IMEELEZWA kuwa bado kuna changamoto kubwa ya Watanzania wengi kutojua wapi wanaweza kupata haki zao jambo ambalo hata sehemu nyingine nje ya Tanzania wanalo. Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angela Kairuki katika uzinduzi wa Mradi wa Elimu ya Uraia kwa njia ya Simu –PCC– ulioratibiwa na Asasi ya kiraia ya C-Sema- na Shirika la –UNIDEF- la Umoja wa Mataifa wenye lengo la kutoa elimu ya uraia kwa...
Mama mzazi wa Samira ambae ni mpenzi wa muimbaji Weasel kutoka Uganda huenda akawa kwenye list ya wazazi wanaojivunia kuwa na watoto wa kike wanaowajali na kuwafanikishia ndoto zao. Hili linakuja mara baada ya mchumba huyo wa mwimbaji Weasel kuwekewa masharti iwapo atahitaji kumuoa mrembo huyo basi moja ya vitu vikubwa atakavyolazimika kuvifanya ni pamoja na kumjengea nyumba mama wa binti huyu. Chanzo cha karibu kimeeleza kuwa Weasel ana mapenzi ya dhati kwa binti huyu ikiwa ni ndoto yake kubwa...
Timu ya Taifa (Special Olympics Tanzania) iliyoko Los Anegels – Marekani imeendelea kupata mafanikio makubwa baaba ya siku ya jana tarehe 30 Julai kujipatia jumla ya medali tano. Medali hizo zimepatikana kupitia michezo na wachezaji wafuatao: Blandina Patrick m. 800 (wk) – Alipata medali ya Dhahabu Deonatus Manyama m. 800 (wm)- Alipata medali ya Fedha Riziki Chilumba m. 100 (wk) – Alipata medali ya Fedha Aisha Kaoneka m. 100 (wk) – Alipata medali ya Shaba Faraja Meza M....
MTU anayedaiwa kubaini ushahidi wa kwanza wa mabaki ya Ndege ya Malysia iliyopotea ameelezea mazingira ya yalipopatikana mabaki hayo,na kwamba yeye alikuwa katika shughuli zake za kawaida katika hoteli moja kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi. Ni takribani miezi sita hadi sasa tangu kupotea kwa ndege hiyo huku kukiwa hakuna taarifa za uhakika kuhusu chanzo cha ajali hiyo Mabaki hayo yaliyopatikana yanapelekwa Ufaransa kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kama niya ndege ya Malaysia iliyopotea Boing 777,MH 370 iliyokuwa ikitoka Quala...
MTOTO mchanga wa kipalestina ameuawa baada ya nyumba yao kumwagiwa petroli na kuchomwa moto katika makazi ya West Bank na walioshuhudia wanawashuku walowezi wa kiyahudi kuwa ndio waliotekeleza shambulizi hilo. Inaelezwa kuwa mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu alikuwa ndani ya nyumba yao ilipomwagiwa petroli na kuchomwa. Wazazi wake na kaka yake walinusurika shambulizi hilo ambalo serikali ya Israeili imelitaja kuwa la...
VYAMA vya siasa vya upinzani nchini vimetakiwa kuwa makini katika kusimamisha wagombea hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ili kuepukana na wagombea wanaotumia fedha katika kupata madaraka. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama cha Alliance for Democratic change – ADC- Saidi Miraji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya siasa nchini ambapo ameviasa vyama kusimamia msimamo yake. Amewashauri kuwaweka wagombea ambao wanafahamu kwa undani na kuzingatia ...
KUFUATIA Tume ya Taifa ya Uchaguzi –NEC– kutangaza kuongeza siku nne za kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura kwa wakazi wa Dar es salaam kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi ulioonekana katika vituo mbalimbali vya uandikishaji, baadhi ya wakazi wa mkoa huo wameipongeza hatua hiyo. Wakizungumza na Efm leo katika vituo mbalimbali vya kujiandikisha katika Daftari hilo la kudumu la mpiga kura kwa njia ya kielektroniki,-BVR, wakazi hao wamesema uamzi huo ni wabusara nakuwataka wananchi kuitumia nafasi...
WAZIRI Mkuu wa Uingereza ameibua utata kwa kutoa maneno ya kuwafananisha wahamiaji haramu wanaojaribu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza kuwa wao ni kama kundi la nyuki. Baraza linalowashughulikia wakimbizi Nchini Uingereza limesema kuwa hiyo haioneshi thamani kwa watu na ni hatari zaidi kwa kuwa imetoka kinywani mwa kiongozi mwenye hadhi kubwa duniani. Waziri huyo mkuu ambaye yuko ziarani Vietnam alikuwa akitoa maoni kuhusiana na vurugu zinazoendelea katika mji wa Calais nchini Ufaransa ambapo mamia ya wahamiaji wamekimbia kuelekea Uingereza....
SHIRIKA la ndege la Kenya –KQ- limetangaza hasara kubwa ya Shilingi bilioni 25.7 za Kenya sawa na dola milioni 2.57 katika kipindi cha fedha cha mwaka 2014-2015. Hii ni hasara ya asilimia 661 ikilinganishwa na kipindi cha fedha cha mwaka 2013-2014 ingawa mwaka uliopita kampuni hiyo ya ndege ilitangaza kupata hasara ya shilingi bilioni 3.3. Uongozi wa shirika hilo unasema kuwa hasara hiyo kubwa imetokana na kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya Kenya ambayo imeporomoka kwa asilimia 11 ya thamani...
SERIKALI imesaini Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya fedha kiasi cha shilingi Milioni 12 laki 3, elfu sitini na mbili na 969 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini. Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa Jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania –TRA– Bernard Mchomvu kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya...
TUME ya taifa ya uchaguzi –NEC– imeongeza siku nne za kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura kwa wakazi wa Dar es salaam kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi ulioonekana katika vituo mbalimbali vya uandikishaji. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu DAMIAN LUBUVA amesema kuwa hali hiyo imetokana na uwepo wa Idadi kubwa ya watu ambao bado hawajaandikishwa na wanahitaji kuandikishwa. Jaji Mstaafu LUBUVA amebainisha kuwa...