KANSELA wa Ujerumani, ANGELA MERKEL na Waziri Mkuu wa Ugiriki, ALEXIS TSIPRAS wamesisitiza nia yao ya kuondoa mvutano uliopo kati ya serikali zao. Hayo wameyaeleza katika mkutano wao na Waandishi wa Habari uliofanyika mjini Berlin. TSIPRAS amezuru rasmi Ujerumani kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani mwezi Januari mwaka...
JUMUIYA ya Wazazi jimbo la Temeke, wamemkabidhi Mbunge wa Temeke, ABBAS MTEMVU kiasi cha Shilingi 200,000 kwa ajili ya kuchukua Fomu ya kugombea tena nafasi hiyo ya Ubunge. Akimkabidhi fedha hiyo kwa Niaba ya Jumuiya hiyo, Mwenyekiti SUDI MLIRO amesema kuwa hatua hiyo inatokana na ushirikiano unaofanywa na Kiongozi huyo kwa wananchi wake na kusababisha kupatikana kwa maendeleo ya haraka ndani ya jimbo. Katika hatua nyingine Mbunge huyo,amekabidhi Pikipiki 20 kwa kila Kata katika jimbo hilo kwa lengo la kurahisisha...
TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wawekezaji na Marais wa nchi 5 za Ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Machi 25 hadi 26 mwaka huu. Akitoa taarifa ya mkutano huo Mkuu wa wa Mkoa wa Dar es salaam, SAIDI MECK SADIKI amesema kuwa,Marais hao PAUL KAGAME wa Rwanda, PIERRE NKURUNZINZA wa Burundi, YOWERI MUSEVENI wa Uganda, UHURU KENYATTA wa Kenya na JOSEPH KABILA wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, watahudhuria mkutano huo wakiwa wameambatana na ...
KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel anakutana leo na waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras , ambaye amemlaumu kansela kwa kusisitiza kuhusu hatua ya kubana matumizi kwa nchi yake ambayo imesababisha mzozo wa kiutu wa umasikini pamoja na ukosefu mkubwa wa ajira. Viongozi hao wa Ugiriki na Ujerumani wanakutana mjini Berlin baada ya wiki kadhaa za hali ya wasi wasi kuhusiana na matatizo ya upatikanaji wa fedha kwa Ugiriki , hisia za baada ya ...
KIONGOZI mashuhuri wa Singapore, anayejulikama kama baba wa taifa hilo , Lee Kuan Yew amefariki dunia. Serikali ya nchi hiyo imetangaza hii leo kwamba Lee mwenye umri wa miaka 91 alilazwa hospitalini mapema Februari akiwa anaugua ugonjwa wa kichomi, na amekuwa akipumua kwa kutumia mashine katika kitengo cha wagonjwa mahututi tangu wakati huo. Rais wa Marekani Barack Obama ametuma salamu zake za rambi rambi na kumuelezea Lee kuwa mtu aliyeona ...
KATIKA kuadhimisha siku ya hali ya hewa duniani, Mamlaka ya hali ya hewa nchini-TMA imeanzisha mfumo ambao utawawezesha marubani wote kupata taarifa mbalimbali za safari za anga kwa njia ya mtandao ambapo kila shirika la ndege limepewa namba ya siri ya kuingia kwenye mfumo huo. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Meneja Masoko na Mahusiano kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa HELLEN MSEMO amesema kuwa kwa kufanya hivyo mamlaka imeweza kutekeleza mpango ujulikanao kama Quality Management...
SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha imewasilisha Muswada wa sheria ya mfumo wa malipo ya Taifa ya mwaka 2015 wenye lengo la kuzuia, kuimarisha na kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza katika mfumo wa malipo uliopo. Akiwasilisha rasmi muswada huo leo Bungeni mjini Dodoma waziri wa Fedha mheshimiwa SAADA MKUYA amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuiweka nchi katika mazingira ya ushindani wa kibiashara na kutengeneza ufanisi mkubwa wa malipo. Mbali na hayo waziri MKUYA ameeleza kuwa katika kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa...
Wazazi huko india wameparamia ukuta kupitisha majibu ya mitihani kwa watoto wao Watoto katika shule ya Bihar wilaya ya Hajipur wamekuwa wakipata msaada wa kupitishiwa majibu na wazazi wanapokuwa kwenye vyumba vya mitihani. Kwenye mkanda wa video uliorekodiwa na chanzo kimoja cha habari za ndani nchini humo kinaonyesha umati wa wazazi wakiparamia kuta za ghorofa kuwapitishia wanafunzi majibu ya mtihani kwa kutumia madirisha ya jengo hilo Zaidi ya wanafunzi milioni 1.4 wapo katika mitihani ambayo inarajiwa kumalizika march 24 nchini...
MASHIRIKA ya utoaji misaada yanaonya hali bado ni tete, mwaka mmoja tangu ugonjwa wa maradhi ya Ebola kulipuka Magharibi mwa Afrika. Shirika la Madaktari wasiokuwa na Mipaka- MSF, limesema kuwa mlipuko huo ambao umewauwa zaidi ya watu Elfu Kumi. Shirika limesema namna Mashirika ya Matibabu na watoaji Misaada ya Dharura, yanavyoendesha shughuli za kuwaokoa watu kuwa ni taratibu mno....
UKOSEFU wa Damu katika hospital mbalimbali nchini unaweza kusababisha madhara makubwa,ikiwemo vifo vya Kinamama na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Hayo yamesema na Shirika lisilo la kiresikali linalojishughulisha na masuala ya Afya la SIKIKA katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea madhara yanayoweza kutokea kutokana na upungufu wa damu. Mkurugenzi wa SIKIKA IRENE KIWIA,amesema kuwa upungufu wa damu uliotangazwa na Mpango wa taifa wa damu salamu-NBTS,unapaswa kushughulikiwa ipavyo ili kuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa kinamama...
WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali,wamemchagua Mbunge wa Viti Maalum,AMINA MWIDAU kupitia CUF,kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Katika Uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma,Mheshimiwa MWIDAU amechaguliwa na Wajumbe wa PAC kwa kupata kura 15 dhidi ya mpinzani wake ,LUCY OWENYA kupitia CHADEMA aliyeambulia kura mbili. Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo,MWIDAU amesema atafanya kazi iliyoachwa na KABWE ZITTO wakati akiiongoza Kamati hiyo kwa kuzingatia maslahi ya nchi na siyo watu binafsi....