SHUGHULI ya kuhesabu Kura imeanza nchini Burundi kufuatia uchaguzi wa urais ambao umeshutumiwa na wengi nchini humo na hata kimataifa. Rais Pierre Nkurunzinza anatarajiwa kupata ushindi mkubwa kwa muhula wa tatu huku upinzani ukisusia kabisa kura hiyo. Huku hayo yakijiri Marekani na Uingereza wamekashifu kura hiyo wakisema kuwa haikuwa ya huru na haki. Marekani kwa upande wake imependekeza kugawana madaraka huku ikitishia kuchukua hatua dhidi ya Burundi iwapo muafaka...
MWILI wa aliyekuwa Brigedia Jenerali mstaafu Dismas Stanslaus Msilu umeagwa leo katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yanatarajiwa kufanyika Mkoani Iringa kesho. Brigedia Jenerali mstaafu Dismas alifariki dunia katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo July 19 mwaka huu. Marehemu Brigedia Jenerali Msilu alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania mwaka 1975 na Alistaafu utumishi Jeshini mwaka...
WAKAZI wa Mkoa wa Dar es salaam leo wameanza Zoezi la kujiandikisha katika Dafutari la Kudumu la mpiga kura kwa njia ya Kielektroniki- BVR. Efm imepita katika vituo mbalimbali vya kujiandikishia na kushuhudia misururu ya watu ambao wamewahi vituoni humo kwa lengo la kutimiza haki yao hiyo ya msingi kikatiba. Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi wamedai kuchelewa kwa waandikishaji katika vituo, ikizingatiwa kuwa ni siku za kazi hivyo kuiomba Tume ya Uchaguzi kulizingatia hilo ili watu wapate nafasi...
KESI ya kihistoria dhidi ya Kiongozi wa zamani wa Chad Hissene Habre iliyokuwa imerejeshwa mahakamani leo nchini Senegal sasa imeahirishwa hadi mwezi Septemba mwaka huu. Mahakama imetoa muda huo kwa wakili wapya wa kiongozi huyo wa zamani wa kimila kujiandaa kwa kesi inayomkabili ya makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili na uhalifu wa kivita. Habre ambaye amekataa kuitambua mahakama hiyo alikataa kuzungumza mahakamani huku akiwashauri wakili wake wasimwakilishe mahakamani hatua iliyomlazimu hakimu kuingilia kati na kushurutisha apewe...
BAADA ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa iliyopita hatimaye raia nchini Burundi sasa wamefika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao atakayewaongoza kwa muhula ujao. Taarifa zinasema kuwa watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura kufuatia vurugu zilizoambatana na gruneti pamoja na milio ya risasi. Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo huku viongozi wanne...
WIZARA ya Afya na ustawi wa jamii inatarajia kuwafanyia upasuaji vikope zaidi ya watu laki tano nchini kipindi kifupi kijacho katika eneo la Kanda ya Kaskazini kufuatia Wilaya za Arusha kuongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa Trkoma. Hayo yamesemwa na mratibu wa kitaifa wa mpango wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele dokta Upendo Mwingira wakati akiwapokea wageni kutoka shirika lisilo la kiserikali la Ending Neglected Disease la nchini Marekani. Akizungumza na kituo hiki Jijini Sinya Longido dokta Mwingira amesema zoezi hilo la...
MTANDAO wa Asasi za Kiraia wa Kuangalia Chaguzi Tanzania-TACCEO unaoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu umeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye mikoa mingine wakati wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kuepuka kufanya makosa hayo katika mkoa wa Dar es Salaam hapo kesho. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa mtandao huo MARTINA KABISANA amesema kuwa ni vyema NEC ikahakikisha inatatua mapema changamoto ya kuharibika...
SERIKALI ya Ugiriki imefanikiwa kuwasilisha sehemu ya malipo ya deni lake kwa Shirika la Fedha la Kimataifa –IMF– hali inayoashiria kutokuwepo tena kwenye hatari ya kufilisika. Msemaji wa –IMF– Gerry Rice amesema katika taarifa yake muda mfupi uliopita kwamba Ugiriki imelipa euro bilioni 2 jana ambapo Kamisheni ya Ulaya iliruhusu nchi hiyo kupatiwa mkopo wa euro bilioni 7 ili kuiwezesha serikali ya waziri Mkuu Alexis Tsipras kulipa sehemu ya madeni yake kwa Benki Kuu ya Ulaya na IMF. Msemaji wa...
MAMLAKA ya Ulinzi nchini Brazil katika mji wa Manaus imeanzisha uchunguzi kufuatia mauaji yaliyotokea na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 35 kati ya wiki iliyopita na siku ya jana asubuhi. Taarifa zinaeleza kwamba Mauaji hayo yalianza mara baada ya sajenti mmoja wa polisi kupigwa risasi nje ya Benki katika nji huo ambao ni mwenyeji wa michuano ya Olympic mwaka 2016. Hata hivyo Mauaji hayo yaliyoanza siku ya ijumaa usiku na kuendelea Siku ya jumatatu yamesababisha Vikosi vya usalama wa...
IMEELEZWA kuwa asillimia 70 ya wagonjwa wa saratani hupoteza maisha katika nchi zinazoendelea na katika Bara la Afrika lenye watu zaidi ya milioni 804 asilimia 12.4 wanapata saratani kabla ya kufikia umri wa miaka 75 na asilimia 90 wanapata ugonjwa huo wakiwa na umri chini ya miaka 40. Hayo yamesemwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati akifungua mkutano wa tisa wa Jukwaa la wake wa marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo...
KIONGOZI wa chama cha –ACT-Wazalendo Zitto Kabwe leo anampokea Mbunge wa Kasulu, mjini Moses Machali kutoka chama cha –NCCR-Mageuzi ambaye atajiunga na kutatambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa –ACT-Wazalendo. Machali anaambatana na Madiwani wawili, Kamishna wa mkoa mmoja na katibu wake pamoja na wenyeviti na makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu mjini., Pia katika mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea makatibu uenezi 9 wa jimbo hilo lenye jumla ya kata 15 za uchaguzi. ...