Shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa limetangaza ubora wa viwango kwa mwezi Agosti ambapo timu ya taifa ya Argentina imeendelea kushika nafasi ya kwanza. Ubelgiji imepanda kwa nafasi moja mpaka nafasi ya pili huku mabigwa wa dunia Ujerumani wakiwa katika nafasi ya tatu. Timu ya juu kabisa toka Barani Afrika ni Algeria ambayo ipo pale pale Nafasi ya 19 na kufuatiwa na Ivory Coast waliobakia Nafasi ya 21. Timu za ukanda wa Afrika mashariki zinaongozwa na Uganda walioko nafasi...
WAASI wa kundi la kigaidi la Boko Haram wamewaua kwa bunduki watu wasiopungua tisa katika vijiji viwili Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Wanakijiji wameelezea namna ambavyo watu waliokuwa wamebeba silaha walivyowasili kwa pikipiki na kuvamia kijiji chao. Wanamgambo walipora mali kwenye nyumba na maduka na kisha kuzichoma moto nyumba zilizokuwa zimeezekwa kwa nyasi. Shambulio hili limewalazimisha mamia ya wakazi wa eneo hilo kukimbilia mji wa Potiskum uliopo kilomita 70 kutoka nyumbani kwao....
WAGOMBE 10 wanaoongoza katika kura za maoni za kumtafuta atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi mkuu wa Marekani jana usiku wamenadi sera zao katika mdahalo ulioonyeshwa kwenye televisheni. Miongoni mwa walioshiriki ni bilionea Donald Trump ambaye kwa sasa ndiye mwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda, pamoja na senator Rand Paul wa jimbo la Kentucky, seneta wa Florida Marco Rubio na seneta wa Texas Ted Cruz. Mdahalo huo uliodumu kwa masaa mawili uliwapa nafasi wagombea kutoa maoni...
WAGOMBEA urais kupitia chama cha Kijamii-CCK na Alliance for Democratic Change-ADC, leo wanatarajiwa kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC , Jijini Dar es salaam. Hivi karibuni ADC ilimtangaza Chifu Lutalosa Yemba kuwa mgombea wake wa urais huku Mwenyekiti wa chama hicho Said Miraji Abdallah akitajwa kuwa mgombea mwenzake. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi-NEC, baada ya vyama hivyo viwili kuchukua fomu leo, itafuatiwa na na ACT Wazalendo ambapo mgombea wake anatarajiwa kuchukua...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete leo anazindua rasmi benki ya kwanza ya Maendeleo ya Kilimo ambayo inalenga kuanzisha mtazamo mpya wa kukiendeleza kilimo kupitia kushirikisha wadau mbalimbali kwa kuangalia kila mnyororo wa thamani kwa ukamilifu wake pamoja na kuwa na ubunifu katika kuchangia fedha kwenye miradi mbalimbali ya sekta ya Kilimo. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kwa awamu mbili ambapo kwa awamu ya kwanza atazindua Makao Makuu ya Benki hiyo leo Jijini Dar es salaam...
MAREKANI imefanya shambulio lake la kwanza la mabomu dhidi ya wanamgambo wa Dola la Kiislamu kutokea Uturuki. Afisa wa Uturuki amesema ndege isiyokuwa na rubani iliruka kutoka kituo cha jeshi la anga kusini mwa nchi hiyo, na kushambulia maeneo karibu na Raqqa nchini Syria. Viongozi wa mataifa ya magharibi wamekuwa wakiitaka Uturuki muda mrefu kuchukua jukumu kubwa zaidi katika mapambano dhidi ya IS, lakini serikali ya ...
HELIKOPTA ya jeshi la Afghanistan imeanguka katika jimbo la kusini la Zabul leo, na wanajeshi 17 wameuwawa, ikiwa ni pamoja na marubani watano. Mkuu wa polisi wa jimbo hilo Mirwais Noorzai amesema sababu ya kuanguka helikpota hiyo haifahamiki na uchunguzi unafanyika. Wizara ya ulinzi imesema ajali hiyo inaaminika imesababishwa na hitilafu ya kiufundi , lakini hayakutolewa maelezo zaidi....
MWENYEKITI wa chama cha wananchi –CUF, Profesa Ibrahim Lipumba leo ametangaza rasmi kujiengua nafasi hiyo kutokana na umoja wa katiba ya wananchi –UKAWA, kushindwa kuenzi na kuzingatia tunu za Taifa juu ya rasimu ya katiba pendekezwa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam, Profesa Lipumba ameeleza kuwa tunu hizo ni pamoja na kushindwa kufahamu utu wa watanzania juu ya kuipata katiba pendekezwa uzalendo, uadilifu umoja, uwazi na uwajibikaji. Amefafanua kuwa kutokana na maudhui ya rasimu ya...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE amesema kuwa serikali itaendelea kushughulikia ipasavyo suala la uboreshaji wa maslahi kwa watumishi wa mahakama kwa manufaa ya utumishi wao. Rais Kikwete ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi viongozi na watumishi mbalimbali wa mahakama nchini Tanzania. Katika hafla hiyo rais Kikwete amesema kuwa kwa kipindi cha miaka kumi aliyokaa madarakani amejitahidi kuboresha shughuli za mahakama kwa kuongeza idadi ya...
WAZIRI MKUU wa Australia Tony Abbott amesema kuwa ile sintofahamu juu ya ndege ya MH 370 iliyopotea inakaribia kupatiwa ufumbuzi baada ya Malaysia kutangaza kuwa mabaki ya ndege yaliyopatikana kuwa ni sehemu ya mabaki ya ndege hiyo iliyopotea. Wataalamu wamethibitisha kuwa kipande cha bawa la ndege kilichokutwa katika ufukwe wa bahari ya hindi ni sehemu ya ndege iliyopotea, iliyokuwa mali ya malaysia, waziri mkuu, Najib Razak amethibitisha hilo jana, jumatano. Razak amesema kuwa, ni siku ya 515 tangu ndege ipotee,...
RAIA wa Japan leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima. Takriban watu laki moja na arobaini walikadiriwa kupoteza maisha baada ya Ndege ya Marekani kudondosha bomu ambalo liliuharibu mji huo tarehe 6 mwezi Agosti mwaka 1945. Katika hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kumbukumbu ya Heroshima inasisitiza uhitaji wa kufanya jitihada ya kupiga vita matumizi ya Nuklia....