ZAIDI ya watu 60 wamefariki kufuatia kulipuka kwa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari katika jimbo la mashariki la Diyala nchini Iraq. Shambulio lingine la bomu limetokea katika mji wa kusini mwa Barsa ambao kwa kipindi kirefu haujakumbwa na mashambulizi ya mabomu huku maafisa usalama nchini humo wakisema bomu hilo lililotegwa katika mtaa wa Zubair limeua watu kumi. Hata hivyo kundi la kiislamu la –IS- limethibitisha kuhusika katika mashambulizi...
SERIKALI ya Kenya imemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta Jakaya mrisho Kikwete kwa kudumisha na kuboresha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. Taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es salaam inaeleza kuwa shukrani za Kenya zimetolewa na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta katika mazungumzo aliyoyafanya na Rais Kikwete nchini humo. Rais Kikwete yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu ambapo leo anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha mabunge mawili ya...
IMEELEZWA kuwa uwepo wa mfumo mpya wa utoaji leseni kupitia mtandao itawezesha kupunguza adha kubwa iliyokuwa ikikwamisha utoaji wa leseni kwa kipindi kirefu. Akizungumzia mfumo wa zamani Kamishna wa Madini nchini Mhandisi Paul Masanja amesema kuwa mfumo huo ulikuwa na changamoto nyingi kwa kuwa ulitegemea umahiri na uadilifu wa Afisa anayeshughulikia leseni hali iliyosababisha baadhi ya Waombaji kukosa leseni bila sababu za msingi. Kamishna Masanja ameongeza kwamba licha ya changamoto walizozipata waombaji wa leseni, Wizara pia ilikuwa na...
WATAFITI nchini kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoka sekta mbalimbali wameshauriwa kutunga sera zenye manufaa kwa lengo la kutambua umuhimu wa kutoa takwimu katika maamuzi. Akizungumza jijini Dar es salam Mkurugenzi wa Repoa Profesa Samwel Wangwe amesema kuwa kinachosababisha kuwepo kwa changamoto katika huduma za kijamii ni kukosekana kwa takwimu yakinifu. Profesa Wangwe amesema ili kukabiliana na tatizo hilo Repoa imeamua kukutana na wadau wa maendeleo wakiwemo watunga sera na mipango ili kuwajengea uwezo juu ya umuhimu wa kutumia...
IKIWA leo ni Siku ya Walimu Duniani, Shule nchini Kenya zimefunguliwa tena baada ya walimu kusitisha mgomo wao uliokuwa umedumu kwa wiki tano. Vyama viwili vinavyotetea walimu nchini humo vilitangaza mwishoni mwa wiki kwamba zitatii agizo la mahakama la kuwataka walimu warudi shuleni. Walimu takriban 280,000 walikuwa wamegoma kuishinikiza serikali iwalipe nyongeza ya mishahara ya asilimia 50 hadi...
NAIBU waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa ANGELLAH KAIRUKI amesema kuwa ni lazima kuweka umuhimu mkubwa katika kupanga, kutenga, kupima, kuendeleza na kusimamia maeneo ya Umma kwa kuzingatia sheria na mahitaji maalum na salama kwa watumiaji wakiwemo wanawake, watoto, wazee na watu wenye ulemavu. Mheshimiwa Kairuki ameiambia EFM leo kwenye maadhimisho ya siku ya makazi duniani yaliyoadhimishwa Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa ili kuhakikisha uwepo wa utumiaji salama wa maeneo ya umma hususani sehemu za ardhi...
WAKAZI wa Manispaa ya Morogoro leo wamelazimika kutembea kwa miguu na wengine kutumia magari ya mizigo pamoja na pikipiki kwenda kazini huku wanafunzi wakibaki katika vituo vya daladala baada ya madereva kugoma wakishinikiza jeshi la polisi kuwaachia huru baadhi ya madereva wanaoshikiliwa kwa siku sita mfululizo kutokana na makosa ya usalama barabarani. Wakizungumza na Efm, katika vituo mbalimbali vya daladala mkoani humo, wakiwemo wanafunzi na wanachi waliokwama kufika sehemu mbalimbali wamelalamikia serikali kushindwa...
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Mohamed Gharib Bilal amesema Shughuli za kibiashara zinahitaji utaalam, uwelewa na uwekezaji mkubwa wa kutambua nafasi za biashara zilipo, namna ya kutumia utaalam wenye ushindani katika soko pamoja na ushirikiano wa pamoja wa kuhusisha Watu hususani katika Makazi ambayo yanazidi kutanuka kutokana na shughuli za kiuchumi. Ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa mkutano wa kujengeana uwelewa juu wa uanzishaji wa biashara na ubunifu wa uendeshaji biashara ulio ratibiwa na...
SHANGWE za muzikimnene wa 93.7 EFM ,kwa mara nyingine tena ziliendelea ndani ya bagamoyo . Burudani ya aina yake ikiongozw anatimunzimaya EFM ilishushwandaniyamagetimiaAdon lodge. Wakazi wa bagamoyo walipata nafasi ya kukutana na watangazaji, na RDJ’s huku wakifurahia burudani ya pamoja. Muzikimnene bar kwa bar ulipambwana kabumbu kati ya EFM na Bagamoyoveterani ambapo Bagamoyo veteran waliibuka na ushindi wa bao moja huku EFM wakiambulia sifuri. Tangu kuanza kwa mechi hizi hii ni mara ya pili kwa 93.7 EFM kufungwa,mara ya kwanza...
WATU wapatao 15 wameuawa katika makabiliano kati ya waandamanaji na polisi kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura. Kiongozi wa Baraza la Haki za Binaadamu la nchi hiyo, Anschaire Nikoyagize, ameliambia shirika la habari la Ujerumani, DPA, kwamba kulikuwa na milio ya risasi kwenye mitaa ya Mutakure na Cibitoke, na hadi wakati huo walishapata maiti 15, ingawa idadi ilitazamiwa kuongezeka. Ghasia zimelikumba taifa hilo dogo la Afrika Mashariki, tangu Rais Pierre Nkurunziza kutangaza azma yake ya kuwania muhula wa tatu madarakani...
ZAIDI ya watu 130 wamefariki dunia baada ya maporomoko ya matope kukiangamiza kijiji kimoja, kando ya mji mkuu wa Guatemala. Taarifa iliyotolewa leo na mamlaka za nchi hiyo ya Amerika ya Kati, ikiwa ni siku ya tatu tangu janga hilo kutokea, zinasema idadi mpya ya waliopatikana wamekufa imefikia 131, huku wengine 300 wakiwa hawajuilikani walipo. Maporomoko yenye matope mazito yalikifunika kijiji cha El Cambray katika manispaa ya Santa Cantarina Pinula, na kuharibu nyumba 125, usiku wa...