RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa linalochunguza jinsi dunia inavyoweza kujikinga na majanga ya magonjwa ya milipuko katika miaka ijayo, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili mjini Geneva, Uswisi, kwa ajili ya kuendesha vikao vya Jopo hilo. Vikao hivyo vitakuwa ni awamu ya pili kwa Jopo ambalo liliteuliwa Mwezi Aprili, mwaka huu, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Ban Ki Moon. Wajibu mkuu wa Jopo hilo ni kutoa mapendekezo ya kuimarisha mifumo...
WANASAYANSI wa NASA kutoka Marekani wanasema kuwa majaribio yao ya kurusha chombo kwenda katika sayari ya Pluto yamekuwa na mafanikio makubwa. Chombo hicho kimefanikiwa kutuma taarifa katika kituo cha utafiti huo cha Maryland zilizochukua takribani saa nne na nusu hadi kufika duniani na kupokelewa na antenna NASA. Saa chache zijazo wanasayansi hawa wa NASA wameeleza kuwa wanatarajia kupata mfululizo wa taariza zaidi na picha kutoka sayari hiyo ya Pluto ambazo zitatoa uhalisia wa undani wa sayari hiyo ya...
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni leo ameingia siku yake ya pili ya mazungumzo ya amani nchini Burundi. Ikiwa imebaki siku chache tu kufanyika kwa uchaguzi wa Rais, inaonekana kuna nafasi ndogo ya Rais Museveni kuweza kushawishi lolote kuhusiana na msimamo wa Serikali ya Burundi kuhusiana na uchaguzi wa Burundi. Mara baada ya kuwasili nchini Burundi, rais Museveni amewakumbusha raia wa Burundi moja ya jambo baya lililowahi kutokea nchini humo na ambalo halipaswi kuwepo kwa sasa ambalo ni mgawanyiko wa kikabila...
VYOMBO vya Habari nchini vimeombwa kutoa taarifa sahihi zisizo na upendeleo ili kuepuka uchochezi katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu. Akizungumza na kituo hiki Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili nchini Bonaventure Mwalongo amesema kuwa vyombo vya habari ndiyo nguzo muhimu katika kulinda Amani ya nchi kupitia shughuli zao. Amewataka waandishi nchini kuepuka ushabiki na badala yake wawaunganishe watanzania ili wafanye maamuzi sahihi katika uchaguzi mkuu kupitia taarifa sahihi zinazotolewa na vyombo...
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amechukua fomu ya kugombea Ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi-CCM. Nyalandu amechukua fomu hiyo ikiwa ni siku ya kwanza kuingia kazini baada ya kutoka kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Nyalandu anaimani kwamba akisimama kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo atashinda kwani ana vigezo vyote vinavyostahili kumpa nafasi hiyo lakini pia...
Rapa aliyewahi kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki na filamu duniani DMX amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela. Earl Simmons mwenye miaka 44, alishikiliwa katika kituo cha polisi ambapo wasemaji maafisa usalama huko Buffalo katika jiji la New York wamesema rapa huyo amefikishwa katika gereza la Erie County Holding Center. Wakieleza sababu ya Dmx kuhukumiwa kifungo hiko wamesema kuwa kushindwa kuzingatia agizo la mahakama ya usuluhishi wa masuala ya kifamilia baada ya kushindwa kuchangia matunzo ya mtoto...
MAOFISA wa Afya nchini Sierra Leone wametahadharisha uwezekano wa kutokea kwa maambukizi zaidi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ikiwa ni mwaka mmoja tangu mgonjwa wa kwanza kubainika nchini humo. Wamesema kuwa hofu ya baadhi ya watu kukataliwa na kutengwa na jamii ni moja ya sababu inayochangia kuenea kwa maambukizi hayo kwani wengi hujificha wanapokumbwa na ugonjwa huo. Hata hivyo kumekuwa na kasi ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika siku za hivi karibuni ingawa katika makao makuu ya...
MAZUNGUMZO kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yemeendelea hadi usiku wa kuamkia leo mjini Vienna kujaribu kufikia makubaliano yatakayoweza kuudhibiti mpango huo na kuizuia Iran kutengeneza silaha za atomiki. Msemaji wa ikulu ya Marekaani Josh Earnest amesema kuwa baadhi ya masuala muhimu yameshughulikiwa, lakini bado kuna masuala mengine yanayoendelea kuleta mzozo. Ikiwa kuna muafaka kuhusu vipengele vyote vya makubaliano hayo, wanadiplomasia wakuu kutoka baadhi ya mataifa makubwa ikiwemo Iran, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani...
WAKATI viongozi mbalimbali wakijitokeza kugombea nafasi za uongozi kada wa chama cha mapinduzi Mathew Yungwe ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo Bagamoyo kupitia chama cha mapinduzi –CCM-ambalo linaongozwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi dokta Shukuru Kawambwa. Akizungumza na viongozi na wanachama wa chama hicho mjini Bagamoyo mkoani Pwani Yungwe amesema ameamua kugombea nafasi hiyokwa lengo la kusukuma maendeleo ya jimbo hilo ambayo yamekwama kwa muda mrefu. Yungwe amesema kuwa mambo...
JESHI la Polisi nchini limetangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni hamsini kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa ya uhakika itakayofanikisha kukamatwa kwa majambazi waliowaua askari na raia pamoja na kuiba silaha katika kituo cha polisi cha sitaki shari kilichopo Ukonga jijini Dar es salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamishna wa Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam SULEIMAN KOVA amesema kuwa jeshi la polisi limeona ni muhimu kuwashirikisha wananchi kikamilifu kwa kutoa zawadi hiyo kwa kuwa suala la...
WAZIRI mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras anazidi kukabiliwa na upinzani huko Athens kwa hatua mpya na kali za malipo alizokubali kuzitambulisha kutokana na masharti mapya ya kuokoa kuporomoka kwa uchumi. Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Panos Kammenos ambaye anaongoza chama kidogo katika muungano wa serikali ya kitaifa ameelezea mpango huo kuwa ni mapinduzi ya serikali. Habari kutoka chama hicho zinasema kwamba mkataba uliowekwa ni wa kuifedhehesha Ugiriki nchi hiyo kwa kuwa unalitaka bunge la ugiriki kupitisha ongezeko la kodi,...