UMOJA wa Afrika umesema mahakama maalumu itaundwa kwa ajili ya kuwashitaki washukiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sudani kusini ambapo imekumbwa na mzozo mkubwa tangu mwaka 2013. Hatua hii inalenga kuunga mkono hatua ya Afrika kushughulikia migogoro yao wenyewe. Uundwaji wa mahakama ni sehemu ya makubaliano ya Rais Salva Kiir na Kiongozi wa waasi, Riek Machar yaliyotiwa saini baada ya kuwepo shinikizo kutoka kwa viongozi wa...
WAUZAJI wa mboga mboga na matunda waliopo karibu na soko la Mjini Babati Mkoani Manyara, ambao wanauza bidhaa zao chini wametoa ombi kwa halmashauri ya mji huo kumalizia ujenzi wa soko jipya ili waweze kuhamishia bidhaa zao hapo. Wakizungumza wakati mwenge wa uhuru ukiweka jiwe la msingi kwenye soko jipya, wafanyabiashara hao wamedai wanakuwa na wakati mgumu kwani soko la sasa ni dogo na halitoshelezi mahitaji. Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela, amemweleza kiongozi wa mbio za...
IMEELEZWA kuwa inahitajika elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya suala zima la ugonjwa wa kipindu pindu na umuhimu uliopo kwa watanzania wote kudumisha hali ya usafi na kujiepusha na mambo yoyote ambayo yatapelekea kwa namna moja ama nyingine ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo. Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni MUSSA NATTY Amesema kuwa suala zima la kudhibiti ugonjwa wa kipindu pindu jijini linashindikana kutokana na watanzania wengi kutozingatia mambo muhimu ambayo yameelekezwa na...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametoa changamoto kwa Wabunge wa Bunge la Marekani kufunga masoko ya pembe za ndovu na faru duniani, kama njia yenye uhakika ya kukomesha ujangili dhidi ya wanyamapori katika nchi za Afrika na kwa haraka zaidi. Aidha, Rais Kikwete amewataka Wabunge hao kuzisaidia nchi za Afrika kifedha, ili kukomesha ujangili huo kwa sababu Wabunge hao tayari wameitangazia dunia kuwa wanazo fedha za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na majanga...
IDADI ya watu waliouwawa katika shambulio la anga kwenye sherehe ya harusi nchini Yemen imefikia watu 131, na kuaminika kuwa shambulio hilo ni baya kuwahi kutokea katika vita nchini Yemen. Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unafanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya waasi nchini Yemen umekanusha kuhusika na shambulio hilo huku msemaji wa muungano huo amesema wanamgambo wa eneo hilo huenda wameshambulia kwa makombora. makombora hayo yaliyorushwa jana...
NCHI ya Urusi imesema kuwa inatafakari uwezekano wake wa kuifuata Marekani ili kuwashambulia kwa ndege wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS). Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin ameyasema hayo baada ya kukutana na Rais wa Marekani Barack Obama kwenye maongezi ya nje ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN). Hata hivyo hotuba zilizotolewa na viongozi hao katika mkutano huo, ziliashiria mgawanyiko kuhusu jinsi ya kumaliza vita nchini Syria ambapo Urusi ilisema itakua “kosa kubwa” kutofanya kazi...
BODI ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imesema kuwa imeandaa miongozo ya utoaji huduma bora katika kufanikisha Mpango wa uwiano wa Itifaki ya pamoja kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki. Mkurugenzi wa ZFDB Dokta Burhani Othman Simai ameeleza hayo katika Mkutano wa wadau wa dawa Zanzibar ulioandaliwa na Mpango wa Udhibiti wa bidhaa za Chakula na Dawa wa Jumuia ya Afrika Mashariki. Katika mkutano huo dokta Simai amesema kuwa kuanzia sasa bidhaa zote za chakula...
JESHI la Wananchi wa Tanzania-JWTZ- leo limekabidhiwa Jengo litakalotumika kwa ajili ya Chuo cha Kijeshi cha kufundishia wataalamu wa Sayansi ya Tiba kwa kiwango cha Shahada lililojengwa kwa msaada na Serikali ya Ujerumani ili kuongeza idadi ya Madaktari Nchini. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Ulinzi Dokta Hussen Mwinyi amesema awali Jeshi hilo lilikuwa na chuo kinachofundisha matabibu kwa kiwango cha Cheti na Stashahada hivyo chuo hicho kitaweza kutoa elimu hiyo kwa kiwango cha kinachotakiwa. Kwa upande wake Balozi...
UMOJA wa Ulaya umesema utaanza kukabiliana na wafanyibiashara wanaowasafirisha wahamiaji kinyume na sheria katika bahari ya Mediterania. Taarifa kutoka Umoja huo zinaeleza kuwa upo uwezekano wa kuanzisha operesheni ambayo itaruhusu majeshi ya nchi wanachama kuingia, kufanya upekuzi na kuzuia boti ambazo zinashukiwa kuhusika katika biashara haramu ya kuwasafirisha wahamiaji kuanzia oktoba saba mwaka huu. Hata hivyo viongozi wa dunia waliopo katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wamezihimiza nchi za Umoja wa Ulaya kuwakaribisha wahamiaji na...
MAMIA ya wafungwa katika Gereza moja nchini jamuhuri ya Afrika ya kati wametoroka wakati ambapo kumekuwa na machafuko yaliyosababisha baadhi ya watu kupoteza maisha. Hali hiyo imekuja baada ya dereva wa gari ndogo muumini wa dini ya kiislamu kuuawa na kusababisha kuibuka kwa mapigano siku ya jumamosi kati ya wanamgambo wa kikristo na makundi ya kiislamu. Wafuasi wa wanamgambo wa kikristo wajulikanao kwa jina Anti-Balaka walishambulia gereza siku ya jumatatu na kuwatorosha mamia ya Wanajeshi na...
VIJANA nchini wametakiwa kutojihusisha na makundi hatari bila kuwa na kazi yoyote na badala yake wahakikishe wanajikita zaidi katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali ili waondokane na umasikini. Kauli hiyo imetolewa na Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini kupitia chama cha mapinduzi-CCM-Silvestry Koka alipokuwa akizungumza na vijana wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa tawi jipya la CCM jimboni hapo. Koka amesema kuwa baadhi ya vijana wanalalamika kutokuwa na ajira tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa husababishwa na wao kwa kutotaka...