Slider

BRENDAN RODGERS: HATMA YANGU IPO KWA WAMILIKI WA LIVERPOOL
Slider

Kocha wa klabu ya Liverpool, England Brendan Rodgers amesema yupo tayari kuondoka klabuni hapo, pale tu wamiliki wa timu hiyo watakapomtaka kufanya hivyo. Liverpool imejikuta ikiaibishwa kwa kukubali kichapo cha bao 6-1 kutoka kwa Stoke City katika mchezo wa kufunga pazia la ligi kuu ya England, lakini pia mchezo huo ndio ulikuwa wa mwisho kwa nahodha Steven Gerrard. “mengi yamepita mwaka huu ambayo yameifanya kazi kuwa ngumu. Msimu uliopita wakati mambo yalipoenda vizuri, tuliungwa mkono na kila mtu, lakini kiwango...

Like
399
0
Monday, 25 May 2015
ETHIOPIA: CHAMA TAWALA KINATAZAMIWA KUSHINDA UCHAGUZI MKUU
Global News

UPIGAJI  kura umesogezwa hadi leo Jumatatu katika baadhi ya maeneo nchini Ethiopia, ili kuruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki katika uchaguzi mkuu ambao chama tawala kinatazamiwa kushinda kwa kishindo na kuendeleza utawala wake. Jana Jumapili, wapigakura wa upinzani walidai kuwepo na unyanyasaji na hata vurugu katika baadhi ya vituo vya kupigia kura. Karibu asilimia 80 ya wapigakura milioni 35 wa Ethiopia walijiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo ambao wengi wanahisi matokoea yake tayari yanajulikana, katika taifa ambako chama tawala...

Like
245
0
Monday, 25 May 2015
WABUNGE WA VITI MAALUM WATAKIWA KUELEKEZA NGUVU KUGOMBEA NAFASI ZA UBUNGE MAJIMBONI
Local News

WABUNGE wa Viti maalum Nchini wametakiwa kuelekeza Nguvu katika kugombea nafasi za ubunge Majimboni kama ilivyo kwa wanaume badala ya kuendelea kutegemea kupata nafasi hiyo kwa kuteuliwa. Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoani Singida CHRISTOWAJA MTINDA wakati akizungumza na EFM ambapo amesema wakati wa Wanawake kusubiri kuteuliwa umepitwa na wakati hivyo ni vyema kufanya jitihada za kutosha kuwatumikia wananchi. MTINDA amesema Umefika wakati ambapo wanawake wanapaswa kuonyesha kwa vitendo kuwa wanaweza kupitia kugombea nafasi...

Like
472
0
Monday, 25 May 2015
SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA ZA MABASI YAENDAYO KASI NA FLYOVER
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea kuchukua jitihada za kutosha katika kuhakikisha inakamilisha miradi ya ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi na za flyover ili kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es salaam. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi dokta JOHN MAGUFULI wakati akijibu swali la mbunge wa kinondoni mheshimiwa IDD AZZAN aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali katika kutekeleza miradi hiyo. Waziri MAGUFULI amesema kuwa jitihada za kufanikisha miradi hiyo zinaendelea kuchukuliwa  ambapo hadi sasa kuna...

Like
241
0
Monday, 25 May 2015
SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA WIKI YA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA ZAANZA LEO
Local News

SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la umoja wa Mataifa-UNESCO– kwa kushirikiana na wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo nchini wameungana kuongoza sherehe za wiki ya kumbukumbu ya wiki ya ukombozi wa bara la Afrika zinazoanza leo hadi mei 29 mwaka huu maeneo mbalimbali ya Afrika. Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika hilo sherehe hiyo hufanyika kila ifikapo mei 25 ya kila mwaka ndani na nje ya bara la Afrika kukumbuka siku ambayo viongozi wa bara hilo walipokutana mwaka...

1
251
0
Monday, 25 May 2015
MALINZI USIONE HAYA KUMPA “MAKAVU” KOCHA STARS
Slider

  Na Omary Katanga. Ni jambo la kuhuzunisha kuona timu yetu ya taifa Taifa Stars,ikigeuzwa kama pombe ya ngomani kila mmoja anajinywea atakavyo,huku maneno ya kutia moyo kutoka kwa viongozi wa shirikisho la mpira nchini TFF yakiendelea kushika hatamu. Tangu mwanzoni uamuzi wa rais wa TFF,Jamali Malinzi wa kuvunja mkataba wa kocha Kim Polsen (Denmark) na kukubali kulipa mamilioni ya shilingi kama fidia ili aondoke na kumleta kocha wa sasa Martin Nooij (Uholanzi),ulipokelewa kwa shingo upande na wadau wa soka....

Like
282
0
Monday, 25 May 2015
AUSTRALIA HAITAWARUHUSU ROHINGWA KUISHI
Global News

AUSTRALIA imeonya kuwa haitawaruhusu wakimbizi wa jamii ya waislamu wa Rohingya waliowasili nchini humo kwa mashua kuishi. Waziri mkuu, wa nchi hiyo Tony Abbott, anasema kuwa ni muhimu mataifa ya magharibi kutafuta mbinu ya kuzuia ulanguzi wa watu. Anasema, njia pekee ni kuhakikisha kuwa hakuna mashua ambayo inawabeba wahamiaji hadi katika taifa lolote la magharibi....

Like
299
0
Thursday, 21 May 2015
AL SHAABAB WAVAMIA MSIKITI GARISSA
Global News

VIONGOZI Kaskazini mwa Kenya wamesema kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi kutoka Somalia la Al Shaabab waliuteka msikiti mmoja katika kaunti ya Garissa kwa masaa kadhaa. Wapiganaji hao waliwahutubia waumini waliokuwa msikitini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea msituni. Waliikosoa serikali ya Kenya na kuonya waumini dhidi ya kuwa majasusi wa serikali ya...

Like
272
0
Thursday, 21 May 2015
SERIKALI YASHAURIWA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA MAHAKAMA
Local News

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya katiba, sheria na utawala bora imeishauri serikali kuwajengea uwezo watumishi wa mahakama pamoja na kuwapatia mahitaji yote muhimu ikiwemo vitendea kazi bora ili kufanikisha utendaji wao wa kazi. Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Bukoba mheshimwa JASSON RWEIKIZA ambapo amesema kuwa uwekezaji wa kutosha katika sekta hiyo ya mahakama ni muhimu kwa kuwa ni miongoni mwa chombo maalumu cha kuleta haki na usawa...

Like
236
0
Thursday, 21 May 2015
KUBUKUMBU YA MIAKA 19 TANGU KUZAMA KWA MELI YA MV BUKOBA
Local News

TANZANIA leo inakumbuka miaka 19 tangu kutokea kwa ajali  ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba ambayo ilizama siku kama ya leo mwaka 1996 ambapo zaidi ya watu elfu moja walipoteza maisha yao. Tangu kuzama kwa meli ya Mv Bukoba limebaki kuwa tukio la kihistoria ambalo athari zake ziko wazi kwa mamia ya familia waliopoteza ndugu na wategemezi wao. Inakadiliwa zaidi ya watu 1000 walikufa kutokana na Meli hiyo kudaiwa kuwa ilijaza kuzidi uwezo...

Like
417
0
Thursday, 21 May 2015
VIKOSI VYA UFARANSA VIMEWAUA WAPIGANAJI WANNE WA KIJIHADI MALI
Global News

VIKOSI maalum kutoka Ufaransa vimewaua wapiganaji wanne wa kijihadi, wakiwemo viongozi wawili katika shambulizi lililofanyika eneo la kaskazini mwa Mali. Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi nchini Ufaransa mmoja wa wale waliouwawa ni Amada Ag Hama, anyeshukiwa kuhusika katika utekaji nyara na mauaji ya wanahabari wawili wa Ufaransa mwaka 2013. Ufaransa iliwatuma wanajeshi wake nchini Mali miaka miwili iliyopita wakati wanamgambo wa kiislamu walipotishia kuuteka mji mkuu, Bamako. Wanajeshi 3,000 wa kikosi cha ufaransa bado wapo katika eneo hilo...

Like
182
0
Thursday, 21 May 2015