Slider

AUA MKEWE KWA UGOMVI WA KIMAPENZI
Local News

MTU mmoja ambaye hajafahamika jina lake mara moja mkazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani amemuua mke wake kwa kumchoma kisu sehemu tofauti za mwili kufuatia kuwepo kwa ugomvi wa muda mrefu baina yao.   Hali hiyo imetokana na kuwepo kwa sintofahamu baina ya wanafamilia hao suala ambalo awali lilifikishwa kituo cha polisi kilichopo wilayani hapo kwaajili ya kulitolea ufafanuzi.   Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ULRICH MATEI amesema kuwa tukio hilo limetokea katika...

Like
197
0
Friday, 21 August 2015
UFARANSA NA UINGEREZA KUIMARISHA USALAMA
Global News

MAAFISA kutoka Ufaransa na Uingereza wamesaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa usalama katika kivuko kimoja muhimu cha mpakani, huku wakitangaza hatua zikiwemo teknolojia ya kisasa ili kuwadhibiti wahamiaji na waomba hifadhi wanaojaribu kuingia Uingereza. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Bernard Cazeneuve na mwenzake wa Uingereza Theresa May, wamesaini makubaliano  ya muafaka jana katika mji wa bandari wa Calais, ambako mamia ya watu wamejaribu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza kutokea Ulaya katika kipindi cha mwaka huu...

Like
327
0
Friday, 21 August 2015
SPIKA WA CONGRESS AFUNGULIWA MASHTAKA BRAZIL
Global News

WAENDESHA mashtaka nchini Brazil wamefungua mashtaka ya rushwa na usafishaji wa fedha chafu dhidi ya spika wa congress, Eduardo Cunha. Cunha anatuhumiwa kupokea dola milioni tano kama rushwa ili kuingia katika mikabata na shirika la mafuta la serikali, Petrobras. Bwana Cunha amekana tuhuma hizo na kusema zina ushawishi wa...

Like
185
0
Friday, 21 August 2015
NEC YAANZA KUPOKEA FOMU ZA UTEUZI ZA VYAMA 13 LEO
Local News

TUME ya Taifa ya uchaguzi Makao makuu, leo imeanza kupokea fomu za uteuzi za vyama 13 kwa ajili ya uteuzi wa nafasi ya kugombea urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika hapa nchini mwezi oktoba mwaka huu. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NEC, Zoezi hilo limeanza leo saa tatu asubuhi na chama cha UPDP na saa tano hiii ni zamu ya Mgombea wa Chama cha Mapinduzi –ccm baada ya mgombea wa Chadema kufanya hivyo saa nne asubuhi. Mwenyekiti...

Like
198
0
Friday, 21 August 2015
OTAMENDI NDANI YA MAN CITY
Slider

Beki wa timu ya taifa ya kandanda Argentina, Nicolas Otamendi, amesaini na miamba wa Uingereza, Machester City, timu hiyo imetangaza Alhamisi kufuatia makubaliano na Valencia wa Uhispania kukamilisha biashara hiyo. Otamendi, 27, amekubali kandarasi ya urefu wa miaka mitano ingawa dau husika halikutangazwa. City wameimairisha ngome yao na Otamendi ambaye ataungana tena na mwenzake wa zamani katika majitu wa Ureno, FC Porto, Eliaquim Mangala na ndugu yake kwenye kikosi cha Argentina, Martin Demichelis pamoja na nahodha Vincent Kompany wa...

Like
205
0
Friday, 21 August 2015
IS WAFANYA SHAMBULIZI MISRI
Global News

BOMU kubwa limelipuka karibu na makao makuu ya usalama kaskazini mwa mji mkuu wa Misri, Cairo ambako watu 29 walijeruhiwa akiwemo maafisa sita wa polisi. Eneo hilo kwa sasa limefungwa na kuna maafisa wengi wa polisi katika barabara za mji huo. Kundi la wapiganaji wa Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi...

Like
210
0
Thursday, 20 August 2015
NKURUNZIZA AAPISHWA KWA MUHULA WA TATU
Global News

RAIS wa Burundi Pierre Nkurunziza anaapishwa kwa muhula wa tatu uliozua utata katika sherehe ambayo inadaiwa kuwa imefanyika kwa mshangao mkubwa kwa kuwa rais huyo alitarajiwa kuapishwa wiki ijayo. Hata hivyo hakuna kiongozi wa taifa lolote aliyehudhuria sherehe za kuapishwa kwake huku Afrika kusini ikishirikishwa na waziri mmoja kwa mujibu wa shirika AFP. Mataifa kadhaa yakiwemo yale ya China na Urusi yalituma mabalozi wao....

Like
185
0
Thursday, 20 August 2015
TANZANIA YAFANIKIWA KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO
Local News

IMEELEZWA kuwa Tanzania imefanikiwa kufikia miongoni mwa malengo ya millennia yakupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano pamoja na vifo vya akina mama wakati wa kujifungua. Hayo yamebainisha leo na mratibu wa maswala ya uzazi kutoka Wizara ya Afya Dokta Kokeleth Winani alipomwakilisha katibu mkuu wa wizara hiyo katika uzinduzi wa mtandao wa waandishi wa habari wa afya ya uzazi na jinsia. Amesema kwa sasa katika kila vizazi elfu moja, watoto wanaopoteza maisha ni...

Like
256
0
Thursday, 20 August 2015
NCCR YAKANUSHA KUJITOA UKAWA
Local News

CHAMA cha NCCR-MAGEUZI kimekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura amesema kuwa chama hicho kimejitoa katika Umoja wa Katiba ya wananchi-UKAWA. Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Nccr, Nderakindo Kessy ambaye amesema kuwa wananchi waamini kuwa chama hicho hakiwezi kujitoa...

Like
206
0
Thursday, 20 August 2015
ROONEY AWATAKA MASHABIKI KUWA NA SUBIRA
Slider

Mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney amesema ”magoli yatakuja” baada ya kuanza msimu mpya bila ya kufunga goli lolote.Rooney, mwenye miaka 29, amecheza kama mshambuliaji wa kati kwenye michezo yote ya ufunguzi wa ligi. Lakini bado hajafumania nyavu katika mchezo wowote tokea kuanza kwa msimu huku baadhi ya watu wakidai kuwa uwezo wake wa kufumania nyavu umeshuka. ”Nimekua na mchezo mbaya msimu huu na kilamtu analizungumzia hilo.Nimewahi kuwa na tatizo kama hilo kipindi cha nyuma lakini natumai mwishoni mwa juma...

Like
235
0
Thursday, 20 August 2015
RYAN JONES ASTAAFU RAGA
Slider

Nahodha wa zamani wa Wales Ryan Jones amestaafu kucheza mchezo wa raga kutokana na ushauri wa madaktari.Mchezaji huyo mwenye miaka 34, aliyeshinda pia vikombe 75 katika timu yake ya Wales,amekua na nafuu kutokana na upasuaji wa bega aliofanyiwa mwishoni mwa msimu uliopita. Lakini Jones amehsauriwa kutorudi tena katika mchezo huo kutokana na kuwepo uwezekano wa kupata majeraha makubwa zaidi jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwake.”Maneno pamoja na umri juu ya kufanya maamuzi pamoja na kuwa na moyo mzito wa kuamini...

Like
249
0
Thursday, 20 August 2015