WAZAZI nchini wameshauriwa kujenga utamaduni wa kuwawekea watoto wao bima za elimu ili ziweze kuwasaidia kutimiza ndoto zao badala yakusoma huku wakiwa na wasiwasi wa karo na kufukuzwa shule. Wito huo umetolewa leo na Afisa mipango fedha kutoka kampuni ya Alliance life Assurance ambayo inayojishughulisha na masuala ya bima ya maisha na elimu, ANNY MUSHI ambaye amesema kuwa endapo familia zitakuwa na mwamko wakuwekea watoto wao bima ya elimu kuna uwezekano mkubwa familia nyingi zikamudu gharama za elimu...
JAMII imetakiwa kuzingatia usafi wa mwili, chakula na mazingira yanayowazunguka kwa kuwa hali ya usafi jijini Dar es salaam na mikoa jirani sio ya kuridhisha kufuatia mlipuko wa Kipindupindu kuendelea kusambaa kwa kasi ambapo hadi sasa idadi ya Wagonjwa waliopokelewa vituoni imefikia 385 huku Mkoa wa Pwani ukiripotiwa kuwa na wagonjwa saba na kifo cha Mtu mmoja. Hayo yamesemwa leo jijjini Dar es salaam wakati wa makabidhiano ya msaada wa nyenzo za ziada za box 1,000 ya dawa za waterguard...
UTAFITI mpya uliyofanywa na shirika la utafiti wa safari za anga la Marekani NASA, unaonyesha kuwa kuongezeka kwa kina cha maji baharini kwa zaidi ya mita moja katika kipindi cha miaka 100 hadi 200 ijayo hakuzuwiliki. Kuongezeka huko kunatishia kuyazamisha maeneo na miji mikubwa duniani iliyoko chini ya usawa wa kina cha bahari kama Tokyo na Singapore. Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha utafiti cha NASA Michael Freilich, zaidi ya watu milioni 150, wengi wao kutoka bara la Asia,...
WACHUNGUZI wa Uholanzi wamesema ripoti ya mwisho kuhusu kuangushwa kwa ndege ya Malaysia MH17 katika anga ya mashariki mwa Ukraine mwaka uliyopita itatolewa Oktoba 13. Bodi ya usalama ya Uholanzi imesema katika taarifa kuwa iliwafahamisha ndugu wa wahanga na wawakilishi walioruhusiwa kwenye uchunguzi wa chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo, juu ya tarehe ya kutolewa kwa ripoti hiyo. Bodi hiyo imesema kabla ya kutolewa rasmi kwa ripoti hiyo, ndugu wa wahanga watafamishwa kuhusu ugunduzi wa uchunguzi huo katika mkutano wa...
soko la samaki kwa sasa limepanda kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hali inayochangia kuuzika kwa bei ya juu tofauti na miezi iliyopita. Akizungumza na Efm makamu mwenyekiti umoja wa wauza samaki -UASADA katika soko la samaki feli Bwana CHARLES MUSSA amesema kuwa mbali na mabadiliko ya hali ya hewa kuchangia kupatikana kwa samaki hao lakini pia hali hiyo inasababishwa na uhaba wa vifaa vya kuvulia. MUSSA amebainisha kuwa kutokana na kutopatikana kwa wingi samaki hapa nchini, wanalazimika kuagiza...
WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam wamesema hivi sasa wanahitaji mabadiliko kutoka kwa viongozi wanaotarajia kuingia madarakani ili jamii iweze kuwaamini. Wakizungumza na EFM katika nyakati tofauti wananchi hao wamesema hawatawafumbia macho viongozi wanaodiriki kuwalaghai wananchi kwa kuwapa fedha na vitu mbalimbali kwa lengo la kuwachagua na kuwaomba watu wote kuwa makini na kumpata kiongozi bora na mwadilifu. Aidha wamesema hali ngumu ya maisha ndio inayopelekea wananchi kujiingiza katika kupokea pesa na vitu mbalimbali vya ushawishi ili...
Kamati itakayoamua ikiwa mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, anapaswa kuachiliwa kutoka gerezani, inatarajiwa kukutana tarehe 18 mwezi ujao. Waziri wa haki nchini humo, alizuia mwanariadha huyo kuachiliwa siku ya Ijumaa wiki iliyopita kama ilivyokuwa imetarajiwa. Waziri huyo amesema kuwa uamuzi wa kamati hiyo ya kutoa msamaha wa kumuachilia mwanariadha huyo, baada ya kutumikia kifungo cha miezi kumi ya kifungo chake cha miaka mitano ulitolewa mapema na haina msingi wowote. Mahakama nchini humo ilimpata Pistorius na hatia ya kuua...
LEO zimetimia siku 500 tangu wanafunzi zaidi ya 200 wa kike walipotekwa nyara na kundi la kigaidi la Boko Haram kutoka mji cha Chibok kaskazini-mashariki mwa Nigeria, huku matumaini ya kupatikana kwa wanafunzi hao yakizidi kufifia. Kumbukumbu hiyo inafanyika wakati hali ya usalama ikizidi kuwa mbaya katika eneo hilo, ambako Boko Haram wamezidisha mashambulizi tangu kuingia madarakani kwa rais Muhammadu Buhari, ambapo wameuwa zaidi ya watu 1,000 katika miezi mitatu. Wapiganaji hao walivamia shule ya serikali mjini Chibok...
MAREKANI imemuonya rais wa Sudan Kusini Salva Kirr, kuheshimu na kutekeleza mkataba wa amani aliousaini jana mjini Juba. Rais Kirr, alikuwa amekataa kusaini mkataba huo wiki iliyopita mjini Adis Ababa Ethiopia. Lakini, licha ya kusaini mkataba huo, ameelezea wasi wasi wake kuhusiana na masuala kadhaa ya mkataba huo, hasa kugawana madaraka na waasi....
SERIKALI kupitia Sekretarieti ya ajira utumishi wa umma imeanza kutumia mfumo wa kupokea maombi ya kazi kupitia njia ya mtandao unaotambulika kwa jina la POTO ili kuwapa urahisi waombaji wa kazi katika nafasi mbalimbali. Akizungumza na EFM Jijini Dar es Salaam Afisa habari wa sekretarieti ya ajira kwa utumishi wa umma Kassim Nyaki amesema mfumo huo wa kimtandao ndio njia rahisi ambayo inatumika kutoa matangazo ya nafasi za kazi...
WATU tisa wa familia moja wamefariki dunia kwa kuteketea na moto baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi iliyoko maeneo ya Buguruni Malapa kuteketea kwa moto na kusababisha vifo vyao papo hapo Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa mtaa wa Malapa KARIMU MAHMUDU amesema kuwa moto huo ulianza majira ya saa tisa ndani ya nyumba hiyo na kusababisha vifo vya watu tisa ikiwemo watoto wanne ambao walijulikana kwa majina ya AHMEDI, ABDULLAH, AISHA, ASHRAFU, Mama wa watoto hao aliyejulikana kwa jina...