Slider

WATANZANIA WAMEAMUA KUWEKA SILAHA CHINI NA KUIUNGA MKONO TAIFA STARS
Slider

Kikosi imara kabisa cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars siku ya jumamosi kilishuka dimbani katika uwanja wa taifa wa Daresalaam kukipiga na timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagle Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana huku stars ikionyesha kiwango cha juu kabisa cha uchezaji MATUKIO KATIKA PICHA Mashabiki wa Stars Supporters wakisherehekea timu yetu kuipa...

Like
320
0
Monday, 07 September 2015
KESI YA HABRE KUANZA LEO
Global News

KESI inayomkabili aliyekuwa rais wa Chad, Hissène Habré dhidi ya uhalifu kwa binadamu, kivita na mateso, inaanza kusikilizwa leo Jaji wa mahakama ya Burkinabe, Gberdao Gustave Kam ataamua iwapo kesi hiyo itaendelea bila upande wa utetezi wa Hissene Habre. Tangu mwanzo wa utaratibu wa kesi hiyo, Hissene Habre, mwenye umri wa miaka 72 amekuwa akikataa kutambua uhalali wa mahakama maalum ya Afrika, ambayo iliundwa na Umoja wa Afrika mwaka 2013, ili kushugulikia kesi yake nchini...

Like
265
0
Monday, 07 September 2015
UTAFITI KUCHUNGUZA JINSI MTU ANAVYOZEEKA
Global News

WANASAYANSI mjini London wamegundua utafiti mpya wa kuwezesha kuchunguza utaratibu wa jinsi mtu anavyozeeka kwa kutumia tabia ya zaidi ya mamia ya vinasaba vya damu, ubongo na seli za misuli. Wanasayansi hao wameambatanaisha matokeo ya watu wenye afya nzuri wenye umri wa miaka 63 na zile za vijana kutengeneza mpagilio wa kufuatilia ili kuweza kuzeeka kwa Afya zaidi. Aidha wamegundua katika baadhi ya kesi zinazohusu watu kuzeeka kwa zaidi ya miaka 15 na umri wao halisi kwani utafiti huo utasaidia...

Like
246
0
Monday, 07 September 2015
MBAO ZAPANDA BEI
Local News

IMEBAINISHWA kuwa kutokana na kufungwa kwa Hesabu ya mapato ya mwaka 2014 kumesababisha ugumu wa upatikanaji wa mbao hali inayochangia bidhaa hiyo kuuzwa kwa bei ya juu. Wakizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam wafanyabiashara wa mbao wamesema kuwa kuanzia mwezi june hadi sasa zimekuwa zikipatikana kwa shida kwenye misitu ikilinganishwa na kipindi kilichopita. Wafanyabiashara hao wamebainisha  kuwa  bei inapo kuwa juu inasababisha hata mwananchi wa kawaida kushindwa kununua  kwa sababu ya gharama zake....

Like
543
0
Monday, 07 September 2015
AZAKI YAZINDUA ILANI YA UCHAGUZI
Local News

ASASI za kiraia nchini–AZAKI-imezindua ilani inayoakisi malengo yatakayoinufaisha jamii katika kipindi cha kuelekea na baada ya uchaguzi mkuu ujao ambayo itakuwa dira na mwongozo kwa wananchi na vyama vyote vya siasa. Akifungua hafla hiyo ya uzinduzi jana katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu Bahame Tom Nyanduga amesema lengo la asasi hiyo ni kuhakikisha kunakuwa na kampeni za Amani na  uchaguzi usio wa vurugu. Aidha Nyanduga ameongeza kuwa tume imejipanga...

Like
305
0
Monday, 07 September 2015
MUZIKI MNENE BAR KWA BAR MKURANGA
Entertanment

Muziki mnene Mkuranga sherehe zilianza na ufunguzi wa mechi ya mpira wa miguu kati kikosi bora kabisa cha E-fm na Mkuranga Veteran ambapo mchezo huo ulimalizika kwa E-fm kuichabanga Mkuranga Veteran bao moja kwa sifuri, huku goli hilo la efm likiwekwa nyavuni na Rdj X five baada ya kupata pasi nzuri kabisa kutoka kwa John Makundi. Baadae moto wa burudani uliwaka pale High Way bar kwa kuwakutanisha wafanyakazi wa efm na mashabiki wake pamoja na wadau wa redio yetu Mkuranga...

Like
736
0
Monday, 07 September 2015
IOC KUFADHILI MICHEZO KWA WAKIMBIZI
Slider

Shirikisho la michezo ya Olimpiki, IOC, leo limetangaza hazina ya dola millioni mbili, ambazo zitatolewa kwa Kamati ya Kitaifa ya olimpiki ya nchi wanachama kufadhili miradi itakayowasaidia wakimbizi katika mataifa yao. Rais wa IOC, Thomas Bach, amesema kuwa kama shirikisho la michezo ya olimpiki, imehuzunishwa na habari zainazowahusu wakimbizi, katika siku za hivi karibuni. Amesema IOC imekuwa ikifuatilia matukio yanayojiri katika eneo la Mashariki ya Kati, Afrika na Ulaya na wao wanataka kutumia michezo kuwaleta wanainchi pamoja, hasa...

Like
272
0
Saturday, 05 September 2015
ZAIDI YA WATU 50 WAHOFIWA KUFA MAJI LIBYA
Global News

ZAIDI ya watu hamsini hawajulikani waliko baada ya meli walimokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Libya.   Msemaji wa shirika la kimataifa ya uhamiaji amesema kuwa wahamiaji wengine waliokuwa kwenye meli hiyo waliokolewa na wanajeshi wa majini wa Italia na wamepelekwa kisiwa cha Lampedusa.   Mwili wa mhamiaji mmoja pia uliopolewa baharini na kupelekwa katika kisiwa hicho.   KWINGINEKO, INAELEZWA kuwa Watu 1,000 nchini Sierra Leone wamewekwa kwenye karantini baada ya kugunduliwa kuwa mwanamke wa umri wa miaka 67 alifariki...

Like
188
0
Friday, 04 September 2015
WATATU MBARONI KWA WIZI WA VIFAA VYA TRANSFOMA DAR
Local News

SHIRIKA la umeme nchini TANESCO kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamewakamata watu watatu wanaohusika na kuiba vifaa muhimu katika TRANSFOMA  mbili za wilaya ya Ilala na kupelekea wakazi wa maeneo hayo kukosa huduma ya umeme. Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Tanesco, Ilala ATHANASIUS MANGALI, Amesema kuwa kumekuwa na wizi wa vifaa muhimu katika transfoma ambavyo vinapelekea kifaa hicho  kushindwa kusambaza umeme ipasavyo. Amesema Tanesco kwa msaada wa karibu kutoka  jeshi la polisi jana majira ya usiku wameweza...

Like
361
0
Friday, 04 September 2015
TFDA YAZINDUA SEHEMU YA MAABARA YA UCHUNGUZI WA DAWA
Local News

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania -TFDA imezindua sehemu muhimu ya maabara ya uchunguzi wa dawa ijulikanayo kama Microbiology Laboratory ambayo imelenga kutumika kwa ajili ya kuchunguza vijidudu  hatarishi kwa afya ya binadamu kwenye chakula, dawa, vifaa tiba pamoja na vipodozi. Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo HIITI SILLO, amesema kuwa uchunguzi utakaofanyika katika maabara hiyo utakidhi vigezo vya uchunguzi wa kimataifa kwa mujibu wa viwango vya...

Like
389
0
Friday, 04 September 2015
UTAFITI UNAONYESHA WANANCHI WANAHINAHITAJI GESI KUBORESHA MAISHA NA HUDUMA ZA JAMII
Local News

UTAFITI wa maswala ya gesi uliofanywa na taasisi ya utafiti ya REPOA kwa kushirikiana na kituo cha maendeleo duniani umeonyesha kua Watanzania wanahitaji gesi iweze kuchimbwa ili isaidie kwenye kuboresha maisha na huduma za jamii.   Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam baada ya kuwasilisha Ripoti ya utafiti huo mtafiti kutoka kituo cha maendeleo duniani Mujobi Moyo amesema Watanzania wengi wametaka gesi iwe ni sababu ya kuboresha huduma za afya, huduma za elimu, kuboresha miundombinu pamoja na...

Like
255
0
Friday, 04 September 2015