AKABILIWA NA UPINZANI
Global News

WAZIRI mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras anazidi kukabiliwa na upinzani huko Athens kwa hatua mpya na kali za malipo alizokubali kuzitambulisha kutokana na masharti mapya ya kuokoa kuporomoka kwa uchumi. Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Panos Kammenos ambaye anaongoza chama kidogo katika muungano wa serikali ya kitaifa ameelezea mpango huo kuwa ni mapinduzi ya serikali. Habari kutoka chama hicho zinasema kwamba mkataba uliowekwa ni wa kuifedhehesha Ugiriki nchi hiyo kwa kuwa unalitaka bunge la ugiriki kupitisha ongezeko la kodi,...

Like
165
0
Tuesday, 14 July 2015
DAWA ZA KULEVYA ZACHAFUA HALI YA HEWA MEXCO
Global News

WAZIRI wa mambo ya ndani wa Mexco ameitisha mkutano wa magavana wa majimbo ili kujadili namna ya kuepusha vurugu zinazoweza kutokea kufuatia kutoroka kwa mtuhumiwa maarufu wa biashara ya dawa za kulevya. Vyombo vya usalama ndani ya Mexico na maeneo ya jirani kwa sasa vinamtafuta Joaquin Guzman ambaye ni mfanyabiashara mkubwa wa dawa hizo kwa kutoroka katika mazingira yanayodaiwa kuwa ni ya rushwa. Naye Rais wa Mexco Enrique Pena Nieto amesema kuwa ana Imani kuwa idara za usalama zitamkamata mtuhumiwa...

Like
158
0
Tuesday, 14 July 2015
23 WAUAWA BAADA YA KAMBI YA JESHI KUPOROMOKA URUSI
Global News

TAKRIBAN wanajeshi 23 wa Urusi wameuawa karibu na mji wa Omsk ulioko Siberia baada ya jengo la kambi ya kijeshi kuporomoka. Wanajeshi wengine 19 waliokolewa kutoka ndani ya  vifusi vya jengo hilo. Mwanajeshi mmoja aliyeokolewa ameileza runinga ya Urusi kwamba wanajeshi walikuwa wamelala wakati wa ajali...

Like
261
0
Monday, 13 July 2015
ULAYA YAKUBALI KUIPA UGIRIKI MKOPO MWINGINE
Global News

VIONGOZI wa mataifa ya ulaya yanayotumia sarafu ya Euro wamekubaliana kwa pamoja kuipa Ugiriki mkopo mwingine ili kuinusuru uchumi wake kuporomoka zaidi. Makubaliano hayo yamejiri baada ya mazungumzo ya dharura baina ya mawaziri wa fedha wa ukanda wa Ulaya waliodhamiria kuiokoa nchi hiyo kiuchumi kutokana na kupungukiwa fedha. Rais wa baraza la ulaya Donald Tusk ametangaza kuwa makubaliano yameafikiwa baada ya mazungumzo hayo marefu yaliyochukua takriban saa kumi na saba ambapo amesema pia kabla ya kutumika makubaliano hayo yatahitajika...

Like
245
0
Monday, 13 July 2015
SOMALIA KUFUNGUA KESI YA MPAKA KATI YAKE NA KENYA
Global News

SERIKALI ya Somalia leo hii itafungua rasmi kesi dhidi ya kenya katika Mahakama ya kimataifa kufuatia mgogoro wa mpaka baina ya nchi hizo mbili. Taarifa zaidi kutoka BBC zinaeleza kuwa Somalia inailamu kenya kuwa inamiliki sehemu ya bahari ya nchi hiyo kwa njia isiyo halali ingawa Mgogoro huu umefikia kipindi cha miaka sita sasa. Somalia inaipeleka Kenya katika mahakama ya kimataifa huko The Hague Uholanzi kwa madai kwamba kenya imekataa usuluhishi nje ya mahakama....

Like
223
0
Monday, 13 July 2015
MEXICO YAANZA MSAKO MKALI KUMSAKA MUUZA MIHADARATI
Global News

SERIKALI nchini Mexico imeanza msako mkali wa kumtafuta Joaguin Guzman ambaye ni maarufu wa biashara ya dawa za kulevya duniani, kufuatia kutoroka katika gereza lenye ulinzi mkali mwishoni mwa wiki. Helikopta za Blackhawk ambazo zimeonekana kuruka juu gerezani Altiplano magharibi ya Mexico City mahali alipokuwa ameshikiliwa mfanyabiashara huyo. Wafanyakazi wa magereza wamehojiwa baada ya kubainika kuwa Joaguin alitoroka kupitia njia ya chini ya ardhi yenye urefu wa kilomita moja na hii ni mara ya pili kwake...

Like
283
0
Monday, 13 July 2015
MBABAZI NA BESIGYE WASHIKILIWA NA POLISI UGANDA
Global News

POLISI  nchini Uganda imewakamata viongozi wawili wa upinzani na wagombea wa urais wanaotazamiwa kupambana dhidi ya rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao. Gazeti la serikali la New Vision limeripoti kuwa waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi amekamatwa na polisi katikati mwa Uganda, wakati Kizza Besigye, kiongozi wa zamani chama cha Forum for Democratic Change FDC, alikamatwa nyumbani kwake nje ya mji mkuu Kampala. Dr. Kizza...

Like
246
0
Thursday, 09 July 2015