Dakika 90 za mchezo wa mpira wa miguu kati ya E-fm Vs Calfornia Fc zilimalizika kwa E-fm kutetea ahadi yake ya kutembeza dozi kwenye michezo yote iliyosalia katika Muziki Mnene Bar kwa bar. Umati wa wakazi wa Boko wameshuhudia E-fm ikiwalaza Calfornia Fc magoli 2-1, huku bao la kwanza likifungwa kipindi cha kwanza ambapo Calfornia walisawazisha goli hilo kabla ya kwenda mapumziko. E-fm ilirudi na kasi ya ajabu katika kipindi cha pili licha ya Calfornia kulilinda goli lao kikamilifu juhudi...
MAHAKAMA ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC imeipa Afrika Kusini muda zaidi kutoa maelezo ni kwanini ilishindwa kumkamata Rais wa Sudan Omar al Bashir anayetakiwa na mahakama hiyo kujibu mashitaka ya uhalifu wa kivita wakati alipoizuru nchi hiyo mwezi Juni mwaka huu. Nchi hiyo ambayo ni mwanachama wa mkataba wa Roma, ina wajibu wa kuheshimu na kutekeleza maagizo ya mahakama ya ICC lakini serikali ya Afrika Kusini ilikataa kumkamata Bashir na kumruhusu kuondoka nchini humo kinyume na agizo la...
TAASISI isiyokuwa ya Kiserikali ya Twaweza inatarajia kuandaa mdahalo wa wagombea urais unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 0ktoba mwaka huu kwa lengo la kuwawezesha Wagombea waweze kutoa sera zao kwa Wananchi pamoja na kuruhusu Wananchi hao kuwauliza maswali Wagombea wao ili waweze kufanya maamuzi sahihi siku ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 Mwaka huu. Mkurugenzi wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema kuwa hadi sasa wamepata uthibitisho wa ushiriki wa vyama vine vya siasa ambavyo ni ACT- Wazalendo , Alliance for Democratic...
ALIYEKUWA mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe ambaye alikuwa anatetea nafasi hiyo kupitia chama cha Mapinduzi(CCM), amefariki kwenye ajali ya helikopta iliyotokea jana usiku kwenye hifadhi ya wanyama ya Selous lililopo eneo la Kilombero mkoani Morogoro. Filikunjombe ni mmoja wa abiria watatu waliokuwa ndani ya chopa hiyo ambao imethibitishwa kupoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jerry Silaa, Meya wa Manispaa ya Ilala anayemaliza muda wake, kapteni William Silaa baba mzazi wa Jerry ndiye aliyekuwa rubani...
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema Faini ya Pauni 50,000 aliyotozwa na chama cha soka cha England (FA) ni fedheha. Mourinho amepewa Adhabu hiyo ya faini pamoja na Kifungo cha Mechi 1 ambacho kimesimamishwa kwa kuchunguza mwenendo wake baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu kufuatia kauli yake kuhusu Refa Robert Madley mara baada ya kufungwa 3-1 na Southampton. Mourinho ameeleza pauni 50,000 ni fedheha, uwezekano wa kufungiwa Mechi 1 ni kitu cha kushangaza!” Mourinho pia alimchimba Meneja...
RAIS wa Marekani,Barack Obama ametangaza kuongeza muda wa majeshi ya Marekani kuwepo nchini Afghanistan. Takriban wanajeshi 10,000 wataendelea kubaki nchini humo kwa kipindi hasa cha mwaka ujao. Obama amesema vikosi vya Afghanistan havina nguvu bado ya kupambana na tishio linaloongezeka kutoka kwa wanamgambo wa Taliban....
WATU kadhaa wameuawa baada ya bomu kuripuka ndani ya msikiti katika mji wa Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria. Idadi kamili ya watu waliouawa bado haijajulikana lakini gazeti la Nigeria, Vanguard limearifu kwamba watu 26 wamekufa. Kwa mujibu wa waliolishuhudia tukio hilo, washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walijichanganya na watu waliokuwamo msikitini, Wameeleza kuwa mmoja wa washumbuliaji aliingia ndani ya msikiti na...
WANANCHI mkoani Iringa wametakiwa kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza. Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa utafiti na matumizi wa mamlaka ya hali ya hewa DR. LADISLAUS CHANG’A alipokuwa akitoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika shule za sekondari mwembetogwa na Efatha mkoani humo. Aidha ameongeza ili kuepukana na janga la mabadiliko ya hali hewa wananchi wanatakiwa kupanda miti mingi katika maeneo...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amekitumia Chama cha Siasa cha National League for Democracy (NLD) salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Mheshimiwa Dkt. Emmanuel Makaidi ambaye ameaga dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Lindi . Katika salamu zake hizo rais kikwete amesema kwa hakika, NLD imepoteza mhimili wake lakini pia Taifa limepoteza kiongozi mzuri na shupavu wa siasa katika kipindi ambacho alihitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote....
RAIS wa Marekani, Barack Obama ametangaza kuwa vikosi vya marekani vyenye silaha vimepelekwa Cameroon kusaidia mapambano dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram. Kikosi cha wanajeshi 300, kitafanya operesheni za upelelezi, kijasusi na operesheni za kipelelezi katika ukanda mzima. Cameroon na Chad zimekuwa zikilengwa na wanamgambo hao kutoka kaskazini mwa Nigeria na Obama amesema vikosi hivyo vitaendelea kubaki Cameroon mpaka watakapokuwa hawahitajiki...
VIJANA wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa kuwa mitandao ni jukwaa zuri lenye mitaji mingi ya biashara na endapo ubunifu utatumika vizuri kuna nafasi kubwa ya kutengeneza na kutoa ajira nyingi kwa kuwa ulimwengu unaendeshwa na TEHAMA katika Nyanja mbalimbali. Akizungumza na Efm Mjumbe wa Vijana Afrika Mashariki, na Mwenyekiti kutoka Mtandao wa Vijana Tanzania TYN Agness Mgongo amesema kuwa Vijana wa Kitanzania wanapata nafasi chache ya kushiriki katika midahalo ya kimataifa kwa kutofahamu au kuwa na matumizi sahihi...