JUMLA ya watu 39 kutoka nchini Afrika Kusini wameshiriki katika zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro lenye lego la kuchangisha fedha za kusaidia Afya ya watoto wa kike huku sehemu kubwa ya fedha hizo zimelenga kusaidia watoto wa kike laki 2 na elfu 72 wa Afrika Kusini pamoja na Tanzania wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Mlima huo. Ugeni huo uliopanda Mlima Kilimanjaro Julai 14 mwaka huu umejumuisha watu mbalimbali wakiwemo wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom na waigizaji maarufu...
WATU 27 wameuawa na wengine wapatao 100 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la bomu lililotokea leo katika mji wa Uturuki wa Suruc ambao upo kwenye mpaka wa Uturuki na Syria. Mlipuko huo ulitokea kwenye bustani ya kituo cha kitamaduni majira ya saa tatu ambapo mamia ya vijana wanaripotiwa kufanya kazi kwenye kituo hicho. Maafisa wanachunguza ikiwa mlipuko huo ulisababishwa na bomu la kujitolea mhanga. Mji huo wa Suruc upo kwenye mpaka wa Uturuki na...
WAMILIKI wa vyombo vya moto hususani madereva wametakiwa kutii sheria bila shuruti kwa kufuata utaratibu wa usalama ili kuepusha madhara yanayojitokeza mara kwa mara barabarani. Rai hiyo imetolewa na Askari wa usalama barabarani eneo la Kawe WIPI HAPPY wakati akizungumza na kituo hiki leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutokea vurugu zilizosababishwa na mmoja wa madereva ambaye hakutaka kutii sheria iliyowekwa na Askari huyo. Hali hiyo imekuja kufuatia Lori la mizigo kufunga barabara ya Mwai Kibaki...
RAIS wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter na bodi ya utawala ya shirikisho hilo pamoja na viongozi wengine wa juu wa shirikisho hilo wanakutana leo kupanga tarehe ya uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo. Blatter alitangaza mwezi uliopita kuwa atajiuzulu kama rais wa FIFA baada ya wiki ya tuhuma za ufisadi kwa baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo. Mkutano huo wa leo pia unatarajia kutaja baadhi ya mambo yatakayorekebishwa ikiwa ni pamoja na kikomo cha urais na viongozi...
BAADA ya kupata mkopo wa usaidizi wa euro biloni 7 kutoka Umoja wa Ulaya,hatimaye benki nchini Ugiriki zimefunguliwa leo, baada ya kufungwa kwa wiki tatu kuepusha uchumi wa nchi hiyo kuporomoka. Hata hivyo, Vikwazo juu ya uhamishaji wa fedha nje ya nchi na udhibiti mwengine wa fedha bado vitaendelea kuwepo. Ugiriki pia inatarajiwa kulipa deni la Euro bilioni 4 kwa wakopeshaji wake Benki Kuu ya Ulaya siku ya...
BAADA ya mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uteuzi wa ndani wa nafasi ya ubunge kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo kumalizika, imeelezwa kuwa zoezi la kura za maoni linaanza leo hadi julai 25 mwaka huu. Katika hatua hiyo kila uongozi wa kanda umepanga ratiba yake ya kura za maoni katika majimbo mbalimbali kwa kuzingatia kuwa zoezi hilo limeagizwa kufanyika na kumalizika ndani ya siku 6 katika majimbo yote ya uchaguzi nchi nzima. Hata hivyo taarifa...
IMEELEZWA kuwa ili kuleta maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika majimbo mbalimbali yanayoongozwa na viongozi wa siasa nchini hususani wabunge, Viongozi hao wanapaswa kufuatilia kwa umakini shughuli zote za kiutendaji zinazofanyika kwenye majimbo yao pamoja na kuwashirikisha wananchi kikamilifu kwenye ngazi za maamuzi. Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi-CCM, CHRISTOPHER JAFET alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi...
Liverpool imekubali kumsajili mshambuliaji Christian Benteke kutoka kwa wapinzani wao kwenye Premier League klabu ya Aston Villa kwa kitita cha pound milioni 32.5. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ubelgiji mwenye miaka 24 kwa sasa anafanyiwa vipimo na daktari wa klabu ya Liverpool. Benteke aliwasili Villa akitokea Genk kwa pound milioni 7 mwaka 2012 akiwa na rekodi ya magoli 49 katika michezo 101 na klabu ya Birmingham. Liverpool inamchukua nyota huyu akiwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na...
MIRIPUKO miwili ya Volkeno iliyotokea jana imesababisha viwanja vya ndege vitatu kufungwa nchini Indonesia, kikiwamo kiwanja cha ndege cha mji mkuu wa pili Surabaya. Mlima wa Raung ulioko katika kisiwa kikuu cha Java umetoa uchafu wa majivu wa hadi mita 2,000 hewani baada ya miungurumo ya wiki kadhaa na mlima wa Gamalama mashariki mwa Indonesia uliripuka pia hapo jana baada ya miezi kadhaa ya tulivu. Miripuko hiyo imejiri katika nchi hiyo yenye idadi kubwa kabisa ya waislamu wakati ambao mamilioni...
FAMILIA yenye watoto saba iliyotelekezwa katika mtaa wa Igelegele wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza imepewa makazi ya muda na balozi wa mtaa huo baada ya kuteseka kwa muda mrefu. Akizungumza na kituo hiki mmoja wa mtoto wa familia hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Grece amesema makazi hayo ya muda yamewasaidia kwa kiasi kikubwa kwani mwanzo walikuwa wakilala nje na hawakuwa na chakula. Hata hivyo amesema kuwa kwa upande wa masomo ameathirika kwa kiasi kikubwa kwani toka shule imefunguliwa hajahudhulia masomo...
MSANII mkongwe wa muziki wa dance Tanzania, Ramadhan Masanja maarufu Banza Stone amefariki dunia leo mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu. Akizungumza na efm kwa njia ya simu, kaka wa Marehemu Jabir Masanja amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kwamba taratibu zote zinafanyika nyumbani kwao Sinza jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, Banza alikuwa anasumbuliwa na fangasi waliokuwa wanamshambulia kichwani (ubongo) na shingoni. EFM inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki na Wapenzi wa Muziki...