Video imeongozwa na Adam Juma Audio produced by Abbah Studio: Vipaji...
Diamond ameachia rasmi video ya wimbo aliomshirikisha Mr Flavour – NaNa Audio imeandaliwa na Nahreal Video imeongozwa na God Father...
RAIS wa shirikisho la soka duniani- FIFA, Sepp Blatter,anagombea kiti cha urais katika uchaguzi wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika leo huko Zurich Uswisi. Uchaguzi huo unaendelea katika kongamano la kila mwaka la shirikisho hilo licha ya shinikizo kutoka kwa wadau Blatter ajiondoe kufuatia tuhuma za ufisadi na ulaji rushwa katika shirikisho hilo uliopelekea maafisa wakuu saba kukamatwa mapema juma hili. Blatter anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mwana mfalme kutoka Jordan Ali Bin al Hussein....
NIGERIA leo imemwapisha bwana Muhammadu Buhari kuwa rais mpya wa nchi hiyo ambako zaidi ya nchi 30 za Afrika zinawakilishwa na viongozi katika sherehe hizo. Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anahudhuria pia sherehe hizo wakati Marekani inawakilishwa na waziri wake wa mambo ya nchi za nje John Kerry,Uingereza na waziri wake wa mambo ya nchi za nje Philipp Hammond na Laurent Fabius anaiwakilisha Ufaransa. Licha ya matatizo yanayolikabili taifa hilo linalochimba mafuta kwa wingi zaidi barani Afrika,ushindi...
WAKATI Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Kimataifa -UN wakijiandaa kuwarudisha wakimbizi walioingia nchini kutoka Burundi mara baada ya hali ya usalama kupatikana, wakimbizi hao wamesema kuwa hawako tayari kurudi nchini humo kwa madai kuwa burundi siyo nchi ya kulinda amani kwa wakati wote. Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wakimbizi hao wamesema kuwa Serikali ya burundi haiaminiki hata kidogo kwani kila mara nchi hiyo imekuwa na migogoro ya hapa na pale ...
WIZARA ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa imeliomba Bunge kuidhinisha zaidi ya shilingi bilioni 154 kwaajili ya kuwezesha utekelezaji wa masuala mbalimbali muhimu ya wizara kwa kipindi cha mwaka 2015 na 2016. Akiwasilisha rasmi Bungeni makadilio na matumizi ya wizara, Waziri wa wizara hiyo BERNARD MEMBE amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha shughuli za wizara ikiwemo kuwezesha kushiriki kikamilifu katika mikutano ya kimataifa ili kuimarisha uhusiano kwa nchi za...
VIONGOZI wa nchi 17 Ulimwenguni wanakutana mjini Bangkok nchini Thailand kutafuta mbinu bora za kukabiliana na tatizo linalozidi kuongezeka la wahamiaji haramu wanaotoka Myanmar na Bangladesh maeneo ambayo nchi zake zinaoongoza kwa kuwa na idaidi kubwa ya wahamiaji. Miezi kadhaa iliyopita maelfu ya wahamiaji haramu walitua katika pwani ya mwambao wa bahari ya Indonesia, Malaysia na Thailand. Hata hivyo wengi wa wahamiaji hao walijikuta wakizama baharini huko nchini Thailand mapema mwezi huu....
RAIA 15 wa China wamefunguliwa mashitaka nchini Marekani kwa tuhuma za udanganyifu wa matokeo na nyaraka za kitaaluma walizozitumia kujiunga na elimu ya juu nchini Marekani. Kwa mjibu wa waendesha mashtaka nchini humo,wamebaini kuwa vijana hao wa China wamefanya udanganyifu wa kutumia simu wakati wa majaribio ya kujiunga na vyuo hivyo. Iwapo watakutwa na hatia kutokana na tuhuma hizo,raia hao wa China watafungwa hadi miaka 20 jela....
TANZANIA imetoa wito kwa wananchi wa Burundi kushirikiana kumaliza tofauti zao za kisiasa zinazoendelea nchini humo ili kurudisha hali ya Amani kwa manufaa yao naTaifa kwa ujumla. Wito huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa BERNAD MEMBE wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum dokta MARY MWANJELWA alitaka kufahamu jitihada za serikali katika kusaidia Amani inarejea nchini Burundi. Mheshimiwa MEMBE amesema kuwa ingawa kuna jitihada kubwa zinafanyika ili...
MWENGE wa uhuru umekabidhiwa leo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda baada ya hapo jana kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Ilala yenye gharama ya shilingi bilioni 14. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo jana, Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Juma Chumu amewataka Watanzania kutunza miradi mbalimbali ya mandeleo inayoletwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau na wananchi wenyewe. Amesema kuwa mbio za mwenge mwaka huu zinatumika katika kutoa elimu na...
Nyota ya Afrika kutoka Senegal inayong’aa ughaibuni Akon amefungua chuo kitakachotoa mafunzo ya uzalishaji wa umeme wa Solar/ nguvu ya nishati ya jua kupitia mradi wake wa Akon Lighting Africa. Katika mradi huo akon amelenga kufikisha umeme kwa waafrika wapatao milioni mia sita. Akon amezindua taasisi hiyo siku ya jumanne na kwa mujibu wa maelezo mafunzo yataanza msimu wa kiangazi huko Bamako katika mji mkuu wa Mali ambapo maengeneer na wajasilia mali wa afrika watapata ujuzi wa kuzalisha umeme wa...