Slider

LAMORDE AKANUSHA UFISADI NIGERIA
Global News

MKURUGENZI mkuu wa shirika la kupambana na ufisadi nchini Nigeria-EFCC– Ibrahim Lamorde amekanusha madai kuwa zaidi ya dola bilioni tano zimetoweka kutoka kwa hazina ya shirika hilo. Lamorde amesema kuwa hata fedha zilizokusanywa na –EFCC- zikijumuishwa na ufadhili wote unaotolewa na shirika hilo, haziwezi kufika dola bilioni tano kwa pamoja. Aidha ameliambia shirika la utangazaji la BBC kuwa madai hayo hayana msingi na yananuia kumharibia sifa, kwa sababu EFCC kwa sasa bado inamchunguza mtu aliyetoa madai...

Like
237
0
Thursday, 27 August 2015
NKURUNZIZA KUPAMBANA NA MAUAJI
Global News

KATIKA hotuba yake aliyoitoa kwa taifa zima rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameonyesha hisia zake kuhusu kujumuisha vikosi vya ulinzi na usalama nchini humo. Hayo yamekuja wiki moja baada ya Rais huyo kuapishwa kushika nafasi ya Urais wa nchi hiyo kwa muhula mwingine huku wakasoaji wakisema kuwa ni kinyume cha Katiba ya nchi hiyo. Rais Nkurunziza amezitaka kamati za ulinzi na usalama kufanya kazi usiku na mchana ili kupambana na kile alichokiita kundi la watu wachache wanaofanya mauaji na kusababisha...

Like
248
0
Thursday, 27 August 2015
MASHEKHE NA WALIMU WA MADRASA WAMETAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUPENDA AMANI
Local News

MASHEKHE na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwahamasisha Wananchi kupenda Amani ili waepuke kujiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu.   Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi alipokuwa akifungua mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.   Katika mkutano huo Sheikh Omary amesema Masheikh na Walimu hao ndio Wasimamizi wakuu wa Amani katika maeneo mbalimbali ikiwemo Miskitini na hata ndani ya Nyumba...

Like
407
0
Thursday, 27 August 2015
SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA MAKUZI NA MALEZI YA WATOTO
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza makuzi na malezi ya watoto katika familia ili kujenga Taifa lenye watu wenye maadili. Akifungua kongamano la wadau wa haki za watoto Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dokta Pindi Chana amesema Serikali inashughulikia marekebisho ya kisera na mipango zilizopo ili kukuza upatikanaji wa haki za watoto nchini.  Kongamano la wadau wa malezi na makuzi ya familia limefanyika muda ambao mpango wa utekelezaji wa malengo ya milenia unafikia ukingoni,...

Like
260
0
Thursday, 27 August 2015
COENTRAO KUTUA MONACO KWA MKOPO
Slider

Real Madrid na Monaco zimekubaliana dili la beki wa kushoto wa Rea Madrid mreno  Fabio Coentrao kwenda kuitumikia Monaco kwenye Ligue 1 kwa mkopo katika msimu wa mwaka 2015-16. Klabu hizi mbili zilitangaza makubaliano hayo siku ya jumatano Coentrao, 27, alijiunga na Real Madrid akitokea Benfica mwaka 2011 kwa ada ya Euro milioni...

Like
220
0
Thursday, 27 August 2015
MAN U YAILAZA BRUGGE 4-0
Slider

Katika muendelezo wa mechi za mkondo wa pili kufuzu kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, usiku wa kuamkia leo timu kadhaa zilishuka dimbani kutafuta tiketi ya kuingia katika hatua ya makundi. Manchester Utd imefanikiwa kusonga mbele kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Club Brugge na kufanya matokeo kuwa 7-1, katika mikondo yote miwili. Katika mchezo huo nahodha Wayne Rooney alidhihirisha kuwa bado yupo vizuri katika kucheka na nyavu, baada kufunga mara tatu. Droo...

Like
197
0
Thursday, 27 August 2015
BEIJING: WANARIADHA 2 WA KENYA WAPEWA MARUFUKU YA MUDA
Slider

Wanariadha wawili wa Kenya wamebainika kwamba walitumia dawa za kusisimua misuli katika mashindano yanayoendelea ya IAAF mjini Beijing. Wawili hao Koki Manunga na Joyce Zakary wamepewa marufuku ya mda baada ya kutumia dawa hizo kulingana na IAAF. Wanariadha hao wa mita 400 walilengwa kabla ya kushiriki katika mbio hizo katika hoteli yao mnamo tarehe 20 na 21 Agosti kulingana na taarifa hiyo ya...

Like
209
0
Wednesday, 26 August 2015
MSCHANA WA MIAKA 16 AKIRI KUTEKELEZA UGAIDI UINGEREZA
Global News

MSICHANA mmoja mwenye umri wa miaka 16 amekiri kutekeleza ugaidi katika mahakama moja ya mjini Manchester Uingereza. Msichana huyo ambaye jina lake haliwezi kutajwa amekiri kumiliki vilipuzi na maelezo ya kutengeza bomu. Kukamatwa kwake mnamo mwezi Aprili kunafuatia uchunguzi na kitengo cha kukabiliana na ugaidi cha kaskazini magharibi. Alikamatwa pamoja na mvulana mmoja wa miaka 14 kutoka eneo la Blackburn ambaye amekiri kuhusika katika njama ya kuwashambulia polisi katika gwaride nchini Australia....

Like
224
0
Wednesday, 26 August 2015
UMABWILA: VYAMA VYA BODABODA HAVIFUNGAMANI NA SIASA
Local News

UMOJA wa madereva wa bodaboda wilaya ya IIala (UMABWILA) wamesema kuwa vyama vya bodaboda havifungamani na siasa na kila mwanachama anahaki ya kupenda na kushabikia chama chochote cha siasa. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Makamu mwenyekiti  wa Umoja huo, BASHIRU KASHAIJA amesema kuwa watashirikiana na chama ambacho kimesaidia kuwezesha bodaboda kuwa chombo rasmi cha...

Like
236
0
Wednesday, 26 August 2015
BAWACHA KUFANYA UZINDUZI WA KAMPENI YA WANAWAKE KESHO
Local News

BARAZA la Wanawake la chama cha Demokrasia na Maendeleo-BAWACHA- linatarajia kufanya uzinduzi wa kampeni ya Wanawake wa chama hicho kupitia kongamano linanalotarajia kufanyika  kesho Agosti 27 jijini Dar es salaam.   Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza hilo Halima Mdee amesema kongamano hilo linalengo la kuwaunganisha wanawake ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 na hatimae kufikia lengo la la idadi ya asilimia hamsini kwa hamsini hasa ikizingatiwa kua wanawake ndio...

Like
226
0
Wednesday, 26 August 2015
WADAU WAKUTANA KUTAHMINI NA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA YA AFYA
Local News

KATIKA kuboresha huduma za afya nchini Wadau mbali mbali wa maswala ya afya wamekutana kutathmini  utoaji huduma na kutazama namna ya kuboresha utoaji huduma za afya kwa Watanzania.   Wadau hao wamekutana katika kongamano la tano la kitaifa la kuboresha huduma za afya  lililoanza leo jijini Dar es salaam linalotarajia kuchukua siku mbili likiwa limeaambatana na maonyesho ya vifaa na huduma mbali mbali zinazotolewa na taasisi za serikali na zile za binafsi zinazojishughulisha na maswala ya afya...

Like
199
0
Wednesday, 26 August 2015