RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Mabalozi wa Afrika katika Umoja wa Mataifa kulitetea Bara hilo kwa sababu hamna mtu mwingine atakayetetea maslahi ya Afrika. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa kila nchi kuamua aina ya mfumo wa kisiasa ambao unaifaa nchi husika bila kulazimika kuwepo ukomo wa kiongozi kukaa madarakani. Rais Kikwete ametoa ufafanuzi huo jana wakati alipozungumza na Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao katika Umoja...
Mshambuliaji nguli wa Uruguay Alcides Edgardo Ghiggia ambaye ndiye aliyeifungia timu yake goli la ushindi dakika 10 kabla ya mchezo kwisha katika michuano ya kombe la Dunia mwaka 1950, amefariki dunia. Ghiggia mchezaji pekee aliyekuwa amesalia hai kati ya wachezaji wote wa kikosi cha kombe la dunia kilichoishinda Brazill mwaka 1950,ambapo dakika za lala salama zilizmuingiza katika historia ya kuipatia ushindi Uruguay. Mchezaji huyo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 ambaye kifo chake kinatajwa kuwa ni pigo kubwa...
Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA lina mpango wa kuzifanyia marekebisho kanuni zake ili kuzibana nchi zinazowania kuandaa Kombe la Dunia, zisitumie mwanya wa misaada ya kifedha kwa nchi nyingine kama rushwa. Kipengele kile kinachoziruhusu nchi zinazoshindania nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia kusambaza pesa katika nchi nyingine huenda kikafutwa. Aidha FIFA inazitaka nchi zote zinazowania nafasi hiyo kuzingatia haki za binadamu na sheria za kazi wakati wote. Hivi sasa nchi zinazotupiwa jicho ni Urusi inayoandaa kombe la dunia mwaka 2018...
Klabu ya soka ya Sunderland imemsajili mchezaji wa Ufaransa Younes Kaboul kutoka Tottenham, klabu hiyo ya Uingereza ilitoa taarifa hiyo siku ya jumatano. Akizungumza mara baada ya kutangazwa rasmi kujiunga na klabu hiyo Kaboul amesema amefurahi kujiunga na ametoa shukrani zake kwa uongozi mzima akiwemo mwalimu wa Sunderland kwakufanya maamuzi sahihi ya...
MTU mwenye silaha amewaua askari wanne wa jeshi la wanamaji wa Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika mji wa Chattanooga, Tennessee. Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja na Maafisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani. Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo. Kufuatia tukio hilo maeneo kadhaa yamefungwa zikiwamo hospitali na shule ili kuchukua tahadhari....
WAFANYAKAZI wa uwokoaji Nchini Nigeria wamesema katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo katika mji wa Gombe watu arobaini wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko kutokea kwenye soko katika eneo hilo. Mlipuko wa kwanza umetokea kwenye maegesho nje ya duka la viatu, na kufuatiwa na mlipuko mwingine muda mfupi baadae. Mashuhuda wa tukio hilo amesema hali ni mbaya kwenye mitaa ya...
JUMLA ya wanachama 36 wa chama cha mapinduzi-CCM-wamejitokeza kutaka kugombea nafasi za ubunge kupitia chama hicho katika majimbo manne ya Kinondoni, Kawe, Ubungo na Kibamba. Hayo yamesemwa na katibu wa –CCM– wilaya ya kinondoni ATHUMAN SHESHA alipokuwa akizungumza na kituo hiki ambapo amesema kuwa hadi sasa jimbo la Kawe linaongoza kwa kuwa na wagombea wengi wapato 15. SHESHA amesema kuwa kila mgombea aliyefika kuchukua fomu amepewa mashariti ya kugombea nafasi hiyo ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo...
SHIRIKA lisilo la kiserikali la The Foundation for Tomorrow limezindua kampeni ya kuchangia SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu lengo ni kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na mazingira yanayowakabili. Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni maalumu ya SHAMIRI inayolenga kusaidia ustawi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. Asukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki katika...
WAKATI huo huo ripoti zinasema waasi wa Houthi wamekiripua kituo cha kusafishia mafuta katika bandari ya Aden leo mchana. Mashahidi wanasema moshi mzito umetanda na wakaazi wa eneo hilo wameanza kuhamishwa. Kituo hicho cha kusafishia mafuta kilikuwa na shehena ya tani milioni moja na laki mbili ya mafuta ghafi pamoja na mapipa kadhaa ya gesi....
BUNGE la Ugiriki limeunga mkono awamu ya kwanza ya mpango wa tatu wa misaada kutoka kanda ya Euro. Wabunge 229 wameunga mkono hatua hizo zinazozungumzia miongoni mwa mengineyo kuhusu kuzidishwa kiwango cha kodi ya ongezeko la thamani ya bidhaa na kufanyiwa marekebisho malipo ya uzeeni. Wabunge 64 wameupinga mpango huo na sita hawakuupigia kura upande wowote....
JESHI la Polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke limesema kuwa limejipanga kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yote katika kipindi hiki cha sikukuu kuanzia katika maeneo ya Ibada. Akizungumza na Efm kamanda wa Polisi mkoa huo Andrew Satta amewataka wananchi kudumisha ulinzi wa mali zao katika kipindi hiki cha sikukuu ya Iddy el fitri. Kamanda Satta amewataka wananchi kutojisahau na kuacha nyumba zikiwa zimefungwa na badala yake waache mtu mzima ili kuzuia vitendo vya uhalifu....