WANAFUNZI kote nchini wametakiwa kuwekeza katika elimu, pamoja na kufanya kazi kwa juhudi ili wanufaike katika maisha yao ya sasa na baadae sanjari na kuliletea Taifa maendeleo. Hayo yamesemwa na Mkuu wa utawala na uongozi wa chuo cha Habari maalum Ernest Karata wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha Full Bright college kilichopo Ngaramtoni wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Akizungumza katika mahafali hayo mkurugenzi mtendaji wa chuo hicho Julius Matiko amewaasa wahitimu kutumia elimu waliyoipata katika kuhakikisha wanatimiza...
MGOMBEA mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi-CCM-Samia Suluhu Hassan amesema kuwa endapo wananchi watakipa ridhaa chama hicho kuwaongoza kwa awamu nyingine atahakikisha anasimamia vyema rasilimali za Taifa. Samia ameyasema hayo wilayani Mkuranga, Kimanzichana wakati akizungumza na wananchi ikiwa ni moja ya ziara zake za kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Aidha Samia amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya tano ya –CCM- itaweka mikakati madhubuti ya kupambana na tatizo la rushwa...
RAIS wa Gabon Ali Bongo amesema kuwa kukamatwa kwa mkuu wa majeshi wa Taifa hilo mjini Paris mnamo mwezi Agosti mwaka huu ni jaribio la kuifedhehesha Gabon. Rais Bongo alikuwa akizungumza katika makao rasmi ya rais Francois Hollande baada ya kukutana naye mjini Paris. Mkuu huyo wa majeshi aliyekamatwa Maixent Accrombessi alizuiliwa kwa muda katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle kwa tuhuma za ufisadi baada ya kandarasi ya sare za kijeshi nchini Gabon kupewa kampuni moja ya Ufaransa...
JAJI mkuu wa Ghana . Georgina Theodora Wood amehutubia nchi kuhusu kashifa kubwa ya rushwa dhidi ya majaji na kuahidi kuchukua hatua na maamuzi ya haraka kuhusu madai dhdi ya majaji 34 wanaoshukiwa na kashifa hiyo. Hii ni mara ya kwanza tangu taarifa ya kashifa hiyo kutokea hali iliyosababisha Jaji huyo mkuu kuzungumza hadharani ambapo amesema kuwa idara ya sheria inapitia katika kipindi kigumu kutokana na maadili ya kisheria yaliyowekwa na wakongwe wa sheria kutetereka. Jaji huyo mkuu amesema kuwa...
VIJANA nchini wametakiwa kutumia vizuri mazingira yanayowazunguka katika kuibua mbinu mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kuondoka na Taifa tegemezi kwa kusubiri kuajiriwa mara baada ya kuhitimu masomo yao. Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Susan Ndunguru alipokuwa akifunga mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha yaliyofanyika Jijini Mwanza. Ndunguru amesema kuwa vijana waliopata mafunzo ya uwezeshaji wa stadi za maisha ni mabalozi ambao wana uwezo mkubwa wa kuweza kujenga Taifa lenye Afya nzuri, weledi...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Victoria Richard Mwakasege kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi ambaye kabla ya uteuzi wake alikuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi. Aidha, Rais Kikwete amemteua Msaidizi wa Rais wa Diplomasia, Balozi Samwel Shelukindo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa Rais Kikwete amemteua Zuhura Bundala kuwa Balozi na...
UMOJA wa mataifa umeelezea masikitiko yake dhidi ya mataifa kadhaa ya bara la Ulaya, namna yanavyozingatia sheria mbalimbali zinazokinzana kuhusiana na mipaka yake. Shirika linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, limeonya kuwa hatua hii itawaacha maelfu ya wakimbizi katika hali ya kutatanika kisheria. Shirika hilo la UNHCR, limesema kwamba muungano wa bara la Ulaya, unatakiwa kuandaa vituo vya kuwapokea wahamiaji, kuwaandikisha na kuwapiga msasa wahamiaji na wale wanaotafuta makao huko hasa wanaowasili nchini Ugiriki, Italia, na...
MAKAMANDA wa kijeshi kutoka pande mbili zinazopigana nchini Sudan Kusini wanakutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili njia za kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita. Mkutano huo utazungumzia masuala yakiwemo kuondolewa vikosi kutoka vitani, kubuni maeneo yasiyo chini ya ulinzi wa kijeshi na kuondolewa kwa wanajeshi wa kigeni kutoka nchini humo. Makubaliano ya amani yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita yakiwa na lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe hayakutekelezwa huku pande zote zikilaumiwa kwa kukiuka makubaliano...
MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA imefanikiwa kukamata dawa na vipodozi haramu vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 135, katika maeneo 243 kwenye Mikoa nane ya Tanzania Bara wakati wa Operesheni ya pili ya Giboia (Operesheni chatu) iliyofanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Agosti Mwaka huu. Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bwana Hiiti Sillo amesema baada ya uchambuzi na uchunguzi wa makosa kukamilika hatua mbalimbali zitachukuliwa pamoja na kuwapeleka Watuhumiwa mahakamani na kutoa adhabu kulingana na sheria ya chakula, Dawa...
IKIWA Zimepita siku tatu tangu kupigwa kwa Mwandishi wa habari wa magazeti ya Uhuru publications Limited UPL, CHRISTOPHER LISSA Katika ofisi za chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jukwaa la Wahariri Tanzania limewataka viongozi wa vyama vya siasa pamoja na mashabiki wa vyama hivyo kuacha vitendo vya kuwashambuliwa waandishi wa habari na kwamba vitendo hivi vikiendelea jukwaa litachukua hatua za kisheria dhidi ya vyama husika. Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jukwaa hilo ABSALOM KIBANDA amesema kuwa Jukwaa wamesikitishwa...
MAWAZIRI wa Mambo ya Ndani kutoka nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels katika mkutano wa dharura kujadili hali ya wakimbizi. Watajadili mapendekezo ya kuwapa makazi wakimbizi 120,000 katika sehemu mbalimbali za umoja huo waliowasili nchini Ugiriki, Italia na Hungary. Mawaziri hao watajadili pia kuanzishwa kwa vituo maalumu kuwasaidia, kuwasajili na kuwachunguza wakimbizi wanaowasili katika mataifa hayo matatu ya eneo la...