Slider

FRONTEX YATAKA MISAADA ZAIDI KWA NCHI ZENYE IDADI KUBWA YA WAHAMIAJI
Global News

SHIRIKA la Umoja wa Ulaya linalopambana na maswala ya uhamiaji haramu na biashara ya binadamu, Frontex limetoa wito kwa nchi wanachama wa umoja huo kutoa msaada zaidi kwa nchi tatu zilizoathirika kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji. Ugiriki, Italia na Hungary ni nchi zinazoelezwa kuathiriwa zaidi. Watu hao wengi wanaelezwa kutoka nchini Syria,Afghanistan na nchi za kusini mwa jangwa la Sahara wakikimbia hali mbaya ya usalama na...

Like
147
0
Wednesday, 19 August 2015
TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO YATAJWA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAPATO YA SERIKALI
Local News

MATUMIZI ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali imeelezwa kuwa yamepunguza upotevu wa mapato uliokuwa ukisababishwa na watendaji wasio waaminifu. Kauli hiyo jijini Arusha  na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bwana Adorf Mapunda wakati akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali Mtandao uliowahusisha maafisa TEHAMA, Rasilimali watu, Utawala na Maafisa Habari kutoka maeneo mbalimbali nchini. Amesema mabadiliko hayo ya ukusanyaji wa fedha kielektroniki yameongeza ufanisi kwa kuongeza ukusanyaji...

Like
181
0
Wednesday, 19 August 2015
TGNP YAWATAKA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSISHA SUALA MAJI KATIKA SERA ZAO
Local News

MTANDAO wa jinsia Tanzania TGNP umeandaa warsha iliyowashirikisha wanaharakati wa masuala ya maji safi na mazingira kutoka maeneo mbalimbali ambapo wamewataka viongozi wa vyama vya siasa kuhusisha suala la maji katika sera zao. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam katika warsha hiyo Mkurugenzi wa TGNP LILIAN LIUNDI amesema kuwa maji ni tatizo sugu ambalo huwaathiri sana...

Like
150
0
Wednesday, 19 August 2015
MUINGEREZA AKAMATWA BANGLADESH KWA MAUAJI
Global News

POLISI nchini Bangladesh wamewakamata watu wengine watatu, akiwemo raia mmoja wa Uingereza kuhusiana na mauaji ya mwanablogu maarufu ambaye anaaminika kuwa si-mcha Mungu. Idara ya Polisi imesema kuwa raia huyo wa Bangladesh mwenye asili ya Uingereza anayefahamika kwa jina la Touhidur Rahman anashukiwa kutoa ufadhili wa kifedha kwa washukiwa hao wengine wawili waliokamatwa juzi akiwemo Niloy Neel. Taarifa zinasema kuwa washukiwa wawili ambao wanatuhumiwa kuhusika moja kwa moja na mauwaji hayo walikuwa wamekamatwa tayari juma lililopita....

Like
186
0
Tuesday, 18 August 2015
RAIS WA GABON AAHIDI KUTOA URITHI WAKE WOTE KWA VIJANA
Global News

RAIS wa Gabon Ali Bongo Ondimba ameahidi kutoa urithi wake wote kwa vijana nchini humo. Rais Bongo amesema kuwa mali yote aliyopokea kama urithi kutoka kwa babaake mzazi aliyekuwa rais wa Gabon kwa kipindi kirefu,Omar Bongo itakwenda kwa vijana wa Gabon. Shirika la habari la AFP limesema kuwa rais Bongo ameahidi kuuza majengo mawili yaliyopo Ufaransa aliyopewa na mzazi kwa thamani ya Franka moja kama ishara ya kujitolea kuimarisha hali ya kiuchumi ya vijana wa taifa...

Like
213
0
Tuesday, 18 August 2015
CCM YAKAMILISHA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE SINGIDA MASHARIKI NA KITETO
Local News

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi –CCM– Taifa katika kikao chake cha siku moja jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Rais dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.   Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau –Singida Mashariki na Ndugu Emmanuel Papian John mgombea wa jimbo la Kiteto.   Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi...

Like
508
0
Tuesday, 18 August 2015
WANANCHI WATAHADHARISHWA KIPINDUPINDU DAR
Local News

WATANZANIA hususani wakazi wa Jiji la Dar es salaam wameombwa kuwa makini katika matumizi ya vyakula na mazingira wanayo ishi kutokana na uwepo wa ugonjwa wa kipindupindu ambao mpaka sasa umeshasababisha vifo kwa watu watatu. Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya kuenea kwa ugonjwa huohatari. Naye mganga Mkuu wa wilaya hiyo dokta Azizi Msuya amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema hasa wanapohisi uwepo wa dalili...

Like
253
0
Tuesday, 18 August 2015
VIJANA WACHANGIA DAMU WANAJESHI CAMEROON
Global News

MAMIA ya vijana wamejitokeza nchini Cameroon kujitolea kuwapa damu wanajeshi wanaopambana na kundi la wapiganaji la Boko Haram kaskazini mwa nchi hiyo. Kampeni hiyo imeandaliwa na baraza la muungano wa vijana nchini humo ambao wamesema kuwa huo ndio mchango wao mkubwa na muhimu dhidi ya ugaidi. Hospilitali ya kijeshi ya Yaounde ambayo wanajeshi waliojeruhiwa kutoka Cameroon na Chad hupewa matibabu, imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa akiba ya damu ya...

Like
295
0
Tuesday, 18 August 2015
MAREKANI YATOA ONYO KWA SALVA KIIR
Global News

MUDA mchache baada ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kukataa kusaini makubaliano ya amani na hasimu wake, Riek Machar, Marekani imemtaka kufanya hivyo ndani ya wiki mbili, au akabiliane na hatua kali. Machar alisaini hapo jana makubaliano ambayo yanakusudiwa kukomesha miezi 20 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini Rais Kiir amesema atarejea mjini Addis Ababa, baada ya siku 15 za mashauriano. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani John Kirby, amewaambia waandishi wa habari kuwa nchi...

Like
199
0
Tuesday, 18 August 2015
WANANCHI WALIA NA DAWASCO KUKOSEKANA KWA MAJI KINONDONI
Local News

BAADHI ya Wananchi wa mtaa wa Mkunguni A Kinondoni Jijini Dar es salaam wameilalamikia Mamlaka ya maji safi na maji taka-Dawasco kwa kutokuwa na huduma ya maji kwa muda mrefu katika eneo hilo. Wakizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam wananchi hao wamesema kuwa tatizo la kukosa maji eneo lao lipo kwa muda mrefu ingawa bado hawajui sababu japokuwa mabomba ya maji yapo. Kwa upande wake Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco Evertasting Lyaro ameeleza kuwa tatizo hilo si la...

Like
353
0
Tuesday, 18 August 2015
NHIF YAINGIA MKATABA NA JWTZ
Local News

MFUKO wa Taifa  wa Bima ya Afya –NHIF, umeingia mkataba na Jeshi la Wananchi wa Tanzania –JWTZ, ambapo wanachama wa mfuko huo na wategemezi wao watapata huduma za matibabu katika hospitali  za jeshi nchini kote. Mkataba huo wa miaka mitatu unalenga kupanua wigo wa vituo vya matibabu na kuanzisha ushirikiano wa kihistoria baina ya pande hizo mbili. Akizungumza wakati wa kutiliana saini mkataba huo, Mkuu wa Huduma za Afya Jeshini Brigedia DENIS RAPHAEL JANGA, amesema amepokea kwa furaha mkataba huo...

Like
621
0
Tuesday, 18 August 2015