WAZIRI MKUU wa Maysia Najib Razak amesema kuwa taifa lake litaanzisha operesheni ya kutafuta na kukomboa mashua za wahamiaji wa kabila la Rohingya katika bahari ya Andaman. Aidha amebainisha kuwa misaada ya kibinadamu kadhalika itatolewa kwa uchukuzi wa barabarani na majini. Tangazo lake limekuja baada ya maafisa kuzuia mashua za wahamiaji hao kuingia katika maji ya Malaysia, na wakati mwingine kuziondoa kwa kuzikokota kutoka maji hayo kwa majuma...
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, kimesema ripoti za CAG ambazo zimeanika ufisadi katika maeneo yaliyokaguliwa ikiwemo Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, mashirika ya umma na miradi ya maendeleo, kwa mara nyingine zimedhihirisha wazi kile ambacho CHADEMA imekuwa ikisema kwa muda mrefu kwamba ufisadi huo unaoendelea kulitafuna taifa na kuwafanya Watanzania wazidi kuwa maskini. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na chama hicho kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene, Chadema kimepokea kwa masikitiko...
JAMII imetakiwa kufuatilia kwa makini zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na kushiriki ipasavyo kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo itagundua kasoro yoyote katika zoezi hilo ili hatua stahiki zichukuliwe. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu mheshimiwa MIZENGO PINDA wakati akijibu swali la mbunge wa Mkanyageni mheshimiwa MOHAMED MNYAA juu ya uwepo wa uandikishaji wa watu wasiohusika kupiga kura hususani Zanzibar katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo. Waziri PINDA amesema...
Klabu ya Sunderland na Arsenal jana wametunushiana misuli baada ya kutoka 0-0 na hivyo kufanikiwa kuondoa mashaka ya kushuka daraja msimu huu katika ligi ya England. Hata hivyo kwa matokeo hayo Arsenal wanashika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City katika ligi hiyo inayomalizika. Hata hivyo katika mchezo huo Sunderland wanapaswa kujilaumu kwa nafasi ambayo walipata na kushindwa kuitumia kupitia mshambuliaji wake Steven Fletcher. Mlinda mlango Costel Pantilimon ndiye aliyeibuka shujaa katika mchezo huo kutokana na uwezo aliouonyesha kwa...
RAIS wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi . Sababu ya hatua hiyo ni mgogoro wa kisiasa unaoikumba nchi hiyo ndogo ya eneo la maziwa makuu. Msemaji wa rais huyo, Willy Nyamitwe ameliambia Shirika la habari la Reuters, kwamba Rais Nkurunziza amechukua uamuzi huo baada ya kupendekezwa na tume ya uchaguzi na kufuatia pendekezo kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na Jumuiya ya kimataifa kutaka uchaguzi uahirishwe. Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa kitisho cha kuzuka machafuko...
WATANZANIA wametakiwa kuepuka kuandika au kutaja takwimu zisizo rasmi kwani vitendo hivyo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria mpya ya takwimu ya mwaka 2015. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu ofisi ya Takwimu Dokta Albina Chuwa amesema takwimu bora husaidia serikali yoyote duniani kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi wake hivyo ni bora kuwekwa kwa chombo maalum kinachotoa takwimu kama ilivyo kwa ofisi ya Taifa ya Takwimu. Ameeleza kuwa ni vyema takwimu...
WIZARA ya maendeleo ya mifugo na uvuvi nchini imewasilisha rasmi makadilio ya matumizi yake katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015 hadi 2016 yanayokadiliwa kuwa ni zaidi ya bilioni 68 kwa lengo la kuboresha na kuimarisha utendaji kazi kwa maendeleo ya Taifa. Akiwasilisha makadilio hayo Waziri wa wizara hiyo dokta TITUS KAMAN amesema kuwa endapo fedha hizo zitapitishwa, zitaisaidia Wizara katika utekelezaji wa shughuli muhimu kwa kipindi cha mwaka mzima kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi....
SERIKALI ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni- UNESCO inatarajia kuadhimisha wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika Mei 25 hadi 29 mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Assah Mwambene ,amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe. Katika ufunguzi huo, Mwambene ameeleza kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa...
RAIS wa Ukraine Petro Poroshenko amesema kuwa hamuamini kiongozi wa Urusi Vladimir Putin katika harakati za kuleta Amani Mashariki mwa Ukraine. Akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC, Poroshenko anasema anahofia kwamba huenda kukawa na kutoku elewana kati ya mataifa hayo mawili. Hata hivyo ameielezea hali hiyo kuwa ni vita kamili kati ya nchi hizo. Vladimir Putin ...
MAWAZIRI wa Mambo ya Nje wa Thailand, Malaysia na Indonesia wanafanya mkutano wa dharula mjini Kuala Lumpur kujadili tatizo la wahamiaji haramu katika ukanda wao. Nchi hizo tatu zinakabiliwa na shinikizo la kimataifa kuwasaidia maelfu ya wahamiaji waliokwama Baharini ambao wanahitaji chakula na maji. Wahamiaji wengi ni waislamu wa jamii ya Rohingya waliokimbia Myanmar, lakini Serikali ya nchi hiyo imekataa kuhudhuria mkutano huo. Bado kuna hofu kuhusu usalama wa waliokwama baharini....
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya nchi imewataka wabunge kushirikiana vyema na wizara hiyo katika kuhakikisha wanatoa hamasa kwa wananchi ili wapate mwamko wa kuchangia ujenzi wa vituo vya polisi katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha usalama. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa wizara hiyo mheshimiwa PEREIRA SILIMA wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu jimbo la Mbeya dokta MARY MWANJELWA aliyetaka kufahamu jitihada za ujenzi wa kituo cha polisi cha Ilembo mkoani humo....