RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA KIKWETE anafungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi –OGP. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inaeleza kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” unafunguliwa leo na kuhitimishwa kesho mei 21, katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Lengo la mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa masuala...
Klabu ya soka ya Inter Milan imetangaza kumuwania kiungo wa Manchester United Yaya Toure kwa kitita cha pound milioni 15 katika kipindi cha miaka mitatu. Inter imepanga kumpatia kiungo huyo pound milioni 4.3 baada ya makato ya kodi katika mshahara. Toure mwenye miaka 31 anatarajiwa kuthibitisha mpango wake wa kuondoka kwenye klabu ya Manchester City mapema wiki ijayo kwenye tamati ya msimu wa ligi Klabu ya Manchester City kwa upande wake imesisitiza kuwa haitasukumwa na uhamisho badala yake inampango wa...
Rais wa Afrika kusini JACOB ZUMA amesema uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Burundi mwezi ujao unapaswa kuahirishwa hadi Amani itakaporejea nchini humo. Rais ZUMA ameyasema hayo wakati akitoa muhtasari wa matokeo ya mkutano wa eneo la kusini mwa Afrika uliofanyika nchini Angola. Mkutano huo maalum uliitishwa baada ya jaribio la mapinduzi kushindwa nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza , ambaye uamuzi wake wa kugombea kipindi cha tatu cha ...
SHIRIKA la Nyumba la Taifa-NHC– kwa kushirikiana na kampuni ya CELCOM limezindua kituo cha Huduma kwa wateja kwa njia ya simu na malipo ya kodi kwa mfumo wa simu za mkononi. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo NEHEMIA MCHECHU amesema kuwa kituo hicho kitasaidia kufikisha huduma kirahisi kwa wateja wao kwa kupiga simu ambayo haitatozwa kiasi chochote cha fedha. MCHECHU ameongeza kuwa huduma hiyo pia itasaidia uwajibikaji kwani mitambo iliyofungwa inasafirisha...
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA KIKWETE anatarajia kufungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi –OGP. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu inaeleza kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” utafanyika Mei 20 hadi 21 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Aidha taarifa imeeleza kuwa dhumuni la mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa...
RAIS wa Msumbiji mheshimiwa FILIPE NYUSSI ameahidi kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ili kuleta manufaa ya kutosha kwa wananchi wan chi hizo mbili. Rais NYUSSI ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akiwahutubia wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni hatua ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu aliyoifanya nchini tangu mei 17 mwaka huu. Mbali na hayo mheshimiwa NYUSSI amewaasa watanzania kuilinda na kuiendeleza amani iliyopo kwa kuwa ni hazina...
Star wa muziki kutokea Nigerian Davido amebahatika kumpokea mtoto wa kike baada ya mpenzi wake Sophie Momodu kujifungua mtoto wa kike siku kadhaa zilizopita Idadi ya mastar wa Afrika wanaotarajia kupata watoto inazidi kuongezeka ambapo mbali na Diamond kutoka Tanzania, Tiwa Savage kutokea Nigeria pia amefanya baby shower ikiwa ni maandalizi ya kumpoea mtoto wake Sherehe hiyo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu wa msanii huyo akiwemo Elohor Aisien ambae baadae alishea taarifa hizo kwenye ukurasa wake wa instagram na kuweka...
UKOSEFU wa Takwimu sahihi katika Masuala mbalimbali umeelezwa kuchangia kutopiga hatua kwenye mipango ya Kimaendeleo inayopangwa na Serikali juu ya Wananchi. Aidha upotoshaji wa Takwimu hizo unaofanywa na baadhi ya Watendaji kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe, pia umekuwa ukichangia kuchelewa hatua za Kimaendeleo. Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar, AMINA SHAABAN,wakati akifungua Semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mjini hapa. Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia...
UONGOZI wa Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania wameshauriwa kuwa makini katika Ujenzi unaoendelea wa Jengo la kutua na Kupaa Ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere -JNIA. Ujenzi huo unaotarajiwa kuongeza uwezo wa Uwanja wa mara tatu zaidi umejikita katika sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya abiria kupumzika, sehemu ya abiria kupanda na kushuka kwenye ndege, Ofisi za Uhamiaji na huduma nyingine muhimu. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo SULEIMAN SULEIMAN amesema Kiwanja cha Kimataifa cha...
BAADHI ya Wagombea waliotangaza nia kuwania Ubunge katika majimbo mbalimbali mkoani Arusha kupitia CCM,walionekana kupigana vikumbo na wengine wakijinadi mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli EDWARD LOWASSA. LOWASSA,ambaye anatajwa kuwania Urais kupitia CCM mwaka huu aliendesha harambee ya Ujenzi wa Msikiti wa Patandi uliopo Wilayani Arumeru mkoani Arusha,akimwakilisha makanu wa Rais,Dokta MOHAMMED BILLAL na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Milioni 200 ikiwa ni zaidi ya makisio ya Msikiti huo. Baadhi ya Watia Nia...
SERIKALI imewaasa vijana kujiepusha na ngono zembe ikiwa ni pamoja na kujiepusha na matumizi ya dawa zakulevya ili waweze kujiletea maendeleo yao na kujiinua kiuchumi. Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa mafunzo elekezi ya jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwa vijana wa halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Amesema vijana kujihusisha na ngono Zembe na Matumizi ya Dawa za kulevya kutawafanya kuwa dhaifu na kushindwa kuchangia katika Ujenzi wa taifa...