KAMPUNI ya usafiri inayofanya safari zake kati ya Ufaransa na Uingereza ya Eurotunnel imesema maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakijaribu kuingia nchini Uingereza kupitia usafiri huo. Ripoti ya kampuni hiyo imebainisha kuwa idadi ya majaribio ya wahamiaji kutaka kuvuka mpaka kupitia usafiri aina hiyo ya usafiri imeongezeka zaidi, kwani wahamiaji hao wanajificha kwenye magari ya mizigo,kupanda vizuizi. Katika mkutano wa Mawaziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa na Uingereza uliofanyika mjini London,mbinu za pamoja kuweza kudhibiti wahamiaji hao kuvuka...
ASKOFU Desmond Tutu na mshindi wa nishani ya Nobel nchini Afrika Kusini, amerejeshwa tena Hospitali kwa matibabu zaidi. Tutu wiki iliyopita aliruhusiwa kurejea nyumbani baada ya afya yake kuonekana kuimarika ndani ya siku saba za matibabu. Hata hivyo kwa sasa Askofu tutu mwenye umri wa miaka 83 yupo katika uangalizi wa madakatari ambao wanaendelea kutibu maradhi yake....
IMEELEZWA kuwa watanzania takribani milion kumi wanatumia huduma za mtandao katika shughuli zao mbalimbali. Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau na watumiaji wa mkongo wa taifa naibu Katibu mkuu kutoka Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia CELINA LYIMO amesema kuwa mbali na kuwa idadi hiyo wizara hiyo inakusudia kupunguza gharama za watumiaji wa mitandao ili watanzania wengi waweze kutumia huduma...
BAADA ya jana kutangaza rasmi kuachana na chama cha Mapinduzi –CCM kwa aliyekuwa kada na mwanachama wa muda mrefu wa chama hicho, Edward Lowasa, na kuunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, baadhi ya Wananchi Jijini Dar es salaam wamekuwa na maoni mbalimbali kufuatia uamuzi huo. Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti Wananchi hao wamesema uamuzi aliochukua Lowasa ni mzuri na wanauunga mkono kwa kuwa maamuzi hayo yatasaidia kukuza siasa ya vyama vingi na hivyo kukuza demokrasia. ...
WAZIRI Mkuu wa Uingereza David Cameron anatarajiwa kulaani matumizi ya fedha chafu kutoka maeneo mbalimbali ya dunia zinazotumiwa kununua mali nchini Uingereza. Katika hotuba anayotarajia kuitoa nchini Singapore muda mfupi ujao waziri Cameron anatarajiwa kuahidi kufichua taarifa ya kutumiwa kwa kampuni za kununua mali za kifahari na kusema kuwa Uingereza haipaswi kuwa mahali pa fedha za wizi. Zaidi ya mali laki moja za Uingereza zimesajiliwa kwa majina ya kampuni za kigeni na zaidi ya robo ya kampuni hizo zipo jijini...
MAHAKAMA moja nchini Libya imemuhukumu kuyongwa mtoto wa aliyekuwa Rais wa Taifa hilo Gaddafi, Saif al Islam na wengine nane kufuatia uhalifu wa kivita uliohusishwa na mapinduzi ya mwaka 2011. Watuhumiwa hao walikuwa wameshitakiwa pamoja na washirika wengine wa kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani kwa kujaribu kuzima maandamano wakati wa mapinduzi hayo. Saif al Islam hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia teknolojia ya kanda ya video ambapo hadi sasa Saif anazuiliwa na kundi moja la waasi la zamani katika mji...
IMEELEZWA kuwa ili kuondokana na migongano kwenye usimamizi wa sekta ya madini Kanda ya Kaskazini, Wizara ya Nishati na Madini imeandaa mafunzo kuhusu sekta ya madini yatakayoshirikisha viongozi mbalimbali katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro yatakayofanyika Agosti 12 mwaka huu. Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Arusha Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro Fatuma Kyando amesema kuwa mafunzo hayo yatashirikisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, maafisa tawala wa wilaya, watendaji na wawakilishi kutoka Mamlaka ya...
TAASISI za Kifedha, Binafsi na Washirika wa Maendeleo nchini wameshauriwa kuzitumia nafasi zilizopo katika sekta ya nishati hususani umeme kwa kushirikiana na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini –REA– ili kujiletea maendeleo. Hayo yamebainishwa na washirika wa Maendeleo katika tasnia ya nishati, kutoka Wizara na Taasisi za Serikali kwa lengo la kujadili namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuhakikisha vijiji vinaunganishwa na nishati ya umeme. Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu...
Uongozi wa Simba Sc kupitia msemaji wao Haji Manara umetoa tamko la kuwataka mashabiki na wanachama wake kujitokeza kwa wingi kesho katika uwanja wa taifa kuishangilia timu ya Azam Fc itakayocheza dhidi ya Yanga katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kagame. Manara ametoa tangazo hilo leo wakati akizungumza na kipindi pendwa cha michezo nchini cha Sports Headquarters kinachorushwa kila jumatatu mpaka ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana kupitia...
Mkali wa r&b kutoka Marekani ambae pia ni muigizaji wa wa movie ya Fast and Furious Tyrese amevifungukia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na watu weupe nchini humo kuwa na ubaguzi wa rangi. Tyres amesema kuwa redio hizo zinapiga nyimbo za R&B/Soul ambazo zimeibwa na watu weupe tu lakini sio watu weusi ambao kimsingi ndio wanafanya vizuri kwenye chart za muziki huo akiwemo yeye mwenyewe ambae albamu yake imeshika namba moja kwenye chart za muziki wa R&B/Soul album. Tyrese...
MAREKANI imethibitisha kuwa itaendeleza mazungumzo na Uturuki kuhusu kutoa majeshi yake yanayopambana na kikosi cha kigaidi cha Islamic State huko magharibi mwa Syria. Msemaji wa idara ya Usalama wa nchi hiyo John Kirby amesema jitihada, nguvu na umoja unapaswa kuwepo kwa kuangazia zaidi katika maeneo muhimu hususani ya mipakani. Hata hivyo Askari wa Kurdish PKK wamesema kuwa shambulio la Uturuki liko juu ya Uturuki ambayo inasimamia mapambano yake dhidi ya PKK ingawa Majeshi ya Kurdish bado yanapambana na wanamgambo wa...