WALINZI wa rais nchini Burkina Faso wamemkamata rais wa mpito Michel Kafando na waziri mkuu Isaac Zida na hivyo kuitumbukiza nchi hiyo katika hali ya wasiwasi wiki chache tu kabla uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu kuondolewa madarakani kiongozi wa zamani Blaise Compaore. Kukamatwa kwao kulisababisha maandamano ya barabarani nje ya ikulu ya rais ambako viongozi hao walikuwa wakizuiliwa. Milio ya risasi ilisikika wakati wanajeshi walipokuwa wakiwatawanya mamia ya waandamanaji na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameghadhabishwa...
SERIKALI ya Uturuki imesema itawaalika wawekezaji kutoka nchini humo ili waweze kutumia nafasi za uwekezaji zilizopo katika Hifadhi za Taifa nchini. Kauli hiyo imetolewa na balozi wa Uturuki nchini, Yasemine Eralp alipotembelea Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha na kukutana na viongozi wa shirika. Balozi Eralp amesema kuwa sekta ya utalii ni miongoni mwa vipaumbele vyake na kwamba atatumia muda wake mwingi kuhakikisha kuwa sekta hiyo inastawi na kuvutia watalii wengi nchini kutoka Uturuki huku akitoa nafasi kwa TANAPA kujitangaza...
MKUU wa kitengo cha manunuzi kutoka wakala wa barabara nchini (Tanroads) Mkoani Manyara, Raphael Chasama amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni1 kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi 7.4. Hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Babati, Bernadeta Maziku akisoma hukumu Mahakamani hapo amesema Disemba 22 mwaka 2009, bwana Chasama alishawishi kupewa rushwa kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na...
MTAALAMU wa uwindaji anayeshutumiwa kuhusika na kifo cha simba aliyepewa jina Cecil nchini Zimbabwe amekamatwa kwa tuhuma za kusafirisha swara 29 kimagendo nchini Afrika Kusini. Theo Bronkhorst anazuiliwa mjini Bulawayo na polisi wa nchini humo wamethibitisha. Bronkhorst anatarajiwa kusimamishwa kizimbani leo kwa kosa hilo la kusafirisha swara 29 kwa...
WANANCHI wa Kijiji cha Endanoga Wilayani Babati Mkoani Manyara, imeelezwa kuwa wamenufaika na mradi wa mashine ya kukamulia alizeti wenye thamani ya shilingi milioni 205 uliodhaminiwa kwa ushirikiano wa Serikali na wananchi. Mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela ameitaka jamii ya eneo hilo kuutunza mradi huo uliofadhiliwa na Wizara ya kilimo, chakula na ushirika iliyotoa shilingi milioni 197.9, Halmashauri ya mji shilingi milioni 3.2 na jamii shilingi milioni 7.9. Meela amesema mashine hiyo itatumika kuongeza uchumi wa jamii...
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa katika uongozi wake ametekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo huku pia, akitekeleza vizuri uongozi wake katika Serikali yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa kwa amani na utulivu. Dk. Shein ambaye ni Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa Kampeni wa chama hicho...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha bwana Casmir Kyuki kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria, na Bibi Sarah Barahomoka kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria. Kabla ya uteuzi huu, bwana Kyuki alikuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria na Barahomoka alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya uandishi wa Sheria. Uteuzi huo umefanyika jana na umeanza mara...
Meneja wa klabu ya Manchester Louis van Gaal ameekeza kuwa mlinzi Luke Shaw was alitolewa uwanjani akiwa anatokwa machozi kufuatia maumivu makali aliyoyapata baada ya kuvunjika mguu hivyo atalazimika kukaa nje kwa muda usiopungua miezi sita. Shaw, 20, aliwekewa hewa ya Oxygen kumsaidia wakati akipokea matibabu na kutolewa uwanjani kuelekea kwenye chumba cha kubadilisha mavazi Mchezo huo ulimalizika huku klabu ya Manchester ikikubali kupokea kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Psv.Memphis Depay alianza kuifungia timu yake bao la kwanza...
Timu za Uingereza za Man United na Man City zimeanza vibaya michuano ya kombe la klabu bigwa barani Ulaya baada ya kuchapwa. Man United wakiwa ugenini nchini Uholanzi wamelala kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Psv.Memphis Depay alianza kuifungia timu yake bao la kwanza kabla ya Héctor Moreno wa PSV kusawazisha kisha Luciano Narsingh akifunga bao la ushindi. Man City nao wakiwa katika Dimba lao la Etihad walikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa vibibi vizee ya Turin Juventus...
VYAMA kadhaa vya upinzani nchini Congo vimeitisha maandamano katika mji mkuu wa Taifa hilo Kinshasa juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu wa Urais uliotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka 2016. Wiki iliopita mahakama ya kikatiba nchini humo ilitaka siku ya uchaguzi huo kutangazwa upya hatua ambayo wapinzani wamesema ni ya kutaka rais Joseph Kabila kusalia madarakani zaidi hata baada ya kukamilika kwa muda wake uliowekwa kikatiba. Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani tangu baba ake aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo auwawe mwaka...
MALCOLM Turnbull ameapishwa kuwa waziri mkuu mpya wa Australia baada ya kuondolewa katika mamlaka kwa aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Tony Abbott. Turnbull aliyekuwa waziri wa mawasiliano katika serikali ya Abbott, sasa atakuwa waziri mkuu wa nne nchini humo tangu 2013 ambaye amesema kuwa huo ndio wakati bora zaidi wa kuwa raia wa Australia. Abbott, aliyeondolewa mamlakani Jumatatu baada ya kura ya haraka kufanywa katika chama tawala cha Liberal, amesema aliondolewa kwa “uchungu” lakini ameahidi kurahisisha shughuli ya mpito...