Slider

ROCKSTAR4000 YATANGAZA COLLABO YA ALI KIBA NA NEYO
Slider

  Kampuni kubwa ya muziki duniani Rockstar 4000 inayosimamia kazi za Ali Kiba imetangaza Collabo ya msanii huyu na mkali wa miondoko ya R&B duniani kutoka Marekani Neyo kupitia akaunti ya Instagram ya kampuni hiyo. Ni furaha kwa muziki wa Afrika Mashariki kuzidi kuvuka boda na mipaka ya dunia, Hongera Ali Kiba pamoja na wasanii wote wanaofanya kazi nzuri kuutangaza muziki na kazi za...

Like
399
0
Friday, 14 August 2015
MOURINHO ASHUTUMIWA KUMTEMA EVA
Slider

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amejipata akishutumiwa vikali baada ya ripoti kuibuka kwamba amemtenga daktari wa mabingwa hao wa Ligi ya Premia Eva Carneiro. Ripoti kwenye vyombo vya habari Uingereza zinasema Carneiro hatakuwa tena akihudhuria mechi za Chelsea wala vikao vya mazoezi baada ya Mourinho kumzomea yeye na daktari wa viungo Jon Fearn kwa kukimbia uwanjani kumhudumia Eden Hazard dakika za mwisho za mechi ya wikendi iliyopita iliyoisha sare 2-2 nyumbani dhidi ya Swansea City. Mourinho, aliyesema Carneiro na Fearn...

Like
439
0
Friday, 14 August 2015
BWANA E AKIGAWA ZAWADI KWA WAPENZI NA MASHABIKI WA EFM KIBAHA
Entertanment

Tukipata picha na mashabiki wa EFM maeneo ya Kibaha kuwashukuru na kuwatunza kuwapa zawadi kwa kutusikiliza ikiwa ni maandalizi ya ujio wa Muziki mnene bar kwa bar. Bango la MUZIKI MNENE lilionekana maeneo ya mjini Kibaha, lilowekwa na mmoja wa mashabiki wa EFM Radio 93.7. Kushoto ni Jimy Jam mfanyakazi wa efm akipozi kwa pamoja na Mmoja kati ya washindi  wa kwanza kutoka kulia, bwana Halid, akipewa zawadi yake baada ya kuweka bango la EFM MUZIKI MNENE eneo la Kibaha jana....

Like
417
0
Thursday, 13 August 2015
BOMU LAUA 50 BAGHDAD
Global News

BOMU  kubwa  lililokuwa  katika  gari  limeripuka  katika soko  lililokuwa  na  watu  wengi mjini  Baghdad  leo na kusababisha  watu 50  kuuwawa  na  wengine  150 wamejeruhiwa.   Polisi   mjini  Baghdad  imesema  gari hilo  liliripuriwa katika  soko  la  chakula  la  Jamila  katika  mji wa  Sadr, ambao wakazi wake wengi ni Washia , Mashariki  mwa Baghdad.   Maafisa  wa hospitali  wamesema  wengi  wa  wahanga wamepata  majeraha  makubwa ....

Like
288
0
Thursday, 13 August 2015
BAKITA YATHIBITISHA KUKUA KWA LUGHA YA KISWAHILI
Local News

BARAZA la Kiswahili la Taifa- BAKITA limethibitisha kukua kwa kasi kwa  lugha ya kiswhili katika nchi za Afrika Mashariki na duniani kutokana na lugha hiyo kutumika katika mikutano mbalimbali ya kimataifa. Msanifu Mkuu wa lugha ya Kiswahili CONSOLATA MUSHI amesema kwa sasa vipo vyuo vikuu mbalimbali Duniani na Taasisi zinazoeneza lugha hiyo kwa kufundisha katika vyuo...

Like
449
0
Thursday, 13 August 2015
UKAWA WAKUBALIANA KUSIMAMISHA MGOMBEA MMOJA KWENYE KILA KATA NAFASI ZA MADIWANI
Local News

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi- UKAWA- Vimesaini Waraka wa Ushirikiano  katika Kugombea nafasi za madiwani kwenye Uchaguzi Mkuu ambapo vitakua na Mgombea mmoja ataewakilisha vyama hivyo kwa kila kata.   Waraka huo umesainiwa leo na Makatibu wakuu wa vyama hivyo mbele ya Waandishi wa habari huku Chama cha NLD kikiwakilishwa na Katibu Mkuu Tozzy Matwanga, Chama cha CUF Naibu Katibu Mkuu Magdalena Sakaya, Chama cha NCCR Mageuzi Kaimu Katibu Mkuu Dokta George Kahangwa na CHADEMA Naibu Katibu Mkuu...

Like
162
0
Thursday, 13 August 2015
SERIKALI YATARAJIA KUFUNGUA MAABARA YA MADINI
Local News

TANZANIA inatarajia kufungua maabara ya madini itakayo kuwa ikitumiwa na Nchi zote zinanzozunguka ukanda wa Maziwa makuu kwa ajili ya kuchunguza madini kwa kutumia teknolojia ya alama ya vidole, kutambua madini yanapotokea ili kudhibiti utoroshwaji wake na baishara haramu katika nchi hizo. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Injinia Ngosi Mwihava katika Mkutano wa Kongamano la nchi za Maziwa makuu-ICGLR wenye lengo la kujadili namna ya kutumia alama za...

Like
229
0
Thursday, 13 August 2015
CHINA: MLIPUKO MKUBWA WATOKEA TIANJIAN
Local News

KUMETOKEA mlipuko mkubwa katika mji wa China Tianjin-ambao ni mji wa Bandari kuu na sehemu ya viwanda katika eneo la kusini kaskazini mwa mji mkuu Beijing. Video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha moto mkubwa na wingu kubwa la moshi lililotanda angani. Shirika la habari la nchi hiyo, Xinhua limesema mlipuko huo umetokea katika mji wa Tianjin Binhai ukanda ulioendelea kiviwanda uliopo karibu na bandari na watu wanakimbia katika eneo hilo kunusuru maisha yao.Mpaka sasa bado hakijajulikana chanzo kikuu cha...

Like
191
0
Thursday, 13 August 2015
JAMII IMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZINAZOTOA HUDUMA KWA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
Local News

JAMII imetakiwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma kwa watoto yatima na wanao ishi katika  mazingira magumu kwani kwa kufanya hivyo itaweza kupunguza ongezeko la idadi kubwa ya watoto wa mitaani.   Akizungumza na EFM Mkurugenzi wa kituo kinacholea watoto wanaoishi katika mazingira magumu –BABA WATOTO CENTER–  MGUNGA MNYENYELWA amesema kuwa mpaka sasa wameweza kulea watoto 200  kituoni hapo pamoja na kuwapatia  mafunzo mbalimbali yanayohusu stadi za maisha.   Amebainisha kuwa Miongoni mwa mafunzo...

Like
274
0
Thursday, 13 August 2015
MISINGI YA AMANI YATAJWA
Local News

IMEELEZWA kuwa ili Tanzania iweze kuwa na amani ya kudumu, Taifa linahitaji kuwa na misingi madhubuti yenye kuzingatia haki na usawa. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya njia ya mitandao ya habari ijulukanayo kama uchaguzi Tanzania 2015 kura yetu,  Kiongozi kijana HUMPHREY POLEPOLE amebainisha kuwa haki na usawa vitasaidia kuondoa vizingiti kati ya wakristo na waislamu, viongozi wa siasa na vyama vyao lakini pia kati ya taasisi mbalimbali zikiwemo...

Like
328
0
Thursday, 13 August 2015
RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE CLARA MWATUKA
Local News

RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mheshimiwa Clara Mwatuka aliyefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara tarehe 9 Agosti, mwaka huu.   Kutokana na kifo cha Mbunge huyo, Rais Kikwete ametoa pole kwa familia yake kwa kumpoteza Mzazi, kwa...

Like
339
0
Thursday, 13 August 2015