Raheem Sterling arejesha matumaini kwa klabu ya soka ya Liverpool kuingia kwenye top four kwenye ligi ya Uingereza lakini pia kujihakikishia nafasi kwenye msimu ujao wa ligi ya mabingwa baada ya kuichabanga 2-0 klabu ya Newcastle United katika uwanja wa Anfield hapo jana. Kikosi cha Newcastle United kilimpoteza nahodha wa timu hiyo Moussa Sissoko alietolewa nje ya mchezo kwa kadi kwenye dakika ya saba Sterling mwenye umri wa miaka 20 ameingia kwenye wakati mgumu kufuatia kunaswa kwa video inayomuonesha akivuta...
Kufuatia matokeo mabaya iliyoyapata klabu ya Manchester City kwenye mchezo wake na klabu ya Manchester United siku ya jumapili ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Manchester United kuichabanga Man City bao 4-2, ikiwa ni mchezo wa sita kwa klabu ya man City kuupoteza kati ya michezo nane. Akizungumza na kituo cha Bbc mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na Manchester Utd, Phil Neville ametoa utetezi wake kwa Yaya Toure wa Manchester City kwa kusema kuwa mwanandinga huyo si...
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR limepewa muda wa miezi mitatu kuifunga kambi ya wakimbizi mashariki ya Kenya na kuwarejesha kwao wakimbizi zaidi ya laki nne wa kisomali la sivyo serikali ya Kenya itawahamisha. Kauli hiyo imetolewa na Makamo wa rais wa Kenya William Ruto ambaye amesema Serikali ya Kenya inasema kambi ya Dedaab imegeuka kituo cha usajili cha wafuasi wa itikadi kali wa Al Shabab-waliowauwa zaidi ya watu 148 wiki iliyopita katika chuo kikuu cha Garissa Akihutubia...
UCHAGUZI Mkuu nchini Sudan umeanza leo huku dalili zikionesha kwamba Rais wa sasa wa nchi hiyo OMAR AL BASHIR anatarajiwa kushinda kiti hicho cha Urais. Taarifa zinasema kuwa Vyama vingi vya upinzani vimesusia uchaguzi huo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ukandamizaji wa kisiasa unaoendeshwa na rais OMAR AL BASHIR. Hata hivyo inaaminika kuwa Rais BASHIR alifanya kampeni kubwa akihutubia mikutano ya hadhara sehemu tofauti za taifa hilo kubwa na kwamba ndiye kiongozi pekee wa nchi aliyewekewa hati ya kukamatwa na...
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni PAUL MAKONDA ameunda tume huru inayojumuisha wataalamu wa mikataba, wasanifu na wahandisi na maofisa kutoka vyombo mbalimbali vya uchunguzi kuchunguza juu ya ubovu wa barabara za wilaya ya Kinondoni ili kujua kama usanifu wa barabara unazingatia viwango. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Wilaya hiyo amesema wananchi wamekuwa wakiilaumu serikali kushindwa kusimamia na kukagua miradi ya barabara hali inayosababisha ongezeko la barabara mbovu. Makonda amebainisha kuwa Wananchi...
WATANZANIA leo wanakumbuka kuzaliwa kwa aliyekuwa Mwasisi wa Taifa hilo na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alizaliwa tarehe 13 mwezi wa nne mwaka 1922 katika familia ya kichifu. Hayati Nyerere ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, alizaliwa, kulelewa na kukua kama watoto wengine wa vijijini akiwasaidia wazazi wake kwa shughuli za kilimo na kuchunga mifugo, moja ya shughuli muhimu za Kiuchumi kwa jamii ya Wazanaki kutoka kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara. Akizungumzia kumbukumbu...
shindano la shika ndinga lilimalizika kwa kuwapata washiriki kumi watakaowakilisha wilaya hiyo kwenye fainali ambapo kati yao wakiume watano na wakike watano shindano hilo litaendelea wiki hii kwa wakazi wa wilaya ya Temeke kuchuana vikali kwakupiga simu na kujibu maswali watakayoulizwa na kujipatia nafasi ya kushiriki shindano hilo. zifuatazo ni picha za washiriki waliochuana vikali wilaya ya Ilala siku ya jumamosi ...
Mama mzazi wa Beyonce mwenye umri wa miaka 61, Tina Knowles amefunga ndoa na muigizaji Richard Lawson mapema mwishoni mwa wiki kwenye boti maalum katika ufukwe wa Newport huko marekani. Hii ni harusi ya pili kwa Tina Knowles ambae alifungua kesi ya madai ya taraka mwaka 2009 kutoka kwa baba mzazi wa Beyonce ambae pia alikuwa meneja miaka ya nyuma bwana Mathew Knowles Mwezi Octoba Tina ambae pia ni mbunifu wa mavazi aliweka wazi mahusiano hayo na muigizaji huyu Richard...
KIONGOZI wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance, DA, amesema hatagombea katika uchaguzi wa chama hicho mwezi ujao. Helen Zille amesema ni wakati muafaka kwake kutogombea, akisema kuwa DA watanufaika na mchango wa vijana. Atabaki kuwa waziri mkuu wa jimbo la Western Cape hadi mwaka 2019. Zille, ni mwandishi wa habari wa zamani na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi amekiongoza chama hicho tangu mwaka...
KUFUATIA Malalamiko ya Wananchi wa Mbezi Mwisho kata ya Tegeta A kuhusu kupandishwa kwa nauli za daladala kiholela hasa nyakati za asubuhi na jioni Serikali ya Mtaa huo imepiga marufuku magari yote yanayopandisha nauli kuendelea kutoa huduma ya usafiri. Akizungumza katika Mkutano na Wananchi wa Kata hiyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta A Marko Maginga amesema imekuwa ni desturi ya magari yanayotoa huduma ya usafiri kutoka Mbezi mwisho kwenda Goba mpakani katika eneo hilo la Tegeta A kupandisha...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameungana na maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Shinyanga, kuhudhuria Ibada rasmi ya kumweka wakfu na kumsimika Askofu mpya wa Jimbo hilo, Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu. Rais Kikwete aliwasili kwenye Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga jana kwa ajili ya Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wasaidizi 38, akiwamo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama...