Klabu ya Barcelona jana ilishuka dimbani mjini Paris wakiwa wageni wa Paris st Germen ya Ufaransa. Katika mchezo wa awali Barcelona iliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Paris st Germen pia hapo jana wababe hao waliendeleza vipigo dhidi ya Wafaransa hao baada ya kuwakandamiza bao 2-0,zilizowekwa kimiani na Mbrazil Neymar katika kipindi cha kwanza.Kwa matokeo hayo Barcelona imefuzu nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-1 katika mchezo mwingine uliochezwa hapo jana,Baada ya kuchezea kichapo cha cha bao...
HALMASHAURI ya Kimataiafa ya safari za baharini IBM imetoa ripoti yake ya hivi punde kuhusu uharamia. Halmashauri hiyo inasema kuwa uharamia sasa umeripotiwa Kusini Mashariki mwa bara Asia, huku Meli ndogo za kusafirisha mafuta zikishambuliwa baada ya kila wiki mbili. Kwenye ripoti yake ya kila baada ya miezi mitatu, IMB inasema kuwa licha ya kupungua kwa mashambulizi kote duniani miaka ya hivi majuzi, visa vya uharamia viliongezeka katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2015....
WANANCHI wa Kisarawe 2 Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam wametakiwa kutumia Wataalamu waliosajiliwa na Shirika la Umeme Nchini- TANESCO,kufanya Wayaring katika nyumba zao ili kuondoa usumbufu wakati wa usambazaji wa huduma hiyo Majumbani. Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata hiyo ISSA HEMEDI ZAHOR katika mkutano na Wananchi, wakati wa Makabidhiano ya Transfoma kwa ajili ya kusambaza umeme kwa Kata hiyo iliyotolewa na Kampuni Property International. Diwani ZAHORO amesema kupatikana kwa kifaa hicho muhimu ni kiashirio tosha kuwa umeme...
MTANDAO wa Jinsia Tanzania –TGNP umewataka Wanawake nchini kuacha tabia ya kuwa tegemezi na badala yake wajishughulishe na kujikwamua kiuchumi ili kuepukana na ukatili wa Kijinsia unaowakabili baadhi ya Wanawake wategemezi. Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa TGNP DEO TEMBA, alipokuwa akizungumza na Kituo hiki juu ya upingaji wa Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto. Amesema kuwa, katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huo, umebaini kuwa, kwa asilimi kubwa ukatili wa Kijinsia unawakabili Wanawake ambao...
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, kimesema hakina tatizo na Wawekezaji kuwekeza katika nchi yetu kwani hakuna nchi inayoweza kuendelea bila kujenga mahusiano na Nchi zingine. Pia CHADEMA, hakipotayari kuona Taifa linaingia Mikataba isiyokuwa na Maslahi kwa Watanzania. Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Chama hicho Dokta WILBROAD SLAA, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage NYERERE akitokea Nchini Marekani kwa ziara Maalumu ya...
Kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers yupo kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kutwaa taji lolote katika misimu mitatu ya mwanzo ya kuwanoa vijogoo hao wa Anfield. Hii ni rekodi ambayo haijawahi tokea kwa kocha yeyote tangu mwaka 1950 ndani ya kikosi hicho. ,Je ni wachezaji wasiokidhi viwango?,au ni mbinu za kocha zilizogota mwisho?hayo ni baadhi ya maswali ambayo bado hayana majibu,huku Brendan Rodgers hata kama anakula basi chakula hakishuki uzuri kwani hajui nini hatima yake kufuatia kuboronga...
ETHIOPIA imeanza siku tatu za maombolezi ya Kitaifa kwa heshima za raia wake waliouawa na Wanamgambo wa kundi la Islamic State nchini Libya. Bendera zitapepea nusu mlingoti wakati pia bunge la nchi hiyo litakutana kujadili hatua ambazo litachukua kufuatia mauaji hayo ya raia wake zaidi ya Ishirini. Msemaji wa serikali REDWAN HUSSEIN, amesema kuwa waathiriwa hao wanaaminika kuwa wahamiaji waliojaribu kusafiri kwenda barani...
Habari za hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Mosri amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kuwachochoea wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood kuwaua waandamanaji wa upinzani alipokuwa madarakani mwaka...
JAMII nchini imetakiwa kujielekeza katika suala la ulinzi na usalama kwa watoto, kwa kutoa taarifa za Ukatili wanaofanyiwa. Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Afisa Ustawi wa jamii Kitengo cha familia Emma Komba wakati alipokuwa akizungumza na kituo hiki . Amesema kuwa tatizo kubwa kwa sasa jamii imekuwa waoga kutoa taarifa za ukatili zinazowakabili watoto hasa ukatili wa kingono kwa watoto katika ngazi ya...
IMEELEZWA kuwa jumla ya Kina Mama Milioni 1 na laki 6 Nchini Tanzania wanakadiriwa kuugua ugonjwa wa Fistula huku kukiwa na ongezeko la wagonjwa Wapya Elfu 3 kila mwaka wanaougua ugonjwa huo kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo uzazi usio salama. Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na CCBRT, nchini Tanzania kuhusiana na Ugonjwa huo, umeonyesha kuwa katika kipindi cha miaka 12 iliyopita Tanzania ilikadiriwa kuwa na wagonjwa Elfu 24 mpaka Elfu 30 wanaougua ugonjwa wa Fistula huku wengi wao wakipata ugonjwa...
Big Sean na Ariana Grande wamwagana baada ya miezi nane ya kuwa kwenye mahusiano na chanzo cha karibu na wasanii hawa kimeeleza kuwa kuachana kwao hakuhusiki kabisa na tukio lilitokea wiki chache nyuma. Katika moja ya show za Ariana Grande wiki kadhaa nyuma alionekena akicheza na Justine Bieber huku akiwa ameshikwa kimahaba na msanii huyo hali iliyozua minong’ono ya hapa na pale huku wengine wakisema wawili hao wapo mbioni kuingia kwenye mahusiano. Tunaelezwa kuwa kuachana kwao ni katika...