WAKATI Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kuanza Machi 17 mwaka,Taasisi za ukusanyaji fedha nchini zikiwemo Halmashauri zimetakiwa kutekeleza wajibu wake, ili kuwezesha lengo la Bajeti kufikiwa badala ya kutegemea fedha kutoka Hazina pekee. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha MWIGULU NCHEMBA wakati akizungumza na EFM kuhusu changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa Bajeti, ambapo amesema Halmashauri zikiwajibika ipasavyo kukusanya fedha na Wizara zenye wajibu wa kukusanya Maduhuli zikitekeleza kazi...
POLISI Mkoani Dodoma wanawashikilia Wahamiaji Haram 64 Raia wa Ethiopia, huku mmoja wao akiwa amefariki. Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amenukuliwa akisema wanamshikilia Dereva wa gari lililokuwa limewabeba watu hao ambao inaaminika walikuwa njiani kuelekea Kusini mwa Afrika. Hii si mara ya kwanza kwa wahamiaji wa aina hiyo kukamatwa katika mazingira...
Kundi la muziki kutoka Kenya Elani, waliofanya vizuri na nyimbo kama kookoo na nyingine kibao zilizowatambulisha kwenye ramani ya muziki Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Wasanii hao kwa sasa wapo mbioni kufanya wimbo wa pamoja na mkali kutoka Afrika kusini Yvonne Chaka Chaka ambapo taarifa hizo zimethibitishwa na Chaka Chaka mwenyewe wakati akitumbuiza kwenye moja ya...
IDADI ya watu waliofariki kutokana na maradhi ya Ebola katika nchi tatu za Afrika magharibi zilizoathirika zaidi na maradhi yao, Guinea, Sierra Leone na Liberia imezidi watu 10,000. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya la Umoja wa mataifa WHO iliyochapishwa mjini Geneva. Hata hivyo shirika hilo limesema maradhi hayo yamepungua hivi sasa na kuna matukio machache mapya ya Ebola yaliyosajiliwa....
WIZARA ya ulinzi nchini Korea Kusini inasema kuwa Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa marefu kwenda baharini eneo la pwani ya mashariki. Tukio hilo limeripotiwa wakati kukiwa na msukosuko katika rasi hiyo huku korea kusini na marekani wakiendelea na mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka. Korea na marekani wanasema kuwa mazoezi hayo ni ya kujilinda lakini korea kaskazini inayaona kuwa ya kutaka...
WIZARA ya maji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni imefanya Operesheni ya kukamata wezi wanaoiba Miundo mbinu ya maji ili kuondoa kero ya upatikanaji wa maji katika sehemu mbalimbali jijini dar es salaam. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, PAUL MAKONDA amesema kuwa, katika oparesheni hiyoWilaya ya Kinondoni ni mojawapo ya wilaya ya Mkoa wa Dar es salaam zilizohujumiwa na kuwa na wizi mkubwa wa maji katika miundo...
BASI la Arusha Express limepata ajali leo maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kisongo jijini Arusha wakati likijaribu kulipita gari ligine na kukutana na lori mbele yake. Imeelezwa kuwa ili kuepusha madhara, dereva wa lori aliamua kuingia kichakani ili asigongane uso kwa uso na basi hilo. Katika ajali hiyo, hakuna aliyepoteza maisha isipokuwa watu ndani ya lori ndiyo wamejeruhiwa na kukimbizwa...
Picha juu ni wanafunzi kutoka Dar es salaam City College waliobahatika kutembelea kituo chetu katika idara ya habari na kupata nafasi ya kujifunza taratibu zinazotumika kuandaa habri wakiongozwa na mhariri mkuu wa efm Scolastica Mazula. Picha juu ni wanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya sekondari ya Zanaki walipobahatika kutembelea studio zetu na kukutana na baadhi ya watangazaji...
KATIKA mapigano makubwa na makali yanaondelea dhidi ya wanamgombo wa Islamic State, majeshi ya Iraq na yale Shia yamezidi kupata ushindi na kuurudisha tena mji wa Tikrit. Majeshi ya nchi hiyo yamesema imewachukua usiku mzima kupambana katika eneo la kaskazini, mashariki na magharibi kando ya mji, kuingian katikati mwa mji. Kwa mujibu wa ripoti moja, kwa sasa wapiganaji mia moja na hamsini wa kundi la Islamic State wameendelea kuwepo katika mji huo wa Tikrit, ambao ni makao makuu ya jimbo...
NAIBU Gavana wa Bank Kuu-BOT, JUMA RELI na baadhi ya maofisa Waandamizi wa Bank hiyo wametimuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali-PAC. Hatua hiyo ya kufukuzwa imekuja baada ya kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu uwepo wa Watanzania ambao wanatajwa kuwa wamefungua Akaunti nje ya nchi wakati sheria inakataza. Akizungumzia uamuzi huo jijini Dar es salaamMwenyekiti wa PAC Mheshimiwa KABWE ZITTO amesema kimsingi BOT wanaonekana kutojiandaa kuhusiana na Sakata hilo hivyo ni vema waende kujipanga...
SAKATA la kushambuliwa kwa aliyekuwa Mlinzi wa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dokta WILBROAD SLAA ,KHALID KAGENZI ,limechukua sura mpya baada ya kiongozi huyo kufika Katika kituo Kikuu Cha Polisi na kuandika maelezo takribani saa Tano. Hivi karibuni Dokta SLAA kupitia kwa mmoja wa Viongozi wa CHADEMA,MABERE MARANDO, alidai kuwepo kwa mpango wa kumdhuru ambao unaratibiwa na Maofisa wa Usalama kwa kushirikiana na baadhi ya Viongozi wa CCM. Mpango huo ulidaiwa kuwa ungetekelezwa kupitia kwa KAGENZI, ambaye baadaye aliteswa na kushambuliwa na...