UFARANSA imeanzisha mashambulizi mapya ya anga usiku wa kuamkia leo nchini Syria dhidi ya kambi ya mafunzo ya kundi la Dola la Kiislamu-IS na mashambulizi zaidi yatafuata. Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, amesema leo kuwa nchi hiyo imewashambulia wapiganaji hao, na haitakuwa mara ya mwisho. Wakati huo huo, taarifa zinaeleza kuwa mshauri wa kijeshi wa Iran, Jenerali Hussein Hamdani, ameuawa na wanamgambo wa IS nchini...
WAKATI kesho ni siku ya Kimataifa ya afya ya Akili duniani Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ina idadi ya watu takriban milioni 45 na kutokana na taarifa ya afya ya akili kwa mwaka 2014/15ambayo inaonyesha kuwa idadi ya watu 817,532 wanaugua magonjwa mbalimbali ya akili nchini, hii ni karibu asilimia 2 ya watanzania wote. Mkoa wa Dar-Es-Salaam unaongoza kwa kuwa n awagonjwa wengi nchini ukifuatiwa na mkoa wa Dodoma na mkoa wa mwisho ni Lindi. Taarifa iliyotolewa leo na...
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amewaasa wabunge wa Bunge la Msumbiji kufanya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao. Rais Kikwete ametoa ushauri huo wakati wa mazungumzo na Spika wa Bunge la Msumbiji Bibi Veronica Macamo ofisini kwake. Rais Kikwete amewaasa wabunge wasikubali nchi yao kuingia katika vita na badala yake wakae pamoja na kuweka makubaliano ambayo yatakubalika kwa vyama vyote na hatimaye kuwaepushia wananchi wa Msumbiji kuingia kwenye vita kwa mara...
UTAFITI mpya umeonya kuwa sigara ina uwezo wa kuua kijana mmoja kati ya vijana watatu nchini China. Hali hiyo itatokea kama hapatakuwa na hatua yeyote itakayofanyika itakayowafanya waache tabia hiyo. Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la Lancet linalohusiana na masuala ya tiba, unasema kuwa China inakabiliwa na ongezeka kubwa la vifo vya mapema kwa kuwa theluthi mbili ya vijana nchini humo huanza kuvuta sigara wakiwa chini ya miaka...
WASIWASI umezuka katika mji wa Calabar, kusini mwa Nigeria kutokana na mtu mmoja kufariki baada ya kuonyesha dalili zinazofanana na zile za ugonjwa wa Ebola. Shirika la usimamizi wa mambo ya dharura nchini humo limesema kuwa watu kumi wamewekwa karantini baada ya kugusana na mtu aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo. Shirika la afya duniani WHO lilitoa taarifa yake siku ya Jumatano kuwa nchi tatu zilizokuwa zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo ambazo ni Guinea, Sierra Leone na...
ZIKIWA zimesalia siku chache kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, wagombea mbalimbali wemeendelea kutoa ahadi zao kwa wananchi huku wengi wakisisitiza kufanyia mabadiliko mambo mbalimbali ikiwemo, elimu, viwanda na suala zima la kukuza uchumi. Mgombea ubunge wilaya ya kilolo kupitia chama cha mapinduzi -CCM ameahidi kufanya mabadiliko katika tarafa tatu wilayani humo na kuleta maendeleo ya kasi. Kwa uapnde wake, Mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA,...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Kimataifa ya Kuchunguza Jinsi ya Kugharimia Elimu Duniani. Tume hiyo, inayoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Gordon Brown ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Elimu Duniani ina jumla ya wajumbe 30, wakiwemo marais na mawaziri wakuu wa zamani, wataalum wa elimu, wafanyabiashara kutoka sekta binafsi na wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali duniani. Tume hiyo italenga...
Video ya wimbo wa Wiz Khalifa na Charile Puth “SEE YOU AGAIN” yafikisha watazamaji zaidi ya bilioni moja. Video hii si ya kwanza miongoni mwa video za muziki kufika kwenye kelele cha kuwa na watazamaji wengi ila muda uliotumika kufikisha kiwango cha idadi hiyo ni mchache zaidi ikilinganiswa na video nyingine. Puth alitweet kwenye akaunti yake ya twitter akitoa taarifa kuwa track hiyo ambayo ni Official soundtrack ya Fast and furious 7 imeingia rasmi kwenye top ten ya music video...
WABUNGE nchini Kenya wanakutana katika kikao cha dharura ili kujadili ni kwa nini serikali haina fedha. Malipo muhimu hayajafanywa na hivyo kuathiri wizara nyingi na huduma kwa umma pamoja na bunge lenyewe ambalo umeme umekatwa kwa siku kadhaa. Hatua hiyo imesababisha huduma za maji na usafi kuzorota na wabunge wanasema kuwa hali hiyo...
MAWAZIRI wa ulinzi wa Jumuiya ya kujihami ya Nato leo wanajiandaa kujadili iwapo waimarishe ulinzi wa kanda ya kusini ya ushirika huo wa kijeshi, kutokana na wasiwasi nchini Syria, baada ya kujiingiza kwa Urusi katika mgogoro huo hivi karibuni. Kabla ya mkutano huo mjini Brussels, Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema makanda wa kijeshi wamethibitisha kwamba jumuiya hiyo inauwezo na miundo mbinu inayohitajika kuliweka jeshi lake upande wa kusini na kubakia eneo...
BARAZA la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA limesema kuwa uamuzi wa Mwanasiasa nguli Nchini Kingunge Ngombale Mwiru kujitoa katika Chama cha Mapinduzi kwa madai kuwa CCM inahitaji mabadiliko ya mfumo ni ishara kuwa Taifa linahitaji mabadiliko ya ukweli na ya uhakika. Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Katibu wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Roderick Rutembeka amesema kuwa Mwanasiasa mkongwe huyo ameweza kuwatoa hofu Watanzania wote kuwa mabadiliko sio jambo geni nchini na kwamba kumekuwa na...