Sports

GONZALO AKABIDHIWA JEZI NO 9
Slider

Nyota mpya wa klabu ya Juventus ya Italia Gonzalo Higuain amekabidhiwa jezi no 9 kwenye kikosi cha mabingwa hao wa ligi kuu ya Italia Serie A. Higuain mwenye umri wa miaka 28 amejiunga na Juventus kwa dau LA Euro million 94.7 akitokea Napoli pia ya Italia. Katika msimu uliopita nyota huyo amefunga magoli 36 akiweka rekodi hiyo kwenye ligi...

Like
332
0
Wednesday, 27 July 2016
ARSENAL YAPATA PIGO
Slider

Klabu ya Arsenal imepata pigo baada ya nyota wake Per Mertesacker kuripotiwa kuwa atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi 5 akisumbuliwa na maumivu ya jeraha la goti. Beki huyo sasa ameondolewa kwenye msafara wa kikosi kitakachokuwa ziarani nchini Marekani kujiandaa na msimu mpya wa ‪#‎epl‬ utakaoanza mwezi ujao. Kwa mantiki hiyo inapotiwa kuwa nyota huyo atakaa nje ya dimba hadi mwaka...

Like
343
0
Tuesday, 26 July 2016
SAKHO MGUU NDANI,MGUU NJE NDANI YA LIVERPOOL
Slider

Maisha ya mlinzi wa kati wa Liverpool Mamadou Sakho yanaonekana kuanza kuwa magumu baada ya kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp kuamuru nyota huyo arudi nchini England kutoka Calfonia Marekani ambapo timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya nchini England inayoanza kutimua vumbi mwezi ujao. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya uingereza kocha Jurgen Klopp hajafurahishwa na mwenendo wa kitabia wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 kwenye kambi yao huko Marekani nakuagiza...

Like
328
0
Tuesday, 26 July 2016
LALIGA: HUU NDIO MKWANJA ULIOVUNWA NA BARCELONA KATIKA MSIMU WA 2015/16
Slider

Machampion wa kandanda nchini Hispania klabu ya Fc Barcelona imetangaza kuvuna kitita cha Euro million 679 katika msimu uliopita 2015/16 wa ligi kuu ya huko ‪#‎Laliga‬. Katika makusanyo hayo yaliyovunja rekodi klabu hiyo imetangaza kupata faida ya Euro milioni 29 baada ya makato ya kodi. Katika hatua nyingine klabu hiyo imetangaza mipango yake ya upanuzi wa dimba la Camp Nue kwa siku za usoni kupitia faida...

Like
457
0
Tuesday, 26 July 2016
SPORTPESA YA KENYA KUDHAMINI KLABU YA EPL
Slider

Kampuni ya mashindano ya bahati nasibu inayodhamini Ligi Kuu ya Kenya imetia saini mkataba wa kuwa mdhamini wa klabu ya Hull City ya Uingereza. Kampuni hiyo ya SportPesa, ambayo huandaa mashindano ya kubashiri matokeo ya mechi nchini Kenya, imetia saini mkataba wa kudhamini Hull City kwa misimu mitatu. Klabu ya Hull City ilifanikiwa kurejea kwenye Ligi ya Premia msimu utakaoanza mwezi ujao. Hull City watafungua msimu kwa mechi ya nyumbani dhidi ya mabingwa Leicester City. Kwa mujibu wa taarifa kutoka...

Like
352
0
Monday, 25 July 2016
DEBI YA MANCHESTER YATIBUKA
Slider

Mechi ya kirafiki kati ya miamba wa Uingereza, Manchester City na Manchester United, imefutiliwa mbali kutokana na mvua kubwa. Mechi hiyo ilikuwa imepangiwa kuchezewa uwanja waBirds Nest, Uchina na ingekuwa ya kwanza kwa mameneja wapya Pep Guardiola na Jose Mourinho. Jumapili, Mourinho alikuwa amedokeza kwamba hali katika uwanja huo ilikuwa mbaya. Hata kabla ya mechi kuahirishwa rasmi, Guardiola alikuwa amesema matumaini yake ni kwamba wachezaji wake wasiumie. City na United wamesema “waandalizi wa mchuano huu pamoja na klabu zote mbili”...

Like
301
0
Monday, 25 July 2016
CAF YAPATA MDHAMINI MPYA
Slider

Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) limepata mdhamini mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kampuni ya mawasiliano ya Orange. Orange imekuwa mdhamini mkuu wa mashindano makubwa ya CAF kwa miaka minane tangu 2009. Kabla ya hapo, kampuni nyingine ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne. Sasa, mdhamini mpya atakuwa kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa. Kampuni hiyo itaanza kwa kudhamini michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2017 ambayo itaandaliwa nchini...

Like
460
0
Friday, 22 July 2016
POGBA AOMBA KUHAMIA MAN UNITED
Slider

Mshambulizi wa Ufaransa na Juventus Paul Pogba ameomba kuihama klabu hiyo ya Italia.Magazeti ya michezo nchini Italia yamechapisha habari hiyo kama kichwa kuwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23 ameomba aruhusiwe kuondoka kwani posho lake linavutia. La Gazzetta dello Sport liliongoza na kichwa ”Pogba ameamua kuondoka Juventus”Gazeti hilo linadai kuwa mfaransa huyo amekwisha kubaliana posho lake na Mashetani wekundu huku ikisisitiza kuwa sababu kuu iliyomfanya makamu wa mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Ed Woodward asiandamane na...

Like
311
0
Wednesday, 20 July 2016
TOM OLABA AAGANA NA RUVU SHOOTING BAADA YA KUIRUDISHA LIGI KUU
Slider

Kocha mkuu wa Ruvu Shooting, Mkenya Tom Alex Olaba aagana na uongozi wa klabu hiyo, akizungumza kupitia Sports headquarters Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwile amesema uongozi wa Ruvu Shooting umetoa pongezi zao pamoja shukrani kwa kocha huyo aliyeirudisha Ruvu Shooting kwenye ligi kuu aidha ameongeza kuwa kwa sasa klabu hiyo itaongozwa na kocha mzawa mwenye uzoefu na klabu...

Like
356
0
Tuesday, 19 July 2016
AZAM YAKANUSHA KUMTEMA JOHN BOCCO ‘ADEBAYOR’
Slider

Mtendaji mkuu wa Azam Fc, SADI KAWEMBA kupitia Sports Headquarters amekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kwamba mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’ ametemwa kikosini na kocha Mkuu wa klabu hiyo Mhispania, Zeben...

Like
292
0
Tuesday, 19 July 2016
NYUKI WALAZIMU MECHI YA KANDANDA KUAHIRISHWA
Slider

Mechi moja ya ligi kuu ya kandanda nchini Ecuador iliaahirishwa kwa dharura baada ya nyuki kuvamia uwanja. Amini usiamini mechi kati ya River Ecuador na Aucas katika jiji la Guayaquil ilisimamishwa baada ya nyuki waliokuwa wakipaa kutua uwanjani. Wachezaji kadhaa walidungwa na nyuki huku mashabiki wengi wakijeruhiwa. Wazima moto walilazimika kuingilia kati kujaribu kuwafurusha wadudu hao. Mechi hiyo iliyokuwa imechezwa kwa dakika kumi pekee ilisimamishwa kwa muda wa dakika 30 hivi, hata hivyo refarii katika mechi hiyo akaamua kuahirisha mechi...

Like
320
0
Monday, 18 July 2016