MISRI imesema jeshi lake la ulinzi limeua raia 12 kwa bahati mbaya,wakiwemo watalii kutoka Mexico wakati wa operesheni ya kupambana na ugaidi. Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imetuma kikosi kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo kwa upande wa Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto amekemea tukio hilo na ameitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi wa...
WATOTO kutoka mabaraza mbalimbali nchini wamekutana Jijini Dar es salaam kwa lengo la kujadili na kutoa maamuzi juu ya masuala muhimu waliyoyapendekeza awali kuingizwa katika Ilani za uchaguzi. Majadiliano hayo yametoa nafasi kubwa zaidi kwa watoto hao kuzichambua Ilani za vyama mbalimbali ambazo zinatumika katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Akizungumza katika mkutano huo mkuu wa kitengo cha habari kutoka shirika la kusaidia watoto la Save The Children– ELLEN OTARU OKOIDION amesema kuwa majadiliano hayo pia...
MAMLAKA ya chakula na dawa –TFDA, kanda ya kati imeteketeza zaidi ya tani tatu za shehena ya vyakula, vipodozi vifaa tiba na dawa zenye thamani ya shilingi milioni 38. 8 kufuatia msako mkali uliofanywa katika maduka yaliyoko Manispaa ya Dodoma na kubaini bidhaa hizo hazifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kumalizika muda wa matumizi pamoja na kuwa na kemikali zenye viambata vya sumu. Meneja wa TFDA Kanda ya Kati, Florent Kayombo amesema bidhaa hizo zimekamatwa kufuatia msako uliofanyika mwezi...
Mechi ya mpira wa miguu kati ya kikosi imara cha E-fm na Mlandizi Veteran umemalizika huku matokeo ya mchezo huo ya kiwa ni sare ya bila kufungana. Mchezo huo uliokuwa na hamasa ya hali ya juu kwakuhudhuriwa na wakazi wengi wa Mlandizi ambao hapo baadae watahudhuria kwenye party ya Muziki mnene bar kwa bar katika viwanja vya First Inn bar hapa Mlandizi mkoa wa pwani MATUKIO KATIKA PICHA...
Baada ya safari kukamilika kutoka Dsm hadi Mlandizi mkoa wa Pwani kikosi cha E-fm kiliwasili salama Mlandizi kikiwa tayari kabisa kukipiga na timu ya Mlandizi Veteran kabla ya kuanza kwa sherehe za Muziki Mnene bar kwa bar eneo la Firdt Inn bar. MATUKIO KATIKA PICHA ...
UCHUNGUZI uliofanywa Nchini Ghana, na mwandishi habari za uchunguzi , Anas Aremeyaw Anas uliomchukua miaka miwili umegundua kuwa majaji pamoja na viongozi wa juu wa mahakama nchini humo wanakula rushwa . Anas tayari amekwisha waandikia waraka Rais wa nchi hiyo pamoja jaji mkuu ambao nao tayari wamekwisha andaa tume ya kuwahoji majaji wote wanaotuhumiwa. Anes, Mwandishi wa habari za uchunguzi, ambaye pia ni mwanasheshia aliwafuata majaji kuwapa hongo ili wawaachie huru watuhumiwa. Katika maeneo mengine alijifanya mwenye kushitaki ili atoe...
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, leo anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi zinazomkabili zitakapoanza kusikilizwa. Katika kesi ya kwanza ambayo inamkabili Gwajima peke yake, anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. Kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo kunatokana na upelelezi wa kesi hiyo kukamilika na mshitakiwa kusomewa maelezo ya...
MWENYEKITI wa chama cha walimu nchini (CWT) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Abraham Kisimbi amesema atawatetea walimu wa wilaya hiyo ambao wanadai serikalini fedha zao ikiwemo kurudishiwa asilimia 15 ya fedha zao. Akizungumza baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Kisimbi ameeleza kuwa walimu wa wilaya hiyo wana changamoto kubwa ikiwemo kutopandishwa daraja kwa muda mrefu, hivyo amesema atatumia nafasi hiyo kutetea haki...
BARAZA kuu la Waislamu Tanzania-BAKWATA, linafanya Mkutano Mkuu leo mjini Dodoma huku ajenda kuu ikiwa ni kumchagua mfti mkuu wa Tanzania. Mufti atakayechaguliwa atakuwa ni wa awamu ya tatu, baada ya kutanguliwa na Mufti Hemed Bin Jumaa bin Hemed na Mufti Issa Bin Simba aliyefariki dunia Juni 15 mwaka huu. Hivi sasa nafasi hiyo inakaimiwa na Shekh Abubakari Zubery ambaye pia ameingia katika miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo ambayo ni ya juu katika Baraza hilo akichuana na Ally Muhidin Mkoyogole,...
JESHI la anga la Ufaransa limeanza kurusha ndege za upelelezi katika anga ya Syria kukusanya data katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Dola la Kiislamu. Waziri wa mambo ya kigeni ya Ufaransa Laurent Fabius amesema kuwa ndege hizo zinaamua muda muafaka na hatua za kuchukuliwa dhidi ya wapiganaji wa IS. Australia leo imetangaza kujiunga na mashambulizi ya anga nchini Syria, na itawachukua wakimbizi elfu 12,000...
KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekosoa jinsi bara la Ulaya linavyoshughulikia mzozo wa sasa wa Wahamiaji. Amesema hali imefikia katika kile alichokiita , ishara ya aibu” kutokana na tofauti zilizopo kimataifa. Jana Jumanne, wahamiaji kadhaa, ikiwa ni pamoja na familia zilizo na watoto, wamelazimisha kupita vizuwizi vya polisi katika kambi ya kuandikishwa katika mpaka wa Hungary na ...