Slider

MEEK MILL AKABILIWA NA KESI YA KUJIBU
Entertanment

  Rapa Meek Mill anakabiliwa na kesi ya kujibu baada ya kupuuza onyo ama katazo lililotolewa na mmiliki wa eneo la moja ya mabangaloo maarufu nchini marekani glass mansion linalopatikana Beverly Hills. Katika onyo hilo lilitolewa na mmiliki huyo lilimtaka Meek kutofanya party ya aina yoyote itakayoleta mkusanyiko wa watu kwenye eneo hilo   Katika mkataba waliowekeana na Meek Mill mmiliki huyo ameelezea kipengere kilichosainiwa na Meek kwamba asifanye party eneo hilo ambapo uongozi wa kampuni ulionya kutofanyika kwa Grammy...

Like
248
0
Thursday, 09 April 2015
PLATINUM FC YAIPONGEZA YANGA KWA USHINDI WA 8-0 DHIDI YA COASTAL UNION
Slider

Katika michezo ya ligi iliyochezwa jana Yanga imeifunza adabu ya timu ya Coastal Union kwakuitandika magoli 8-1. Huenda Yanga iliutumia mchezo huo kama salamu kwa vigogo wa Tunisia Etoile du Sahel, ambao siku za usoni watakutana katika kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora. Katika kipindi cha kwanza cha mchezo hadi mapumziko Yanga ilikuwa mbele kwa magoli 3-0. Katika kiindi cha pili cha mchezo Amisi Tambwe alifunga magoli 4, huku Simon Msuva, Salem Telela na Mliberia Kpah Sherman wakiona nyavu...

Like
335
0
Thursday, 09 April 2015
AFCON 2017: STARS YAKABILIWA NA KIBARUA KIZITO
Slider

shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF jana limetangaza makundi ya timu yatakayoshiriki kwenye kombe la mataifa Afrika maarufu kama Afcon kwa mwaka 2017 yatakayofanyika huko Gabon. katika makundi hayo timu za Afrika Mashariki hususani Tanzania zina kazi ya ziada kuhakikisha wanapambana vikali kutokana na timu walizopangiwa RATIBA YA MAKUNDI AFCON 2017 Group A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti Group B: Madagascar, DRC, Angola, CAR Group C: Mali, Equatorial Guinea, Benin, South Sudan Group D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoros...

Like
279
0
Thursday, 09 April 2015
WAZIRI MKUU WA UGIRIKI AWASILI MOSCOW KUFANYA MAZUNGUMZO MAALUM
Global News

WAZIRI Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, amewasili mjini Moscow kukutana rais wa Urusi Vladimir Putin kwa mazungumzo maalum. Ugiriki inasema kuwa mazungumzo yao yatajadili uhusiano kati ya muungano wa bara la Ulaya na Urusi. Uhusiano huo ulidorora kwa kiasi kikubwa katika siku za hivi karibuni kufuatia mzozo wa Ukraine. Wachanganuzi wanasema kuwa Ugiriki inapania kuboresha uhusiano na Moscow hasa ikiwa uhusiano wao na wadeni wao bara Ulaya wa kuikopesha pesa ukishindikana ambapo kesho nchi hiyo inatakiwa kulipa deni la dola...

Like
236
0
Wednesday, 08 April 2015
UGANDA: WATU KADHAA WASHIKILIWA KUFUATIA MAUAJI YA MWENDESHA MASHTAKA JOAN KAGEZI
Global News

UGANDA inasema imekamata watu kadhaa kuhusiana na mauaji ya mwendesha mashtaka Joan Kagezi yaliyotokea wiki iliyopita. Mwendesha mashtaka huyo aliuawa na watu waliokuwa na bunduki wakitumia pikipiki na polisi kuanza uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo. Kutokana na matukio ya kigaidi katika nchi jirani ya Kenya, polisi Nchini Uganda wamekuwa wakichukua tahadhari dhidi ya matukio yoyote...

Like
282
0
Wednesday, 08 April 2015
BALOZI SEIF ALI IDDI ASISITIZA MSHIKAMANO MIONGONI MWA WATANZANIA
Local News

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi, amesema Watanzania wanaoishi Zanzibar na Bara, wataendelea kushirikiana kwa miaka mingi zaidi kutokana na mwingiliano wao wa kidamu. Balozi Seif Ali Iddi amesema uwepo wa ushirikiano huo ndio njia pekee itakayotoa fursa kwa Watanzania hao kusaidiana katika kutatua changamoto zinazowakabili miongoni mwao na vizazi vyao. Balozi Iddi ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa ujirani...

Like
442
0
Wednesday, 08 April 2015
VIJANA WATAKIWA KUJIAJIRI
Local News

VIJANA nchini wametakiwa kuacha kubweteka na kusubiri kuajiriwa na badala yake wajiajili wenyewe kwa ujasiliamali pamoja na kilimo cha kisasa. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara wa kutembelea shamba lenye ukubwa wa Ekari 300 lililopo katika kijiji cha Ngarambe wilayani Mkuranga mkoani Pwani ambalo linamilikiwa na Shirikisho la Wasanii Tanzania-  SHIWATA,  Mwenyekiti wa Mtandao huo Casim Taalib amesema kuwa mashamba hayo  ni fursa nzuri kwa vijana kujiajiri. Taalib amesema vijana wamekuwa na dhana tofauti ya kusubiri...

Like
891
0
Wednesday, 08 April 2015
MAREKANI: AFISA WA POLISI AHUKUMIWA KWA MAUAJI YA MTU MWEUSI
Global News

WAKUU katika jimbo la South Carolina nchini Marekani wamemhukumu Afisa mmoja wa polisi mweupe, kwa kosa la mauaji. Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumpiga risasi raia mmoja mweusi na kumuuwa. Mkanda wa video unaonesha mtu mmoja, WALTER SCOTT, akipigwa risasi alipokuwa akimkimbia Afisa huyo.  ...

Like
285
0
Wednesday, 08 April 2015
MADEREVA WA MABASI NA MALORI YA MIZIGO WAPANGA KUFANYA MGOMO MKUBWA
Local News

MADEREVA wa mabasi ya abiria na malori ya mizigo nchini,wako kwenye mikakati mizito ya kuingia kwenye mgomo mkubwa, unaotarajiwa kuanza Ijumaa. Makakati huo unalenga kushinikiza Serikali kuingilia kati na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu malalamiko yao dhidi ya Mamlaka za serikali, ikiwemo kikosi cha usalama Barabarani na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na nchi Kavu-SUMATRA. Aidha madereva hao wameomba kukutana na Waziri wa Uchukuzi,SAMWEL SITTA,ili kuwasilisha malalamiko yao na kwamba ombi hilo likishindikana,hakutakuwa na maongezi zaidi...

Like
935
0
Wednesday, 08 April 2015
JESHI LA ZIMAMOTO LATOA MISAADA KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA
Local News

JESHI la Zimamoto na Uokoaji mkoani Iringa,limetoa misaada mbalimbali kwa Kituo cha kulelea watoto Yatima Cha Sister Theresia, kilichopo Tosamaganga. Akikabidhi msaada huo,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoani humo,KENNEDY KOMBA,amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwa karibu na jamii. Amesema Watoto Yatima,wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kupata  mahita muhimu ikiwemo chakula, Afya na malazi, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia ili kuondokana na hali ya utegemezi....

Like
432
0
Wednesday, 08 April 2015
NDESAMBURO ATARAJIWA KUPELEKA HOJA BINAFSI BUNGENI KUHUSU MAUAJI YA JAMES JOHN
Local News

MBUNGE wa Moshi Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, PHILEMON NDESAMBURO, anatarajia kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge kuhusu mauaji ya JAMES  JOHN. Katika hoja hiyo,NDESAMBURO anatarajia kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuliambia Bunge sababu zinazolifanya Jeshi la Polisi kushikwa na kigugumizi kuwakamata watuhumiwa waliohusika katika mauaji hayo. JOHN, ambaye alikuwa meneja wa Baa na Car wash ya Mo-Town iliyopo Mjini Moshi Mjini,anadaiwa kutekwa June 09 mwaka 2009 na Ndugu Wanne wakiongozwa...

Like
305
0
Wednesday, 08 April 2015