Wanachama kumi wa shirikisho la soka la Amerika ya kaskazini, America ya kati na muungano wa visiwa vya Caribbea (Concacaf) kwa pamoja wamefikia maamuzi ya kumuunga mkono Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter katika uchaguzi wa FIFA hapo May. Azimio hilo la kumuunga mkono Blatter limefanywa katika mkutano wa (Concacaf). Rais wa chama cha soka cha jamhuri ya Dominic Osiris Guzman, amemfananisha rais huyo wa FIFA na watu mashuhuri walioweka historia duniani ikiwemo Moses, Abraham Lincoln na Martin...
Mwimbaji Chris Brown kwa sasa huenda asisike tena kwenye vyombo vya habari kwa mabaya ikiwemo kuhusishwa na fujo katika club anazotembelea ama kufanya show kama ilivyozoeleka nah ii inatokana na msanii huyo kutambua thamani yake kama mzazi. Cb kwa sasa amekuwa karibu zaidi na motto wake Royalty mwenye umri wa miezi kumi, kupitia akaunti yake ya instagram cris amepost picha yake yake akiwa na mtoto huyo huku wakiwa wenyefuraha zaidi Wataalamu wa mambo wanasema kwamba ukaribu huo wa Cris kwa...
Kuelekea mchezo wa Yanga na Etoile du sahel utakaopigwa katika uwanja wa taifa hapo kesho tayari timu ya Etoile du sahel imewasili jijini Dar es salaam katika hali isiyokuwa ya kawaida kocho wa timu hiyo amekataa kuongea na waandishi wa habari. Nahodha wa timu ya Yanga Nadir Haroub Cannavaro kwa upande wake akizungumza na sports headquarters ya Efm amesema mpira ni mchezo wa makosa hivyo wamejipanga vyema ili kuwezakufanya vizuri katika mchezo wa kesho Nahida huyo pia akizungumzia timu kwa...
Rapa Lil Wayne anakabiliwa na kesi ya kujibu baada ya kushtakiwa na aliekuwa dereva wa gari la msafara wa show yake ya mwaka 2014 summer concert tour. Mark Jones amemtuhumu Lil Wayne kwakutaka kufanya jaribio la kumuua wakati anaendesha msafara wa msanii huyo na kikosi chake ambapo dereva huyo amedai kuwa Wayne alikuwa akitumia lugha za vitisho anapotoa maelekezo ya msafara huo mfano alipotaka kwenda hotelini alimfuata na bunduki na kuiweka sawa kisha akamuamuru afuatishe matakwa yake la sivyo...
Ikiwa zinahesabika siku na masaa kuelekea kwenye pambano linalosuriwa kwa hamu ulimwenguni kati mmarekani Floyd Mayweather na mfilipino Manny Pacquiao, Mayweather ameendelea kutamba na kumfanya azidi kuzungumziwa na vyombo vya habari duniani Taarifa kutoka jarida la Forbes la nchini Marekani zinasema Mayweather atatumia kifaa cha kulinda meno (mouth Guard) chenye gharama ya dola za kimarekani elfu ishirini na tano....
Kwenye usiku wa Ulaya jana michezo miwili ilichezwa katika hatua ya robo fainali ambapo FC Porto ya Ureno waliwakaribisha Bayern Munich ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Bayern Munich kukubali kichapo cha 3-1. Huko nchini Ufaransa pia Paris Saint German ilikuwa mwenyeji wa miamba ya soka ya Hispania Barcelona ambapo mchezo huo ulimalizika kwa PSG kukubali kichapo cha 3-1 katika uwanja wa nyumbani. Magoli ya Barcelona yalitiwa nyavuni na Neymar Jr huku Luis Suárez akiziona nyavu za PSG mara mbili magoli...
POLISI mjini London wamekuwa wakiupekua msikiti mmoja ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi wake wa mauaji ya Imam mmoja wa zamani kutoka Syria. Abdul Hadi Arwani alipigwa risasi na kuuawa wiki moja iliopita katika makazi ya Wembley mjini London. Msemaji wa polisi amesema kuwa maafisa wamekuwa wakiwasiliana na wawakilishi wa jamii ya waislamu ili kuwahakikishia kwamba upekuzi huo ni muhimu, na kwamba msikiti huo utafunguliwa haraka iwezekanavyo. Abdul Arwani ameripotiwa kuwa mpinzani wa rais Assad wa Syria. Watu wawili wamekamatwa kuhusiana...
SERIKALI ya Kenya imeahidi kuwasamehe wakenya ambao wamepokea mafunzo ya kigaidi endapo watajitokeza katika kipindi cha siku 10 zijazo. Waziri wa Usalama wa Mambo ya Ndani, Jenerali mstaafu Joseph Nkaissery ambae pia amewaonya wazazi wa vijana kama hao kwamba watachukuliwa hatua kali endapo hawataijulisha serikali kuhusu kujiunga kwa wanao na kundi la Al Shabaab. Serikali imewapa wale wote waliopokea mafunzo kutoka kwa Al Shabaab siku kumi kujisalimisha katika ofisi za wasimamizi wa miji ya Garissa, Mombasa au Nairobi....
CHAMA cha Demokrasia na maendeleo -CHADEMA- Kimeitaka Serikali kuongeza nguvu ya Kupambana na Ajali za Barabarani kama ilivyo katika vita dhidi ya Mauaji ya Walemavu wa Ngozi kwani ajali zimekuwa na mchango mkubwa wa kumaliza nguvu kazi ya Taifa kila siku. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho kwa Upande wa Bara John Mnyika amesema badala ya Serikali kuwa ni sehemu ya kutuma salamu za rambirambi pindi ajali zinapotokea ni vyema...
MTU mmoja amefariki Dunia, na wengine ishirini kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha basi kampuni ya Air Jordan na gari ndogo baada ya kuacha njia na kuanguka katika eneo la migua wilaya ya Nzega mkoani Tabora. Efm imezungumza na kamanda wa mkoani humo Suzan Kaganda, amesema kuwa chanzo cha awali cha kutokea kwa ajali hiyo kinaonesha ni mwendo kasi wa basi hilo ambalo lilikuwa likitokea jijini Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam. Kamanda Kaganda ameeleza kuwa hadi sasa maiti imeshatambuliwa na ndugu...
MIILI ya watu nane wakiwemo wanafunzi sita wa shule ya msingi Kibirizi, Manispaa ya Kigoma, Ujiji, Mwalimu mmoja na Mkazi mmoja wa eneo la Bangwe, waliofariki jana baada ya kupigwa na radi imeagwa leo mchana katika Viwanja vya shule hiyo ya Kibirizi. Pamoja na Viongozi na wananchi, Shughuli hiyo pia imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya ambaye ametumia nafasi hiyo kutoa salamu zake za rambirambi kwa wanakigoma, pamoja na familia zilizopoteza wapendwa wao....