Slider

SERIKALI YATOA TAMKO JUU YA ADHA YA MAJI DAR
Local News

SERIKALI imetoa tamko kuhusu utekelezaji wa upatikanaji wa huduma ya Maji safi na uondoaji wa maji taka katika jiji la Dar es salaam ili kupunguza adha na matatizo wanayoyapata wakazi wa jiji ambao idadi yake inaongezeka kila siku. Akizungumza wakati wa kutoa hoja hiyo  Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Maji Profesa JUMANNE MAGHEMBE amesema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kuona ukubwa wa Tatizo hilo jijini,kufatia hoja binafsi juu ya tatizo hilo iliyowahi kutolewa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo...

Like
255
0
Tuesday, 31 March 2015
MUSWAADA WA SHERIA YA KUUNDWA KWA BARAZA LA VIJANA UMEHITIMISHWA LEO BUNGENI
Local News

MJADALA kuhusu Muswaada wa Sheria ya Kuundwa kwa Baraza la Vijana Tanzania umehitimishwa leo Bungeni Mjini Dodoma, ambapo Waziri na Naibu Waziri wenye dhamana ya Vijana wamepata nafasi ya kupitia hoja mbalimbali zilizotolewa na Wabunge juu ya kuundwa kwa Mabaraza hayo. Akizungumza Bungeni Mjini  Dodoma  Waziri wa Habari,Utamaduni Vijana na Michezo Dokta FENELA MUKANGALA amesema Muswaada huo umekuwa halali baada ya kua umefuata taratibu sahihi tangu hatua ya awali ya kufanyiwa  matayarisho hadi kufikia hatua ya kupelekwa Bungeni. Amebainisha...

Like
327
0
Tuesday, 31 March 2015
UZINDUZI WA TIDAL KAMPUNI YA JAY Z INAYOTARAJIWA KULETA MAPINDUZI
Entertanment

Mastar wakubwa duniani katika tasnia ya muziki wameunganisha nguvu pamoja na katika uzinduzi wa kampuni ya muziki ya Tidal. Katika uzinduzi huo wa kampuni ya kwanza kubwa ya muziki duniani kumilikiwa na msanii Jay z uliofanyika siku ya jumatatu katika jiji la New York ulishuhudiwa na mastar ambao pia wametajwa kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hiyo Miongoni mwa mastar hao ni Rihanna, Madonna, Beyonce, Usher, Daft Punk, Arcade Fire, Jack White na Kanye West. Akizungumzia matarajio yake juu ya...

Like
565
0
Tuesday, 31 March 2015
OBAMA KUZURU KENYA JULAI MWAKA HUU
Global News

RAIS BARACK OBAMA wa Marekani ataizuru Kenya mwezi Julai mwaka huu. Hiyo itakuwa ziara yake ya kwanza akiwa Rais. Taarifa Zaidi I meeleza kuwa nchini Kenya, Rais OBAMA ambaye baba yake ni Mkenya atahudhuria mkutano wa Kilele wa Kimataifa wa wajasiriamali. Mkutano huo utafanyika Kati ya Julai 24 na...

Like
264
0
Tuesday, 31 March 2015
CUF YATARAJIA KUMTANGAZA MAHARAGANDE KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE MOROGORO MJINI
Local News

KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, imeelezwa kuwa Chama  cha Wananchi CUF kinachounda Umoja wa Katiba wa wananchi –UKAWA, kinatarajia kumsimamisha MBARARA MAHARAGANDE kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Morogoro mjini. Akizungumza na Kituo hiki MAHARAGANDE amesema kuwa anauhakika wa kushinda nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba  mwaka huu kwa kile alichodai kuwa wananchi wa Morogoro wamepania kufanya mabadiliko. Amesema kuwa wananchi wamechoshwa na ahadi zisizotekelezeka huku...

Like
407
0
Tuesday, 31 March 2015
WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATANGAZA UGUNDUZI WA GESI ASILIA KWENYE BAHARI KUU YA TANZANIA
Local News

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetangaza ugunduzi wa Gesi Asilia katika Miamba ya Mchanga kwenye Kisima kinachochimbwa na Statoil cha Mdalasini-1 kwenye Bahari Kuu ya Tanzania. Waziri wa Nishati na Madini, GEORGE SIMBACHAWENE amebainisha hayo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma baada ya kuthibitishwa na Makamu wa Rais wa Statoil, NICK MADEN pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania -TPDC. Statoil ni Mkandalasi katika Leseni ya Utafutaji ya Kitalu namba 2 kwa niaba ya TPDC...

Like
350
0
Tuesday, 31 March 2015
TIGER WOODS AWEKA MATUMAINI YA KURUDISHA KIWANGO CHAKE
Slider

Aliyekuwa kinara kwenye mchezo wa gofu duniani Tiger Woods ameporomoka katika viwango vya dunia vya mchezo wa gofu baada ya kutolewa katika orodha ya mia bora. Eldrick Tont Woods ambae ni raia wa Marekani hii ni mara kwanza kushuka kiwango katika historia yake ya kipindi cha uchezaji wa mchezo huo. Woods ambaye ni bingwa mara 14 aliingia mia bora kwa mara ya kwanza mwaka 1996 ameweka rekodi ya kuwa bingwa wa dunia kwa wiki 683, lakini sasa ameteremka mpaka nafasi...

Like
251
0
Tuesday, 31 March 2015
LEWIS HAMILTON AONGEZA MKATABA KUITUMIKIA MERCEDES
Slider

Bingwa wa dunia wa mbio za magari Lewis Hamilton anatarajiwa kusaini mkataba mpya wiki hii utakaomwingizia zaidi ya pound milioni 27 kwa mwaka. Hamilton mwenye umri wa miaka 30 raia wa Uingereza amekuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa kampuni ya magari ya Mercedes ambapo dili hilo nono kwa dereva huyu lipo kwenye hatua za mwisho kumaliziwa na wanasheria. Hamilton amesema mchakato wa kusaini mkataba huo utamalizika wiki hii wala hakuna sababu itakayokwamisha kwani hakuna makubaliano yaliyoachwa hivyo mchakato huo umekamilika...

Like
302
0
Tuesday, 31 March 2015
TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LARIPOTIWA KATIKA PWANI YA PAPUA NEW GUINEA
Global News

TETEMEKO la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha Richter 7.6 limeripotiwa kwenye pwani ya Papua New Guinea. Tetemeko hilo limetokea asubuhi ya leo katika eneo hilo la Asia Pasifiki. Kituo cha Pasifiki cha tahadhari kuhusu tetemeko na Tunami lilikuwa limeonya juu ya uwezekano wa kutokea mawimbi yenye hatari katika masafa ya kilomita 1,000 kutoka kitovu cha tetemeko hilo. Ingawa hakuna uharibifu uliotarajiwa kutokana na tetemeko hilo, nchi za eneo zima zikiwemo Papua New Guinea, visiwa vya Solomon, New Zealand, Mashariki...

Like
251
0
Monday, 30 March 2015
NIGERIA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI LEO JIONI
Global News

ZOEZI la kuhesabu kura linaendelea nchini Nigeria katika uchaguzi wa rais na wabunge ambao ulifanyika siku ya Jumamosi na jana Jumapili. Kwa kiasi kikubwa uchaguzi ulifanyika kwa amani, licha ya mashambulizi kadhaa katika eneo la kaskazini, ambayo kundi la Boko Haram limeshutumiwa kuyafanya huku kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Nigeria, Muhammadu Buhari, akitarajiwa kumpa changamoto kubwa rais wa sasa Goodluck Jonathan katika uchaguzi huo. Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa urais nchini...

Like
331
0
Monday, 30 March 2015
MKAPA ATARAJIWA KUHUDHURIA TAMASHA LA PASAKA DAR
Local News

RAIS wa  awamu  ya tatu, Benjamin  Mkapa  anatarajiwa kuwa ni  mmoja  wa  waalikwa  wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka huu kwenye  uwanja  wa  Taifa  jijini Dar es Salaam. Kwa  mujibu  wa  Mwenyekiti  wa  Kamati  ya  maandalizi  ya  tamasha  hilo, Alex  Msama   Mheshimiwa Mkapa  ni kiongozi wa kitaifa ambaye anastahili kuhudhuria tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake. Msama  amesema  Viongozi wengine waioalikwa, ni Askofu  Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,...

Like
251
0
Monday, 30 March 2015