Slider

MAREKANI: MICHAEL BROWN AKUMBUKWA
Global News

MAANDAMANO yamefanyika nchini Marekani kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa kijana mweusi, Michael Brown ambaye hakuwa na silaha. Kijana huyo aliuawa na polisi mzungu katika mji wa Ferguson jimboni Missouri Agosti mwaka uliopita. Miezi michache iliyofuata, watu wengine kadhaa weusi wasio na silaha waliuawa na maafisa wa polisi katika miji mbali mbali ya Marekani, ikiwemo New York, Cleveland na Baltimore. Mamia ya watu wamekusanyika katika mji wa Ferguson jana Jumapili, na kufanya matembezi ya kimya ambayo yaliongozwa na baba wa...

Like
210
0
Monday, 10 August 2015
KUMI WAUAWA MALI
Global News

JESHI nchini Mali limesema zaidi ya watu kumi wameuawa katika shambulio moja kwenye mji wa Gaberi kaskazini nchini humo. Shambulizi hilo limekuja siku moja baada ya watu kumi na watatu wakiwemo washambuliaji wanne kuuawa ambapo washukiwa wa tukio hilo Wanajeshi wa Kiislam walishambuliana na jeshi la serikali walipowazingira kwenye hotel moja katikati mwa mji wa Sevare. Msemaji wa jeshi la Mali alikaririwa akisema ni mapema mno kujua kama mashambulizi hayo mawili yalikua na uhusiano ama...

Like
175
0
Monday, 10 August 2015
WATANZANIA WAMEOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUCHANGIA MFUKO WA UWEZESHAJI WATU WENYE ULEMAVU
Local News

WATANZANIA wameombwa kujitokeza kwa wingi katika kuchangia mfuko wa uwezeshaji watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu hao.   Akizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam makamu mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu wilaya ya Temeke Shany Zubery amesema kuwa endapo suala la uchangishaji litafanikiwa litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwasaidia watu hao.   Aidha amesema kuwa shirikisho hilo limekuwa likikabiliwa na changamoto nyingi ambazo husababisha kushindwa...

Like
302
0
Monday, 10 August 2015
CHADEMA KUFANYA MAANDAMANO KUMSINDIKIZA LOWASA KUCHUKUA FOMU
Local News

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimesema hakijapata taarifa ya Jeshi la polisi inayowazuia kufanya maandamano ya kumsindikiza mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi –UKAWA– Edward Lowasa anayetarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo leo katika ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC- akiambatana na Mgombea mwenza Juma Duni Haji.   Jeshi la Polisi kanda  Maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano ya mgombea huyo kwenda kuchukua fomu NEC kwa maandamano yanayoanzia ofisi za CUF...

Like
267
0
Monday, 10 August 2015
MOURINHO: HATUJAMMISS PETR CECH
Slider

Kocha mbwatukaji Jose Mourinho amesema Chelsea haijammis aliyewahi kuwa mlinda mlango bora kabisa katika klabu hiyo Petr Cech na kuongeza kuwa ana uhakika mabingwa hao watetezi wataikabili vizuri kabisa klabu ya Manchester City siku ya jumapili watakaposhuka dimbani. Mourinho hakuwa tayari kumuacha mlinda mlango huyu mwenye miaka 33, ajiunge na wapinzani wao wa London klabu ya Arsenal baada misimu 11 ya mafanikio na ubingwa . “hatujammis Petr, alikaliliwa Mounrinho akizungumza na vyombo vya habari nchini Uingereza “tuna walinda mlango...

Like
227
0
Monday, 10 August 2015
COUNTINHO AITOA LIVERPOOL KIMASOMASO
Slider

Bao la kiuchawi kutoka mganga wa kutoka Brazil, Phillipe Coutinho, lilianzisha kampeni ya musimu huu ya Liverpool kwa ushindi walipolipisha kisasi dhidi ya Stoke City kwa kuwanyuka vijana wa nyumbani 1-0 Jumapili. Liverpool walirudi uwanja wa Britannia ambapo waliandaliwa kichapo kikali cha 6-1 katika ngoma ya kufunga muhula uliopita lakini waliweza kuibuka na ushindani uliotafutwa kwa hima katika mechi ambayo ilibanwa kiubunifu. Hakuna kipa alifanyishwa kazi ya kuokoa lango lake katika makabiliano yalioonekana kufikia tamati kwa sare nunge...

Like
348
0
Monday, 10 August 2015
MAKOSA YA PETR CECH YAIGHARIMU ARSENAL
Slider

Klabu ya soka ya Arsenal imekuwa na hali ngumu katika mchezo wa ufunguzi wa ligi ya England kufuatia makosa ya mlinda mlango Petr Cech kuiwezesha klabu ya West Ham kuweka rekodi ya kuitandika Arsenal 2-0 katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates Cech alisajiliwa kutoka Chelsea huku usajili wake ukitarajiwa kuisaidia Arsenal kutwaa taji la ligi hiyo lakini kwa mchezo huo wa siku ya jumapili umefungua vibaya ujio wake kwenye klabu hiyo kufuatia rekodi yao ya kufungua michuano hiyo huku...

Like
260
0
Monday, 10 August 2015
RIPOTI ZA KUTATANISHA ZAWAKERA NDUGU WA ABIRIA WALIOKUWEMO KWENYE NDEGE YA MALAYSIA
Global News

NDUGU na jamaa wa abiria waliokuwemo katika ndege ya Malaysia iliyotoweka, yenye namba za safari MH370 wameoneshwa kukasirishwa na kile wanachosema kuwa ripoti zinazotolewa juu ya kupotea kwa ndege hiyo ni za kutatanisha. Jana Malaysia ilithibitisha kuwa kipande cha bawa la ndege kilichogunduliwa katika kisiwa cha Reunion kilikuwa ni sehemu ya ndege hiyo iliyopotea. Hata hivyo nchi ya Ufaransa imesema itapeleka vifaa zaidi vya majini na angani nje ya kisiwa cha Reunion leo kutafuta mabaki zaidi ambapo jumla ya watu...

Like
215
0
Friday, 07 August 2015
MALI: HOTELI YASHAMBULIWA KATIKA MJI WA SEVARE
Global News

WATU waliojihami kwa kutumia bunduki wameshambulia zaidi ya hoteli mbili katika mji wa Sevare eneo la katikati ya nchini Mali. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kwamba watu hao waliokuwa  wakiendesha pikipiki wameingia katika eneo hilo na kuanza kufyatua risasi kwenye majengo hayo. Imebainika kwamba ingawa Mji wa Sevare una kituo cha jeshi la anga pamoja na wanajeshi kadhaa wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani lakini bado matatizo kama hayo...

Like
216
0
Friday, 07 August 2015
VIONGOZI WA VIJIJI MANYARA WATAKIWA KUFANYA MAAMUZI KWA KUFUATA SHERIA KUMALIZA MIGOGORO
Local News

VIONGOZI wa vijiji katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wametakiwa kufanya maamuzi kwa kufuata sheria ili kumaliza migogoro ya ardhi kwa kutotoa nafasi kwa watu wanaotumia fedha kujipatia ardhi. Mkuu wa wilaya hiyo Crispin Meela ameyasema hayo katika kijiji cha Kiongozi wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo kuhusiana na migogoro ya ardhi ambayo imekithiri vya kutosha wilayani humo. Aidha amesema sheria inapaswa kusimamiwa kwani watendaji hao wanatambua wazi kuwa mtu mwenye fedha hana haki kwenye mgogoro lakini wanajipa upofu...

Like
248
0
Friday, 07 August 2015
JESHI LA POLISI DODOMA YATANGAZA KUTOA MILIONI 5 KWA ATAKAEFANIKISHA KUKAMATWA KWA WAUAJI KATIKA KITUO CHA MAFUTA
Local News

JESHI la polisi mkoani Dodoma limetangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni tano kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa majambazi waliohusika na tukio la mauaji ya walinzi wawili katika kituo cha mafuta cha state oil kilichopo eneo la kisasa manispaa ya Dodoma. Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma DAVID MISIME amesema majambazi hao wamefanya uharifu huo na kufanikiwa kupora vitu mbalimbali pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 10 Aidha kamanda misime ameiasa jamii...

Like
305
0
Friday, 07 August 2015