MTANDAO wa kijinsia Tanazania TGNP umelaani kitendo cha baadhi ya Wabunge wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushindwa kuhudhuria Vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini dodoma huku wakitumia kodi za wananchi waliowachagua bila manufaa yoyote na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam Afisa mawasiliano kutoka TGNP MELCKDEZEL KAROLI amesema kuwa kitendo cha wabunge kutokuwepo ndani ya bunge wakati maamuzi mbalimbali yakiwa yanafanyika ni kuwanyima haki wananchi kwa kuwa wao ndio...
WATANZANIA wameshauriwa kuwa waangalifu na kuacha tabia ya kuiga matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamlaka husika kwa kuwa ni hatari kwa Afya zao. Rai hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo mheshimiwa JUMA NKAMIA kwa niaba ya Waziri wa Afya, wakati akijibu swali la mheshimiwa RIZIKI JUMA aliyetaka kufahamu jitihada za serikali katika kudhibiti tatizo hilo nchini. Mheshimiwa NKAMIA amesema kuwa ni vyema kwa kila mwananchi kuchukua...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, amemwapisha Katibu Mkuu mpya, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula. Aidha, katika sherehe fupi ya uapisho iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwapisha Balozi Hassan Simba Yahya kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo. Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Mambo ya...
WAZIRI MKUU wa Uingereza David Cameron amependekeza mbele ya mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean Claude Juncker, masharti ya nchi yake kuwa mwanachama wa Umoja huo, yabadilishwe. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika makazi ya waziri mkuu huko Chequers, David Cameron ameweka wazi kabisa Waingereza hawakubaliani na hali namna ilivyo hivi sasa. Kwa mujibu wa msemaji wa waziri mkuu wa Uingereza, mkuu wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya ameahidi kusaidia kupatikana ufumbuzi wa haki kwa Uingereza....
SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limelaumu majeshi ya Hamas huko Gaza kwa kuendesha vitendo vya kikatili na utekaji nyara, mateso na mauaji kwa raia wa kipalestina kufuatia mgogoro kati ya Israel na makundi ya wapiganaji wa Palestina katika maeneo ya mpakani. Mashambulizi hayo yaliwalenga raia wakiwatuhumu kwa kushirikiana na Israel. Amnesty imesema kwamba hali ni mbaya wakati vikosi vya askari wa Israel wakiwa katika harakati zao za mauaji ya kutisha na uharibifu kwa watu...
WAZIRI wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok amesema ushirikiano katika Nyanja za utalii,utamaduni na michezo ndio njia pekee ya kukuza uhusiano uliopo kati ya Nchi ya Zanzibar na Malawi. Ameyasema hayo wakati alipokutana na Balozi mpya wa Malawi Nchini Tanzania Hawa Ndilowe alipofika ofisini hapo kwa kujitambulisha kwa waziri huyo. Amesema ushirikiano huo utafanya mataifa yao kutembeleana katika Nyanja hizo na kubadilisha mawazo Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk katikati akiwa katika...
WAZIRI wa Uchukuzi mheshimiwa SAMWEL SITTA ameagiza meneja wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini-SUMATRA-mkoa wa Katavi kushughulikia haraka tatizo la utozwaji wa nauli zisizo idhinishwa na mamlaka hiyo katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo. Mheshimiwa SITTA ametoa agizo hilo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Nkasi mheshimiwa ALLY KESSY aliyetaka kufahamu uhalali wa nauli hizo kutoka kwa mamlaka hiyo. Mbali na hayo waziri amesema kuwa ni muhimu kwa Sumatra katika kila...
Kiungo wa Real Madrid Gareth Bale ameelezea matarajio yake ya kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo msimu ujao, japokuwa kumekuwepo na tuhuma nyingi kutoka kwa mashabiki wa Madrid na baadhi ya vyombo vya habari nchini Hispania kutoridhishwa na kiwango cha mwanandinga huyo ikilinganishwa na pesa zilizotumika kumnunua. Bale ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter huku timu hiyo ikitangaza kuachana na kocha wake Carlo Ancelotti. “nitajituma katika kipindi hiki ambacho msimu umeisha na kutazama mbele juu ya kurejea tena kwenye...
ASKARI mmoja ameripotiwa kujeruhiwa baada ya kuwepo kwa mapambano makali kati ya Polisi na wanamgambo wa Al Shabaab Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Kenya Wizara ya usalama wa Taifa nchini Kenya kupitia kwa msemaji wake MWENDA NJOKA imethibitisha kuwa askari mmoja amejeruhiwa wakati wa shambulizi la wanamgambo hao katika kijiji cha Yumbis. Wakati huo huo AL SHABAAB wamekiri kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi 20 lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo sio ya...
SHIRIKA la kimataifa la utafiti wa Saratani limebaini kuwa binadamu kuwa na uzito mkubwa katika umri mdogo kunaweza kusababisha ugonjwa wa saratani ya utumbo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mtafiti wa masuala ya saratani kutoka shirika hilo la kimataifa RACHEL THOMSON zinasema kuwa uzito wa kupita kiasi unaweza kusababisha Kansa ya utumbo kwa kuwa kuna uhusiano wa karibu wa uzito mkubwa na ugonjwa huo. Uchambuzi uliochapishwa kwenye jarida moja unaonyesha kuwa vijana wadogo wapo hatarini mara mbili zaidi kupata...
SHIRIKA la kimataifa la kuhudumia watoto la Save the children leo limewakutanisha watoto pamoja na viongozi wa vyama vya Siasa nchini kwa ajili ya kusikiliza maoni ya watoto hao ili kuingiza katika ilani zao za uchaguzi pamoja na kutoa tamko la watakachofanya baada ya miaka 5 ijayo. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam amesema kuwa kwa sasa wanafanya utaratibu wa kukutana na vyama vya Siasa ambavyo vimeshiriki katika mchakato wa uchaguzi na kuweza kuchukua maeneo 10 ambayo...