kupitia joto la asubuhi waweza kuwa mshindi pia, njia ni rahisi zaidi unachotakiwa kufanya ni kusikiliza kipindi cha Joto la asubuhi jumatatu hadi ijumaa Picha kulia n bwana Lwantwalr James Lutakoibwa kutokaMwananyamala Picha kulia ni Kijungu C Mwanji mkazi wa wazo...
Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech aliokoa mara mbili mipira ya hatari iliyokuwa ikielekea langoni mwake na kuisaidia timu yake kupata alama moja katika mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool. Katika mchezo huo mikwaju miwili ya Philippe Coutinho ililenga mwamba huku kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey akikataliwa goli alilofunga kipindi cha kwanza kutokana na kuwa katika mstari wa kuotea. Cech aliokoa kwa mara nyingine mkwaju wa karibu wa Christian Benteke na kuucheza tena kwa umahiri mpira uliopigwa...
WAZIRI wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond amekutana na rais wa Iran Hassan Rouhani mjini Tehran kwaajili ya mazungumzo ya kiserikali baina ya nchi hizo mbili. Waziri Hammond amesema Iran ina ushawishi mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati na inaweza kuwa mshirika mojawapo muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi. Amesema mataifa hayo mawili yana msimamo wa pamoja licha ya historia ya kutoaminiana na yamekubaliana juu ya hoja ya kulishinda kundi la Dola la Kiislamu na kuzuia mihadarati...
NCHI za Korea kaskazini na Kusini zimefikia makubaliano ya kupunguza hali ya wasiwasi iliyopo mpakani mwa nchi hizo mbili. Hatua hiyo imefikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu ambapo nchi zote mbili ziliweka vikosi vyake vya ulinzi kama tahadhari baada ya mapigano ya muda mfupi yaliyotokea wiki iliyopita. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na pande hizo mbili, Korea kusini imekubali kuacha kueneza habari zenye propaganda zinazochochea pande hizo, huku Korea kaskazini ikielezea masikitiko yake juu ya tukio la hivi karibuni...
IMEELEZWA kuwa kukosekana kwa huduma ya umeme katika baadhi ya vituo vya afya Jijini Mwanza kumesababisha kuzorota kwa upatikanaji wa huduma katika vituo hivyo. Zainabu Chambo ni Muuguzi kutoka zahanati ya Buhongwa iliyopo wilaya ya Nyamagana Jijini humo amesema hali hiyo husababisha mama wajamzito kwenda kutafuta zahanati nyingine kwa umbali mrefu kwaajili ya kupatiwa huduma hali inayowalazimu kutoa kiasi kikubwa cha fedha. Zainabu amesema kitendo cha kukosekana kwa umeme kimewawia vigumu wao kufanya ufuatiliaji na kujua nani ana...
CHUO kikuu cha Dodoma-UDOM-kinatarajia kufanya hafla ya kumuenzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete kama sehemu ya kutambua mchango wake wa kuwezesha kujengwa kwa chuo hicho. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa chuo hicho profesa Idris Kikula wakati akizungumza na baadhi ya mabalozi na maafisa wa uwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika umoja wa mataifa inasema kuwa Rais Kikwete amefanya kazi kubwa katika kuhimiza na kufanikisha ujenzi wa chuo hicho. Profesa Kikula...
MAELFU ya wahamiaji, wengi wao wakimbizi wa Syria, wamesafiri kupitia Macedonia na Serbia wakielekea Ulaya Magharibi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR limesema zaidi ya watu elfu 7,000 wakiwemo wanaume, wanawake na watoto, walivuka mpaka na kuingia kusini mwa Serbia na Macedonia usiku wa kumkia jana Jumapili, huku wengi wakitarajiwa kuwasili. Shirika hilo limesema jana limehakikishiwa na serikali ya Macedonia kwamba mipaka itakuwa wazi kwa wakimbizi wanaokimbia mizozo katika nchi...
KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anaendelea na ziara yake ya siku mbili nchini Nigeria. Ki Moon aliwasili jana mjini Abuja saa chache baada ya jeshi kutangaza wapiganaji wa kundi la Boko Haram walikuwa wameushambulia msafara wa mnadhimu mkuu wa jeshi la nchi hiyo Luteni Kanali Tukur Buratai. Buratai ambaye hakudhurika, alikuwa akiwatembelea wanajeshi Jumamosi wakati wanamgambo walipokishambulia kijiji cha Falijari, kilometa 40 mashariki ya mji mkuu wa jimbo la Borno,...
KATIKA kufanya Tathmini ya matatizo ya usafiri kwenye jiji la Dar es salaam, Mgombea Urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA– Edward Lowasa akiambatana na Mgombea mwenza Juma Duni Haji ametembelea maeneo mbalimbali ya jiji kwa kutumia usafiri wa daladala. Lowasa ametumia usafiri huo majira ya asubuhi akitokea Gongo la Mboto wilayani Ilala jijini Dar es salaam hadi eneo la Pugu na kutoka Pugu hadi Mbagala ambapo amejionea namna ambavyo wananchi wa Dar es salaam wanavyopata shida...
WAKATI Zoezi la kuhakiki taarifa kwa waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura likitarajiwa kukamilika leo Tume ya Taifa ya uchaguzi –NEC- imesema kuwa imebaini zaidi ya watu Elfu 52 waliojiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari hilo. Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani amesema kuwa ingawa Zoezi hilo limepitia changamoto nyingi lakini limefanikisha lengo lililowekwa kwa kiasi kikubwa. Aidha amewataka watanzania kutoyumbishwa na maneno yanayotolewa na baadhi ya watu na yasiyo na ukweli wowote juu ya mfumo wa BVR...
KATIBU mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amewasili jana nchini Nigeria tayari kwa kuanza ziara ya siku mbili nchini humo. Katika ziara hiyo Ban ki-moon anaitembelea Nigeria kwa lengo la kuwatembelea waathirika wa mashambulizi yaliyofanywa katika ofisi za umoja huo mjini Abuja yanayodaiwa kufanywa na wanamgambo wa Boko Haram miaka minne iliyopita. Ban Ki Moon pia atakutana na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ili kujadili namna ya kupambana na vikundi vyenye msimamo mkali ambapo pia anatarajiwa kuwa na mazungumzo...