WAZIRI wa mambo ya ndani wa Mexco ameitisha mkutano wa magavana wa majimbo ili kujadili namna ya kuepusha vurugu zinazoweza kutokea kufuatia kutoroka kwa mtuhumiwa maarufu wa biashara ya dawa za kulevya. Vyombo vya usalama ndani ya Mexico na maeneo ya jirani kwa sasa vinamtafuta Joaquin Guzman ambaye ni mfanyabiashara mkubwa wa dawa hizo kwa kutoroka katika mazingira yanayodaiwa kuwa ni ya rushwa. Naye Rais wa Mexco Enrique Pena Nieto amesema kuwa ana Imani kuwa idara za usalama zitamkamata mtuhumiwa...
CHAMA cha Sauti ya Umma kimewataka wanawake wenye uwezo wa uongozi kujitokeza katika kuwania nafasi mbalimbali kwenye vyama vya siasa na kuleta uwiano sawa wa hamsini kwa hamsini katika uongozi hapa nchini ili kuiondoa asilimia 30 iliyopo sasa. Akizungumza na kituo hiki Katibu Mkuu wa Chama hicho Ally Kaniki amesema kuwa wapo wanawake wenye uwezo mkubwa wa kuongoza lakini wamekuwa nyuma na kushindwa kuthubutu kutokana na uoga na kutokujiamini. Aidha amewataka wanawake kote nchini kuondoa dhana ya kusubiri...
MGOMBEA wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi-CCM-dokta John Magufuli anatarajiwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kutambulishwa kwake. Akizungumzia suala hilo katibu wa siasa na Uenezi wa chama hicho Mkoani hapa Juma Simba amesema kuwa dokta Magufuli atawahutubia wananchi katika viwanja vya Mbagala Zakheim, hotuba itakayolenga kuonesha vipaumbele vya chama katika kipindi kijacho cha uongozi. Dokta Magufuli alipitishwa kuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia –ccm- baada...
Aliyewahi kuwa mchezaji bora wa dunia kupitia timu ya taifa ya Brazil huyu ni Ronaldinho hatimae amerudi nyumbani na kuingia mkataba wa kuitumikia timu ya Fluminense huko Rio de Janeiro nchini Brazil. Picha ya mchezaji huyu akiwa na jezi ya timu hiyo ilipostiwa kwenye mtandao wa Twitter kupitia akaunti ya klabu hiyo mapema mwishoni mwa wiki pindi alipokubali kuungana na Fred aliyewahi kuwa mchezaji mwenzake kutoka Brazil Baadae Ronaldinho alitweet kuelezea furaha yake kurudi nyumbani na kuitumikia timu...
Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati jumamosi wiki hii inaanza kutimua vumbi mjini Dar es Salaam Tanzania huku jumla ya vilabu 13 vikishiriki. Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajiwa kutoa kiasi cha dola elfu 60 za marekani kama zawadi kwa washindi. Kundi A itajumuisha timu za Yanga yaTanzania, Gor Mahia ya Kenya, Kmkm Zanzibar, Telecom ya Djibout na Khartoum- Sudani Kaskazini. Kundi B – APR Rwanda, Al Shandy ya Sudan, LLB FC Burundi naHeegan Somalia. Wakati kundi C...
TAKRIBAN wanajeshi 23 wa Urusi wameuawa karibu na mji wa Omsk ulioko Siberia baada ya jengo la kambi ya kijeshi kuporomoka. Wanajeshi wengine 19 waliokolewa kutoka ndani ya vifusi vya jengo hilo. Mwanajeshi mmoja aliyeokolewa ameileza runinga ya Urusi kwamba wanajeshi walikuwa wamelala wakati wa ajali...
VIONGOZI wa mataifa ya ulaya yanayotumia sarafu ya Euro wamekubaliana kwa pamoja kuipa Ugiriki mkopo mwingine ili kuinusuru uchumi wake kuporomoka zaidi. Makubaliano hayo yamejiri baada ya mazungumzo ya dharura baina ya mawaziri wa fedha wa ukanda wa Ulaya waliodhamiria kuiokoa nchi hiyo kiuchumi kutokana na kupungukiwa fedha. Rais wa baraza la ulaya Donald Tusk ametangaza kuwa makubaliano yameafikiwa baada ya mazungumzo hayo marefu yaliyochukua takriban saa kumi na saba ambapo amesema pia kabla ya kutumika makubaliano hayo yatahitajika...
BAADHI ya Wananchi wamekipongeza Chama cha Mapinduzi -CCM- kwa Kumpitisha Dokta John Magufuli kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya Tano kwa tiketi ya chama hicho. Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema Chama hicho kimewapatia Watanzania aina ya Mtu ambae wamekua wakimhitaji kwa kipindi kirefu kwani Watanzania wanahitaji mtu mwenye ujasiri mkubwa wa kutoa maamuzi kama alivyo Dokta Magufuli kwani mara nyingi amekua akichukua maamuzi magumu katika utendaji wake...
JUMLA ya watu saba wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao wamevamia kituo cha polisi cha Stakishari usiku wa kuamkia leo kilichopo ukonga jijini Dar es salaam. Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini –IGP-ERNEST MANGU amesema kuwa miongoni mwa watu waliouawa ni Askari 4 na raia 3 ambapo kati ya raia hao watatu waliouawa mmojawapo ni jambazi. IGP Mangu amebainisha kwamba watu wengine watatu waliokuwa katika eneo...
Na Omary Katanga. Mzozo kati ya klabu ya Simba na mchezaji Ramadhani Singano “Messi” ndiyo habari iliyochukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa,huku kila upande ukidai kuwa na haki katika kile inachokiamini. Hebu nikukumbushe kidogo mzozo huu ulipoanza,siku chache kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa klabu ya Simba ilianza kupekuwa mikataba ya wachezaji wake kujua ni yupi mkataba wake umekwisha na yupi bado,ndipo jicho la upekuzi wao likanasa kwa mchezaji Ramadhani Saingano. Hapo wakagundua...