Hatuwezi kumzuia Ngasa kuiaga Yanga kama atapata timu nje na Tanzania pia ni heri na faraja kwetu kwani lengo ni kukuza mpira wa nyumbani kwa kuona wachezaji wanafika mbali kupitia Yanga Kama ataona amepata nafasi ya kusonga mbele sisi hatuna kipingamizi kwani mpira ni biashara Hayo yamesemwa na afisa habari wa klabu ya Yanga Jerry Mulo alipohojiwa kupitia kipindi cha Sport Headquarters Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu wa ligi na tayari tumeanza mazungumzo nae ila hatutamlazimisha kubaki Yanga...
Atletico Madrid imetinga robo fainali za michuano ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Bayer Leverkusen kwa mikwaju ya penati. Klabu hiyo ya nchini Hispania ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Bayer Leverkusen kutokea Ujerumani. Hatua hiyo ya kutembezeana mikwaju ya penati ilikuja baada ya dakika 120 za mchezo huo kumalizika huku wenyeji Atletico Madrid wakiwa mbele kwa goli moja Goli hilo moja lilishindwa kuifanya klabu hiyo kuibuka na ushindi kutokana na matokeo ya mchezo wa awali ambapo Leverkusen iliitandika Atletico...
Arsenal imeshindwa kuifikia hatua ya robo fainali ya michuano ya Mabingwa huko barani Ulaya richa ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini katika mchezo wao wa jana usiku. Klabu hiyo ya washika bunduki jana imeshindwa kusonga mbele kutokana na kosa la kuruhusu magoli mengi wakiwa nyumbani pale walipopokea kichapo cha 3-1 dhidi ya Monaco. Kwa matokeo hayo klabu hiyo itaikosa hatua hiyo muhimu ya robo fainali ikiwa ni mara ya tano mfululizo Goli la kwanza la Arsenal lilitiwa...
KIONGOZI Mkuu wa familia ya kifalme nchini Saudia ameonya kwamba makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran huenda yakasababisha nchi zingine katika eneo hilo la ghuba kuanza kurutubisha madini ya atomiki. Mwanamfalme Turki al-Faisal amesema kwamba Saudi Arabia pia itatafuta haki sawa kama yatakavyofanya mataifa mengine. Mataifa sita yenye nguvu duniani yanayojadiliana na Iran yanadai kwamba inatosha kudhibiti shughuli za nyuklia za Iran ili isiweze kuunda silaha za...
WANAWAKE na watoto wachanga zaidi ya 45 wameuawa katika shambulizi lililotekelezwa katika kijiji kimoja huko Egba katika jimbo la Benue Nigeria. Maafisa wa usalama katika jimbo hilo la kati wanasema kuwa wavamizi walishambulia kijiji hicho alfajiri kuamkia leo . Hata hivyo,mwanasiasa mmoja kutoka eneo hilo Audu Sule ameiambia BBC kuwa zaidi ya watu 81wamauawa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki aina ya...
KATIKA kusheherekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kituo hiki cha Efm – 93.7, tarehe 2/4/2014 , imeelezwa kuwa zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wasikilizaji wa Radio hii ambayo imejipatia umaarufu mkubwa Katika kipindi cha muda mfupi, ikiwa ni sehemu ya kutoa shukrani kwa wasikilizaji wake. Akizungumza na wandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Mawasiliano wa Efm, Denis Ssebo, amesema Sherehe hizo ambazo zimepewa kauli mbiu ya Twende sawa zitachukua takribani miezi miwili na zitakuwa na matukio mengi ...
WANANCHI wametakiwa kujitokeza na kujiunga na mifuko ya jamii ya uwekezaji wa pamoja ya UTT AMIS ili kunufaika na faida mbalimbali za uwekezaji zinazotokana na kuongezeka kwa thamani ya vipande kufuatia kukua kwa mifuko hiyo ya uwekezaji kwa asilimia 25 kutoka bilioni 179 na kufikia bilioni 227 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita . Akisoma ripoti ya mifuko hiyo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Afisa mwendeshaji mkuu wa UTT AMIS Simon Migangala amesema hayo ni...
Unaweza kusikiliza vibonzo hivi pia kupitia vipindi vyetu vya michezo ambavyo ni Sport Headquarters na E...
Miezi michache tu tangu mkali kutoka Uganda Cindy na mpenzi wake Ken Muyisa waanze kuwekeza kwenye biashara ya bar sasa hiki ndicho kinachofuata kutoka kwa msanii huyu. Cindy ametangaza kuanzisha biashara mpya ya ubunifu wa mavazi na mitindo, akiongea kwenye moja ya interview yake hivi karibuni anampango wa kufungua kampuni hiyo hivi karibuni na kwa sasa ameanza kusambaza T-shirt, kofia nk. Pia ametangaza jina litakalosimama kama label ambalo ni CS herufi zilizotoka kwenye jina lake Cindy...
ZAIDI ya Watu Milioni moja kutoka nchini Brazil wameandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo DILMA ROUSSEFF, huku wengi wao wakitaka Rais huyo afunguliwe Mashtaka ya Ufisadi uliofanyika katika Shirika la Mafuta La serikali, Petrobras. Maandamano kama hayo yamefanyika katika miji mingi ya Brazil ikiwemo Mji Mkuu wa nchi hiyo Brasilia. Maandamano makubwa kabisa yamefanyika katika mji wa Sao Paulo ambalo ni eneo la upinzani waliokuwa wakipita mitaani. ...
TATIZO la Uhaba wa damu nchini limeendelea kuwa tishio kwa wagonjwa wanaohitaji damu kwenye vituo vya huduma nchini na kubababisha maisha yao kuwa hatarini. Takwimu zinaonyesha mahitaji ya Damu kwa mwaka ni Chupa 450,000 lakini makusanyo kwa mwaka ni Chupa 150,000,hali inayosababisha baadhi ya wagonjwa wanaohitaji damu kukosa huduma hiyo. Kutokana nma Hali hiyo,Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Kupitia Mpango wa Damu Salama,Inaendesha Kampeni ya Uchangiaji damu Katika mikoa...