Wimbo mpya kutoka kundi la Waswazi waliomshirikisha Rich Mavoko Song Nakosa Imani Producer Abba Process Video directed by Adam Juma...
Yaya Toure aliiongoza Man City katika ushindi mnono dhidi ya West Brom ambapo Raheem Sterling aliyesajiliwa majira ya joto kwa dau la pauni milioni 49 akicheza mchezo wake wa kwanza kwa timu yake mpya. Mkwaju wa Toure uliombabatiza mchezaji mwenzake David Silva ulikwenda pia kwenye miguu ya mlinzi wa West Brom Craig Dawson kabla ya kutinga nyavuni. City waliendeleza kupanua ushindi wao baada ya Toure kupiga mkwaju mwingine uliokwenda kona ya juu na kuwa goli la pili.Nahodha Vincent Kompany alihitimisha...
BUNGE la Iraq limepiga kura kwa wingi kuunga mkono mapendekezo yaliotolewa na waziri mkuu Haider al Abadi kwa lengo la kukabiliana na ufisadi pamoja na kupunguza matumizi ya fedha serikalini. Spika wa bunge hilo Salim al Juburi amesema kuwa muswada huo umepitishwa bila upinzani wowote ambao unalenga kupunguzwa kwa baadhi ya nyadhfa serikalini, kumaliza ubaguzi wa kidini pamoja na wa kisisasa. Hatua hiyo imefikiwa wakati ambapo kumekuwa na maanadamano ya raia kuhusu kukatika mara kwa mara kwa umeme wakati ambapo...
NCHI ya Uturuki imeanzisha tena msururu wa mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi yanayolenga maeneo 17 kusini mashariki mkoani Hakkari katika mpaka na Iran. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Uturuki imeshuhudia ghasia zaidi katika wiki za hivi karibuni kati ya wanajeshi na wapiganaji wa Kikurdi wanaotaka kujiondoa katika utawala wa jeshi. Mashambulio hayo yanajiri siku moja baada ya watu tisa kuuawa katika msururu wa mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama huku wengine wakiwa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi...
WANANCHI wa kata ya Makumbusho wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam wameilalamikia serikali ya mtaa wa Kambangwa kwa kitendo cha watendaji hao kujichukulia sheria mkononi ya kuwatoza faini juu ya matumizi ya huduma za kijamii ambazo kwa mujibu wa halmashauri huduma hizo hutolewa bure. Aidha wanachi hao wameshindwa kufahamu mapato na matumizi ya ofisi ya serikali yao kutokana na kutoitwa katika vikao tangu kupatikana kwa uongozi mpya mwishoni mwa mwaka jana. Akizungumza na kituo hiki jijini hapa mwenyekiti wa...
KUTOKANA na ongezeko la uhalifu katika mitandao ya kijamii, kampuni mbalimbali nchini zinazojihusisha na shughuli zake kwa kutumia Mitandao zimetakiwa kuongeza umakini katika kulinda taarifa zao dhidi ya watumiaji wabaya wa mitandao hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano uliowakutanisha wataalamu mbalimbali wanaoshughulika na mifumo ya k ompyuta, mtendaji mkuu wa wakala wa serekali mtandao Dokta GABRIEL BAKARI amesema kuwa sekta ya teknolojia inakuwa kwa kasi nchini hivyo ni vyema tahadhari za kulinda mitandao hiyo...
SERIKALI ya Marekani imesema kwamba ina wasiwasi mkubwa kuhusiana na kuzuiwa kwa wapinzani tisini katika mji mkuu wa Cuba, Havana mwishoni mwa wiki iliyopita. Wajumbe wa kundi moja la kipinzani la wasichana wanaovaa nguo nyeupe wamesema kuwa wanausalama wa Cuba waliwazingira na kuwashililia kisha kuwaachilia huru baada ya saa nne unusu kupita. Kukamatwa huko kumekuja siku chache kabla ya ziara ya John Kerry jijini Havana, ziara ambayo ni ya kwanza kutoka kwa kiongozi wa marekani baada ya miaka saba....
BARAZA la usalama la umoja wa mataifa limeunga mkono mpango wa kutuma maafisa wake wa ngazi ya juu nchini Burundi kwa ajili ya kutatua hali ya sintofahamu iliyopo nchini humo. Baraza lililopo kwa sasa chini ya Mnigeria Joy Ogwu limesema kuwa kumekuwepo na wasiwasi mkubwa juu ya hali ya usalama nchini Burundi huku likitoa wito kwa serikali kufanya mazungumzo ya amani na upande wa upinzani. Kiongozi mwandamizi wa umoja wa mataifa kuhusiana na haki za binaadam Ivan Simonovic ambaye alipelekwa...
KUFUATIA matukio kadhaa ya wanasiasa kuvihama vyama vyao baada ya kuenguliwa katika kinyang’anyilo cha kugombea nyadhifa mbalimbali Msanii wa sanaa ya Uigizaji Nchini Steven Mengere amewataka Wanasiasa kuwa na Msimamo ndani ya vyama vyao. Mengere ameyasema hayo wakati akizungumza na kituo hiki na kudai kuwa mfumo huo umekuwa ndio kimbilio la Wanasiasa wanaokosa sifa za kugombea kupitia vyama vyao wakidhani kwamba hiyo ndio njia ya kupata uongozi. Amebainisha kuwa pamoja na kushindwa katika kinyang’anyilo hicho ni...
WATUMISHI wa Serikali wameaswa kuwa na nidhamu ya matumizi bora ya rasilimali fedha ili kuleta ufanisi na maendeleo endelevu kwa manufaa ya wananchi.\ Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha dokta Servacius Likwelile alipokuwa akiongea na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya wafanyakazi wa Hazina Ndogo mkoani Lindi . Dokta Likwelile amesema kuwa Serikali inafanya mapitio ya Mkakati wa Kupunguza Umasikini Tanzania –MKUKUTA- na kuhakikisha kuwa changamoto zilizokuwepo awali zinapatiwa ufumbuzi ili kuleta tija na...
BAADA ya kumalizika kwa Tamasha la muziki mnene Bar kwa bar awamu ya kwanza, na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena, Uongozi Efm umekubali ombi hilo na sasa Tamasha hilo linarudi tena kwa kishindo likiwa limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia watu wengi zaidi. Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu wake na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa utapelekwa...