Sports

DEMBA BA AVUNJIKA MGUU UWANJANI
Slider

Mshambulizi wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Demba Ba amevunjika mguu akiwa uwanjani katika mechi ya ligi kuu ya Uchina. Raia huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 31 alikabiliwa na mlinzi wa timu hasimu katika ligi kuu ya Uchina hapo jana Jumapili tarehe 17 Julai. Ba ambaye anaichezea Shanghai Shenhua aligongwa na mchezaji wa timu hasimu ya Shanghai SIPG mita chache tu kabla ya kisanduku cha hatua 18, Alipoanguka mguu wake ulipinduka kwa hali isiyo ya kawaida...

Like
382
0
Monday, 18 July 2016
MEDEAMA WATUA YANGA KUIKABILI YANGA
Slider

Wapinzani wa klabu ya Young Africans, katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Medeama kutoka Ghana, wametua Dar es Salaam tayari kwa mechi baina ya timu hizo Jumamosi. Wachezaji hao waliwasili Dar Alhamisi na wakafanya mazoezi katika uwanja wa Karume. Yanga itaikaribisha Medeama kwa mchezo wa tatu kuwania taji hilo hatua ya makundi katika uwanja wa taifa Dar es Salaam. Mchezo huo utaanza saa 10.00 jioni Michezo miwili ya awali ya Yanga katika michuano hiyo ilikuwa ni dhidi...

Like
290
0
Friday, 15 July 2016
MAN UNTD NAMBARI 5 KWA UTAJIRI DUNIAN
Slider

Klabu ya Manchester United imeorodheshwa ya tano kwa utajiri duniani na jarida la Forbes, thamani yao ikiwa imepanda kwa asilimia saba. Klabu ya NFL, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake ikiwa $4bn (£3.03bn), na ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi kandanda kuongoza katika orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake 2011. United, walioongoza orodha hiyo 2011 na 2012, wana thamani ya $3.32bn (£2.52bn). Real Madrid ni wa pili kwa $3.65bn (£2.77bn) na Barcelona wa tatu $3.55bn (£2.69bn). United, klabu pekee...

Like
380
0
Thursday, 14 July 2016
JERRY MURO ABWAGA MANAYANGA, HUU NDIO UJUMBE WAKE
Slider

Kila nikizifikiria figisu za soka la bonge aisee nachoka kabisaa, let me walk away for a while though I will be missing my funs and my people wa kimataifa but I must walk away for a while...

Like
404
0
Wednesday, 13 July 2016
RONALDO AMBWAGA MESSI KWA MWAPATO 2015
Entertanment

Christiano Ronaldo ndiye mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes. Ronaldo ameorodheshwa katika nafasi ya 4 akiwa na jumla ya mapao ya dola milioni 88.($88m (£67m) Licha ya kuzoa taji la mchezaji bora duniani na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 kwa kukwepa kulipa kodi, mshambulizi wa Argentina na Barcelona ya Uhispania Lionel Messindiye mwanamichezo wa pili katika orodha hiyo. Messi ameorodheshwa katika nafasi ya 8 akiwa na mapato ya takriban dola milioni themanini na...

Like
458
0
Tuesday, 12 July 2016
EURO 2016: URENO YATWAA UBINGWA
Slider

Ureno wameshinda michuano ya kandanda ya Ulaya, Euro 2016, kwa kuwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika dakika za ziada kwenye mchezo wa fainali mjini Paris. Goli la ushindi lilifungwa na Eder katika dakika ya 110, na kusababisha huzuni kubwa kwa mashabiki wa Ufaransa waliofurika kwenye uwanja wa Stade de France. Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Ureno. Hii ni mara ya kwanza Ureno kushinda michuano mikubwa. Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano bila ya mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo aliyetoka kutokana...

Like
499
0
Monday, 11 July 2016
ICELAND WAPOKEWA KISHUJAA
Slider

Maelfu ya raia wa Iceland wamekusanyika katikati ya mji mkuu wa Reykjavik kukaribisha msafara wa timu yao ya taifa kwa mafanikio iliyopata kwenye michuano ya Kombe la mataifa Bingwa barani ulaya mwaka huu 2016. Wachezaji walipita katikati ya mji wakiwa ndani ya basi kubwa la wazi wakisindikizwa na ngoma hadi katika mlima wa Arnarholl ambapo mashabiki waliwasalimia kwa shangwe na makofi . Iceland ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza mashindano makubwa ya Kombe la mataifa barani Ulaya ilifikia ukingoni mwa...

Like
473
0
Tuesday, 05 July 2016
MCHEZAJI MWENYE ASILI YA DRC ATUA CHELSEA
Slider

Klabu ya Chelsea ya Uingereza imemsajili mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Michy Batshuayi amehamia Chelsea kutoka klabu ya Marseille ya Ufaransa na kutia saini mkataba wa miaka mitano. Mamake ni Viviane Leya Iseka na babake Pino Batshuayi. Michy alikuwa na fursa ya kuchezea timu ya taifa ya DR Congo kutokana na asili ya wazazi wake lakini mwaka jana aliamua kuwa mchezaji wa Ubelgiji. Aliwachezea mechi ya kwanza dhidi ya Cyprus Machi 2015 na kufunga bao....

Like
354
0
Monday, 04 July 2016
KOCHA WA UINGEREZA ROY HODGSON AJIUZULU
Slider

Saa chache tu baada ya timu ya kandanda ya Uingereza kubanduliwa nje ya mashindano ya mwaka huu ya Euro 2016, Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzulu wadhfa wake. Hodgson alikuwa ameshuhudiwa uingereza ikiambulia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Iceland katika mkumbo wa 16 bora huko ufransa. Kocha huyo mwenye umri wamiak 68 amekiongoza kikosi hicho cha Uingereza kwa miaka 4 sasa. Hodgson alichukuwa wadhfa huo kutoka kwa kocha muitaliano Fabio Capello aliyetimuliwa kufuatia matokeo duni. Hata hivyo kocha huyo...

Like
291
0
Tuesday, 28 June 2016
RAIS WA ARGENTINA AMSIHI MESSI ASIJIUZULU
Slider

Rais wa Argentina Mauricio Macri amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo Lionel Messi kwa lengo la kumuomba atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka la kimataifa. Messi alifikia maamuzi hayo baada ya timu yake kushindwa kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za Copa America huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliokosa mikwaju ya penalti. ”Amemwita na kumueleza namna anavyoona fahari kwa kiwango kizuri kilichoonyeshwa na timu yake katika michuano hiyo huku akimtaka asisikilize maneno ya watu” alisema msemaji wa...

Like
290
0
Tuesday, 28 June 2016
VARDY AKUBALI KUMWAGA WINO NA KUITUMIKIA TENA LEICESTER
Slider

Mshambuliaji wa Uingereza na Leicester Jamie Vardy amekubali kuweka kandarasi mpya na viongozi wa ligi ya Uingereza Leicester. Leicester imesema kuwa mchezaji huyo wa miaka 29 ambaye mabao yake yameisaidia klabu hiyo kushinda taji la ligi ya Uingereza msimu uliopita ameongeza kandarasi yake hadi miake minne na klabu hiyo. ”Pande zote mbili zinatumai tangazo hilo litamaliza uvumi wa hivi karibuni kuhusu hatma ya Jamie”,taarifa ya klabu imesema. Vardy alitarajiwa kununuliwa na klabu ya Arsenal kwa kitita cha pauni milioni 20...

Like
357
0
Thursday, 23 June 2016