JUMLA ya watu 11 wameuawa kufuatia shambulio lililotokea kaskazini mashariki mwa Kenya ambapo inahofiwa kuwa shambulio hilo lilikuwa na nia ya kuwalenga wafanyikazi wa machimbo ya mawe wasiokuwa wenyeji wa eneo hilo. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kuwa ilisikika sauti kubwa ya milipuko miwili kisha ikafuatiwa na milio ya risasi huku Shirika la msalaba mwekundu tayari limeshaanza jitihada za kuwaokoa majeruhi ambao idadi kamili haijulikani. Hata hivyo haijathibitishwa wahusika wa shambulio hilo ingawa kwa kipindi kirefu wanamgambo wa...
WATANZANIA wametakiwa kutofanya makosa katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuchagua wabunge watakaoweza kuhimili changamoto na kujenga hoja katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Rai hiyo imetolewa leo na Naibu katibu Mkuu wa Chama cha-Alliance For Democratic Change–ADC– Doyyo Hassan Doyyo wakati akizungumza na EFM juu ya sakata la wabunge wa Upinzani kutoka nje ya Bunge kwa kupinga miswada iliyowasilishwa bungeni kwa hati ya dharula. Aidha amesema kuwa kutokana na umuhimu wa miswada...
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-imetoa wito kwa wananchi wote wa Mikoa ya Pwani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili wapate haki yao ya kupiga Kura na kuchagua Viongozi bora katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imeeleza kwamba uboreshaji wa daftari hilo kwa mkoa wa Pwani unaanza leo hadi julai 20 mwaka huu kabla ya kuanza mkoa wa Dar es salaam. Mbali na kutoa ratiba...
Agenti wa mshambuliaji wa Uholanzi, Robin van Persie amepuuzilia mbali uvumi mteja wake amekubali kuondoka Manchester United na kujiunga na majabali wa Uturuki, Fenerbahce. Taarifa zilitapakaa wikendi iliyopita kuwa straika huyo amewekwa sokoni na miamba hao wa ligi Premier Uingereza na amekubali kufunga virago vyake kuhamia klabu hicho cha Super Lig baada ya kukubaliana matakwa binafsi. Kess Vos alikanusha ripoti hizo akisema mshambuliaji huyo nyota, 31, ataendelea kufanya matayarisho wa msimu ujao Old Trafford kama ilivyotarajiwa. “Ikiwa...
Timu ya Simba imesema Mganda Hamisi Kiiza atakuwa chachu ya mafanikio katika msimu ujao baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili Kiiza amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba ya Tanzania katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara. Kiiza aliichezea timu ya Yanga, ambayo ni mahasimu wa Simba katika msimu uliopita na baadae klabu hiyo kuamua kuachana naye. Habari kutoka SImba zinasema wana imani mchezaji huyo ataisaidia timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu katika msimu uliopita na ikiwa na...
Kutana na Debora charles mkazi wa kinondoni mkwajuni ambae ni mshindi wa shindano la sakasaka Wilaya ya Kinondoni aliyejibebea kitita cha shilingi milioni moja na nusu za kitanzania kupitia shindano hili lenye msisimko wa kipekee. Hata wewe pia waweza kuwa mshindi na kuweza kubadilisha maisha yako kwakusikiliza efm na kufuata maelekezo. Debora charles ...
MKUTANO wa tatu wa dharura kujadili mzozo na mkwamo wa kisiasa nchini Burundi uliosababisha maelfu ya raia kuitoroka nchi hiyo umeanza leo jijini Dar es salaam. Viongozi hao wakiwemo mwenyekiti na mwenyeji wa jumuiya, rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na Yoweri Museveni wa Uganda, ambao tayari wamewasili kwenye kikao hicho, wanajadili na kuwasilisha mapendekezo ya ripoti mbili kuhusu mgogoro wa Burundi. Ripoti hizo ni pamoja na ya kikosi cha pamoja cha kimataifa cha Usuluhishi wa mgogoro wa Burundi, kinachojumuisha, Umoja...
BUNGE la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi wa mwaka 2015 wenye lengo la kuwezesha nchi kunufaika na mapato yanayotokana na mafuta hayo. Awali akitoa ufafanuzi wa masuala muhimu katika muswada huo, Naibu waziri wa fedha mheshimiwa Mwigulu Nchemba amesema kuwa serikali itahakikisha mapato yote yatokanayo na mafuta yanasaidia katika kuleta maendeleo ya...
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imewahukumi kifungo cha Miaka mitatu jela Mawaziri waandamizi wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona. Hata hivyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja ameachiwa huru baada ya Mahakama kumwona hana hatia. Viongozi hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni...
MAELFU ya raia wa Ugirik usiku wa kuamkia leo wametawanyika katika mitaa ya mjini Anthens karibu na jengo la bunge, wakifurahia kura ya hapana waliyoipiga ambayo imeshinda kwa ya asilimia 60. Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras,amesema matokeo hayo ya hapana, hayana nia ya kwenda kinyume na jumuiya ya Ulaya bali yataiongezea Ugiriki uwezo wa majadiliano zaidi kuhusiana na mzozo wa madeni. Tsipras ameongeza kuwa serikali ya Ugiriki iliitisha kura hiyo ya maoni ikiamini kuwa kura ya Hapana italeta makubaliano...