RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan. Katika mkutano huo kwenye Hoteli ya Intercontinental, viongozi hao wawili wamezungumzia masuala mbali mbali ya kimataifa, ikiwamo hali ya Burundi. Hapo jana Mwenyekiti huyo wa Jopo la Kimataifa Linalopendekeza Jinsi Dunia inavyoweza kukabiliana na majanga yajayo ya magonjwa ya milipuko, ameongoza vikao vya Jopo hilo ambalo kazi yake imeungwa mkono na nchi 21 ambazo zilichangia mapambano...
RAIS wa Marekani Barack Obama amezungumza na mwenzake Vladmir Putin, akimshukuru rais huyo wa Urusi kwa mchango wake katika kufanikisha makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Ikulu ya Marekani ya White House imesema viongozi hao wawili waliahidi kuendelea kuwa na mawasiliano ya karibu, na watashirikiana pamoja . Lakini hakukuwa na kauli yoyote kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Ukraine....
WAZIRI wa Mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema vyombo vya usalama nchini humo vimefanikiwa kuwakamata watu wanne wanaodaiwa kupanga njama za kushambulia maeneo ya jeshi. Bernard amesema kuwa watu hao wanaoshikiliwa miongoni mwao yupo mmoja aliwahi kuwa mwanajeshi mwenye umri wa miaka 30. Idara za usalama nchini Ufaransa kwa sasa zimekuwa makini zaidi tangu kufanyika kwa mashambulizi yaliyosababisha mauaji ya watu yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa...
KATIKA kutambua umuhimu wa watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo walemavu wa vioungo mbalimbali , Madiwani wa Halmshauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wameitaka Halmshauri hiyo kujenga shule za kutosha kwa ajili ya walemavu hao. Hata hivyo wameitaka pia jamii nzima kuondokana na utamaduni wakudhani kuwa ulemavu ni mkosi katika familia na kutowaficha watu hao na badala yake wawapeleke shule kwa lengo la kupata Elimu kwani ni haki yao ya Msingi. Kauli hiyo ya Madiwani imetolewa katika kikao chao cha kuvunja...
WAUMINI wa Dini ya Kiislamu pamoja na Watanzania kwa ujumla wametakiwa kuzidisha mshikamano na umoja hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu. Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Sheikh Mkuu wa Mkoa huo ALHAD MUSSA SALIM alipo kuwa anatoa mwaliko wa kuswali pamoja swala ya idd el fitr kwa waumini wa dini hiyo katika viwanya vya mnazi mmoja ambayo itategemea na kuandama kwa mwezi kati ya tarehe 17 au 18. Alhad amesema kuwa sikukuu...
Mwimbaji wa muziki wa r&b kutoka Marekani Chris Brown huenda akapoteza nafasi aliyoipigania kwa kipindi kirefu kuishi na binti yake Royalty. Haya yanakuja mara baada ya nyumba yake kuvamiwa na kundi la waharifu hali aliyopelekea mama wa mtoto huyo kuwa na hofu ya kumpoteza mwanae atakapomuacha chini ya uangalizi wa Cris Brown kutokana na rekodi yake ya kujihusisha na makundi ya wahuni. Nia Guzman anafikiria kuwa makundi hayo kwa sasa yanamrudia Cris na kumfanyia uhalifu hivyo ni hatari kwa maisha...
Meneja wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal ametangaza uamuzi wake wa kumuuza mlinda mlango Victor Valdes huku sababu ya msingi ikiwa ni utovu wa nidhamu. Hatua hiyo inakuja baada ya mlinda mlango huyo kukataa kucheza kwenye kikosi cha pili ndani ya Manchester United. Van Gaal amesema mlinda mlango huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona ambae alimwaga wino mwezi wa kwanza atakutana utakuwa ni mwisho wake kuitumikia klabu hiyo baada ya kushindwa kufuata filosofia za meneja huyo “kama...
Ligi mpya ya kabumbu itang’oa nanga wikendi ya Agosti 23, na mechi kali za “clasico” kati ya Real Madrid na Barcelona zitachezwa Novemba na Aprili, shirikisho la soka nchini humo lilisema Jumanne. Mechi hizo kati ya mahasimu hao wa jadi zitachezwa Novemba 8 mjini Madrid na Aprili 3 mjini Barcelona, Shirikisho la Soka la Uhispania lilisema baada ya droo kufanywa makao makuu ya shirikisho hilo. Mabingwa wa ligi Barcelona watakuwa wakipigania kuhifadhi mataji ya Ligi ya Uhispania, Kikombe cha Ligi...
TAARIFA za kijeshi zimesema wapiganaji tiifu kwa upande wa rais wa Yemen wamefanikiwa kuyadhibiti maeneo kadhaa ya mji wa Aden leo, baada ya kuukomboa uwanja wa ndege wa mji huo ambao ulikuwa ukishikiliwa na waasi wa kihuthi kwa zaidi ya miezi minne. Operesheni hiyo iliyopewa jina “Operesheni ya Mshale wa Dhahabu” ni ya kwanza kupata mafanikio makubwa, tangu wanamgambo wa kihuthi walipoingia mji huo wa bandari na kumlazimisha rais Abedrabbo Mansour Hadi kukimbilia nchi jirani ya Saudi Arabia. Rais wa...
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amefanya mazungumzo ya upatanishi nchini Burundi huku rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza akijiandaa kugombea muhula wa tatu madarakani licha ya kuwepo kwa machafuko ya wiki kadhaa sasa yanayoipinga hatua yake hiyo. Museveni alikutana jana jioni na wajumbe wa serikali na viongozi wa upinzani mjini Bujumbura. Burundi imekuwa katika mgogoro wa kisiasa tangu mwezi Aprili mwaka huu baada ya chama tawala cha CNDD-FDD (cndede –fdede) kumteua rais Nkurunziza kama mgombea rasmi wa urais kwa muhula...
MWANASIASA Mkongwe na Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi- CCM -Kingunge Ngombale Mwiru ameeleza kusikitishwa kwake na mchakato mzima wa kumpata Mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho kuwa ulikua ni batili na kulikua na ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama hicho. Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipozungumza na Waandishi wa habari, ambapo amesema kwa Mujibu wa Taratibu za Chama hicho Kamati kuu ndio yenye jukumu la kuteua Tano bora katika wanachama wote waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea...