WAZAZI nchini wametakiwa kuacha tabia ya kudharau mikakati mbalimbali ya serikali kuhusu afya za watoto na badala yake wawapeleke kupata chanjo na kuchunguza afya zao. Aidha wazazi pia wametakiwa kuwapeleka watoto wenye chini ya umri wa miaka 15 katika zahanati na vituo mbalimbali vya afya kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi. Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha akina mama na watoto wa zahanati ya Arafa Ugweno iliyopo Tandika jijini Dar es salaam Latifa...
SERIKALI imeahidi kuendelea na utekelezaji madhubuti utakaowezesha kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya kutoka mkoani Kigoma hadi Kasuru kwa lengo la kuboresha miundombinu katika mkoa huo. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa JOHN MAGUFULI wakati akijibu swali la mbunge wa Muhambwe mheshimiwa FELIX MKOSAMALI aliyetaka kujua utekelezaji wa serikali juu ya suala hilo. Waziri Magufuli ameahidi kuwa wizara itahakikisha inakamilisha ujenzi wa barabara...
SHIRIKA la ndege la Ujerumani, Lufthansa limetoa tangazo kuhusu taarifa lilizokuwa nazo juu ya matatizo ya kiakili ya Andreas Lubitz, rubani msaidizi wa ndege ya Germanwings iliyopata ajali ambaye anadhaniwa kuiangusha ndege hiyo kwa makusudi, na kuuwa watu wote 150 waliokuwemo. Shirika hilo limesema kwamba Lubitz, mwaka 2009 aliiarifu shule ya marubani ya shirika hilo, kwamba siku za nyuma alikuwa na matatizo makubwa ya msongo wa mawazo. Tangu kutokea kwa ajali hiyo Jumanne wiki iliyopita, taarifa nyingi zimekuwa zikijitokeza kuhusu...
WAKAZI wa Kinondoni mkoani Dar es salaam,wametakiwa kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa Utulivu na Amani bila kufanya fujo. Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, AUGUSTINO SENGA,wakati akizungumza na Efm,ofisini kwake. Kamanda SENGA amesema ni vema wananchi kutumia Sikukuu hiyo kwa kusherehekea kwa Amani na Utulivu na kurejea nyumbani, kwani kinyume na hapo, jeshi la polisi litawachukulia hatua....
IMEELEZWA kuwa hujuma zinazofanywa na baadhi ya Wafanyabiashara nchini, zimeendelea kuigharimu Serikali kwa kuikosesha mapato. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya Wafanyabiashara hao kuingiza bidhaa ambazo, zimekuwa zikilipiwa Ushuru mdogo. Kwa muda mrefu sasa, kumekuwepo na wimbi la Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es salaam, ambapo huandikisha taarifa na maelezo tofauti na bidhaa halisi zilizomo ndani ya makontena, ili kuwawezesha kukwepa kodi kwa kulipia kiasi...
SERIKALI imeondoa Muswada wa Mahakama ya Kadhi uliokuwa uwasilishwe. Katibu wa Bunge Dokta THOMAS KASHILILLAH,amesema Muswada huo hautakuwa kwenye orodha ya shughuli za Bunge. Amesema Suala la Mahakama ya Kadhi, lilikuwa lijadiliwe kwenye Muswada wa Mabadiliko ya sheria ndogo, ambao ulikuwa kwenye orodha ya kujadiliwa leo, hivyo nafasi ya Muswada huo itatumika kuendelea kujadili Miswada iliyoanza kujadiliwa....
Katika michezo ya kirafiki kwa mataifa usiku wa kuamkia leo , Italy imekuwa mwenyeji wa England Kikosi cha Italy kimekuwa na rekodi yakutofungika kirahisi tokea michuano ya kombe la dunia mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare moja ya magoli 1-1 katika michezo mingine iliyochezwa jana Uholanzi ililipa kisasi cha fainali za mwaka 2010, baada ya kuisambaratisha Hispania bao 2-0. Ureno wakicheza bila Christian Ronaldo, walikiona cha moto baada ya kuadhibiwa nyumbani bao 2 kwa nunge dhidi ya Cape Verde,...
Andy Murray amekuwa Mwingereza wa kwanza kuweka historia ya kushinda mara 500 katika mchezo wa tenis baada ya kumshinda Kevin Anderson kutoka Afrika Kusini. Murray alishinda kwa seti 6-4 3-6 6-3 na kuwa mchezaji wa 46 kushinda mara 500 tangu kuanzishwa kwa mashindano ya wazi. Akizungumza na kituo cha BBC Murray alisema amefurahishwa na ushindi huo alioupata huko Miami sehemu ambayo ameitumia kwa muda mrefu kwakufanya mafunzo na kujinoa kwa ajili ya michuano yake, Pia ameongeza kuwa atautumia ushindi huo...
Huu ni wimbo uliyotayarishwa katika studio za Vipaji Tz chini ya Producer Abba Artist : Muzdy ft Rich Mavoko Song: Mboni yangu unaweza kuusikiliza na kudonwload hapa ...
MATOKEO ya awali ya kura zilizopigwa siku ya Jumamosi huko Nigeria zinaonesha kuwa Kiongozi wa upinzani MUHAMMADU BUHARI anaongoza kwa zaidi ya Kura Milioni Mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni Rais GOODLUCK JONATHAN. Generali BUHARI wa chama cha All Progressives Congress -APC anaonekana kupata matokeo mazuri mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos. Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache zinazokuja wakati majimbo yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo...
POLISI Mkoani Katavi inamshikilia mkazi wa kitongoji cha Ntumba , Kijiji cha Mnyengele Wilayani Mpanda , DEOGRATIAS PASTORI kwa kumjeruhi mkewe kwa kumkata mkono wa kushoto na kupasua tumbo la Mgoni wake kwa panga . Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , DHAHIRI KIDAVASHARI amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku katika kitongoji cha Ntumba kijiji cha Mnyagala Kata ya Mnyagala Wilayani Mpanda. KIDAVASHARI amewataja majeruhi hao kuwa ni pamoja na Mke wa mtuhumiwa TABU NESTORY, MASAGA ELIAS ambao ...