Global News

MKUTANO WA MATAIFA IMARA YANAYOINUKIA KIUCHUMI DUNIANI KUANZA LEO URUSI
Global News

MKUTANO wa kilele wa baadhi ya mataifa imara yanayoinukia kiuchumi duniani unaanza rasmi leo nchini Urusi. Nchi zinazoshiriki zinafahamika kama BRICS yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini. Benki ya BRICS ilizinduliwa mapema wiki hii, ambayo itafadhili miradi ya miundo mbinu katika nchi...

Like
153
0
Thursday, 09 July 2015
DILMA ROUSSEFF ATOA MSIMAMO WAKUTOTISHIKA
Global News

WAKATI tuhuma zikiongezeka juu ya mustakabali wa serikali yake rais Dilma Rousseff  wa Brazil ameliambia gazeti la Folha de Sao Paulo kwamba hatishiki na kwamba hakuna msingi wa yeye kuachishwa kazi na bunge. Ikiwa ni miezi saba baada ya kuingia katika muhula wake wa pili wa uongozi serikali yake inazidi kutikiswa na kashfa ya rushwa katika kampuni kubwa ya mafuta nchini Petrobras. Tuhuma za hivi karibuni zinadai kwamba kampeni yake ya kuwania urais ilifadhiliwa kwa fedha haramu kutoka kampuni hiyo...

Like
193
0
Wednesday, 08 July 2015
UGIRIKI YAAHIDI KUTIMIZA MASHARTI MAPYA
Global News

SERIKALI ya Ugiriki ipo katika harakati za kuandika mapendekezo mapya yatakayofanikisha mazungumzo ya kutafutia ufumbuzi wa matatizo yake ya kiuchumi. Hali hiyo imekuja kufuatia viongozi wa Ukanda wa Ulaya mjini Brussels kuipa nchi hiyo muda wa siku tano kupeleka mapendekezo yake ya kusaidia kuondokana na tatizo la uchumi. Mbali na nchi hiyo kupewa muda huo wa kupeleka mapendekezo yake  lakini Raisi wa baraza la viongozi wa ukanda wa ulaya Donuld Tusk ameonya kuwa zimesalia siku chache kutatua mgogoro wa Ugiriki...

Like
220
0
Wednesday, 08 July 2015
MKUTANO MKUU WA NCHI ZENYE NGUVU DUNIANI KUENDELEA VIENNA,AUSTRALIA
Global News

MKUTANO mkuu wa nchi sita zenye nguvu duniani ikiwemo Iran unatarajiwa kuendelea tena huko Vienna nchini Australia, pamoja na tarehe ya kuhitimishwa kwa mazungumzo hayo kutajwa . Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi,Sergei Lavrov, amesema kwamba awali kulikubwa na sababu ya kuamini kuwa suala hilo litahitimishwa katika siku chache lakini haikuwa hivyo. Naye waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa,Laurent Fabius amehakikisha kutoondoka mapema katika meza ya mazungumzo hayo ambapo pia ametaja hatua zitakazo chukuliwa...

Like
186
0
Wednesday, 08 July 2015
MAREKANI NA VIETNAM ZAIMARISHA MAHUSIANO YAO
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amefanya mazungumzo na kiongozi wa chama cha jamii ya wavietnam Ikulu mapema wiki hii,mkutano ambao ni wa kwanza tangu nchi hizo mbili kurejesha uhusiano baada ya miaka ishirini iliyopita. Rais Obama amesema kwamba pamoja na kutofautiana kwa falsafa za kisiasa,nchi kati ya nchi hizo mbili bado unahitajika ushirikiano wa dhati, katika kujiimarisha kiuchumi. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba Rais Obama anatafuta kuweka historia ya serikali yake kutoka katika uhusiano tete na Vietnam na...

Like
162
0
Wednesday, 08 July 2015
CHINA YAIDHINISHA HATUA KADHAA KUNUSURU SOKO
Global News

SERIKALI ya China imeidhinisha hatua kadhaa mwishoni mwa juma kulishinikiza soko ambalo limepoteza takriban asilimia 30 ya thamani yake katika wiki tatu zilizopita kurudi katika hali yake. Wawekezaji wengi wana wasiwasi na kwamba robo ya kampuni zilizoorodheshwa kuomba kusitisha kuuza hisa zao zinasababisha uwezo wa serikali kukopa unazidi kuwa katika hatari. Taarifa zaidi zinaonesha kuwa hali hiyo ni kama hatua ya kuzilinda kampuni hizo dhidi ya hasara zaidi ambapo kwa kipindi cha mwaka uliopita serikali ilifurahia uwekezaji katika soko la...

Like
199
0
Tuesday, 07 July 2015
AL SHABAAB WAKIRI KUHUSIKA NA SHAMBULIZI MANDERA,KENYA
Global News

WANAMGAMBO wa kundi la Al Shabaab wamekiri kuhusika na shambulizi lililotokea eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambapo watu 14 wameuawa usiku wa kuamkia leo. Taarifa za awali zimeonesha kuwa shambulio hilo lilikuwa na nia ya kuwalenga wafanyikazi wengi wa machimbo ya mawe wasiokuwa wenyeji katika maeneo hayo. Hata hivyo imeelezwa kuwa mashambulizi kama hayo yametishia kudumaza shughuli za maendeleo na kiuchumi katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambapo wengi wa wafanyikazi wake ni watu kutoka maeneo ya nje...

Like
248
0
Tuesday, 07 July 2015
ZIMBABWE KUPAMBANA NA UJANGILI KWA KUUZA TEMBO WAKE CHINA
Global News

MASHIRIKA ya kutetea maslahi ya wanyama nchini Zimbabwe yameonesha kushangazwa na hatua ya nchi hiyo kuuza Tembo kwa madai kwamba inahitaji fedha kwaajili ya kukabiliana na uwindaji haramu. Waziri wa mazingira  nchini humo amesema kuwa tembo hao walisafirishwa kwa ndege hadi China kwenye ndege binafsi ya mizigo huku wahifadhi wa wanyama wanasema wanyama hao wanahitaji uangalifu wa miaka kadhaa kutoka kwa wazazi wake. Tembo hao wataishi katika mbuga ya wanyama karibu na mji uliopo kusini mwa china– Guangzhou wakati taarifa...

Like
192
0
Tuesday, 07 July 2015
11 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO MANDERA,KENYA
Global News

JUMLA ya watu 11 wameuawa kufuatia shambulio lililotokea kaskazini mashariki mwa Kenya ambapo inahofiwa kuwa shambulio hilo lilikuwa na nia ya kuwalenga wafanyikazi wa machimbo ya mawe wasiokuwa wenyeji wa eneo hilo. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kuwa ilisikika sauti kubwa ya milipuko miwili kisha ikafuatiwa na milio ya risasi huku Shirika la msalaba mwekundu tayari limeshaanza jitihada za kuwaokoa majeruhi ambao idadi kamili haijulikani. Hata hivyo haijathibitishwa wahusika wa shambulio hilo ingawa kwa kipindi kirefu  wanamgambo wa...

Like
270
0
Tuesday, 07 July 2015
MKUTANO WA TATU KUJADILI MZOZO NA MKWAMO WA KISIASA BURUNDI WAANZA LEO DAR
Global News

MKUTANO  wa tatu wa dharura kujadili mzozo na mkwamo wa kisiasa nchini Burundi uliosababisha maelfu ya raia kuitoroka nchi hiyo umeanza leo jijini Dar es salaam. Viongozi hao wakiwemo mwenyekiti na mwenyeji wa jumuiya, rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na Yoweri Museveni wa Uganda, ambao tayari wamewasili kwenye kikao hicho, wanajadili na kuwasilisha mapendekezo ya ripoti mbili kuhusu mgogoro wa Burundi. Ripoti hizo ni pamoja na ya kikosi cha pamoja cha kimataifa cha Usuluhishi wa mgogoro wa Burundi, kinachojumuisha, Umoja...

Like
207
0
Monday, 06 July 2015
UGIRIKI WAPIGA KURA YA HAPANA
Global News

MAELFU ya raia wa Ugirik usiku wa kuamkia leo wametawanyika katika mitaa ya mjini Anthens karibu na jengo la bunge, wakifurahia kura ya hapana waliyoipiga ambayo imeshinda kwa ya asilimia 60. Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras,amesema matokeo hayo ya hapana, hayana nia ya kwenda kinyume na jumuiya ya Ulaya bali yataiongezea Ugiriki uwezo wa majadiliano zaidi kuhusiana na mzozo wa madeni. Tsipras ameongeza kuwa serikali ya Ugiriki iliitisha kura hiyo ya maoni ikiamini kuwa kura ya Hapana italeta makubaliano...

Like
189
0
Monday, 06 July 2015