Slider

DANNY WELBECK AIONDOA MAN U KOMBE LA FA
Slider

Danny Welbeck amerejea katika viwanja vya old Trafford kwenye mechi iliyochezwa jana ambapo timu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa 2-1 baada ya kuichapa Manchester united kwenye uwanja wa nyumbani Mshambuliaji wa Uingereza Welbeck aliejiunga na klabu ya Arsenal akitokea Man u alishinda goli lililoipa Arsenal ushindi wao wa kwanza katika viwanja hivyo tangu mwaka 2006 Goli la kwanza la Arsenal lilifungwa na Nacho Monreal katika kipindi cha kwanza cha mchezo huolakini baadae Wayne Rooney alisawazisha bao hilo Goli hilo...

Like
260
0
Tuesday, 10 March 2015
BURUNDI: ALIEKUWA MWENYEKITI WA CNDD-FDD AMTUHUMU RAIS KUPANGA NJAMA ZA KUMFUNGA JELA
Global News

ALIYEKUWA mwenyekiti wa chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD Hussein Rajabu aliyekuwa ameripotiwa kutoroka jela amemlaumu rais Pierre Nkurunziza kwa kumpangia njama ya kumfunga jela ili kutokomeza demokrasia nchini humo. Akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC, Bwana Rajabu amesema kuwa yeye yuko salama na wala hakutoroka jela kama ilivyodhaniwa bali alitoka jela rasmi baada ya kushirikiana na wafuasi wa chama chake. Rajabu amesema kuwa wazalendo wenzake wa CNDD-FDD ndio walifanikisha kuondoka kwake gerezani kwa ”heshima....

Like
258
0
Monday, 09 March 2015
WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI TOFAUTI KWENYE UCHAGUZI
Local News

WANAWAKE nchini wamehimizwa  kuachana na malumbano na badala yake wameshauriwa kuondoa hofu  na kujitokeza kwa wingi  kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa ndani na nje ya chama katika ngazi za mikoa na Taifa lakini pia wajitokeze kuomba nafasi ambazo  zitawaniwa  kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu . Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam  na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mabadiliko na Uwazi-ACT, MOHAMED MASSAGA kwenye sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa jana Machi 8....

Like
220
0
Monday, 09 March 2015
UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI KUANZA KUTOA MAFUNZO KWA JESHI LA POLISI NA MAHAKAMA
Local News

UBALOZI wa Uingereza nchini leo umekutana na wadau mbalimbali ikiwemo Jeshi polisi na Mahakama kwa lengo la kutoa mafunzo yatakayowasaidia katika utendaji kazi wao wa kila siku kwa manufaa ya Taifa. Akizungumza wakati wa utoaji mafunzo hayo leo jijini Dar es salaam mshauri mkuu wa masuala ya kimahakama kutoka Ubalozi huo LINDSEY MCNALLY amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yatasaidia kutatua kwa haraka kesi nyingi za kimahakama zinazochukua muda mrefu....

Like
357
0
Monday, 09 March 2015
MAKONGORO NYERERE AKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA MAMA YAKE
Local News

MTOTO wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere, amekanusha taarifa zilizotambaa Katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa Mjane, Mama Maria Nyerere amefariki dunia. Akizungumza na Efm kwa njia ya simu kutoka nchini Uganda, Mheshimiwa Makongoro amesema familia imesikitishwa na mtu aliyevumisha taarifa hizo, nakwamba mama yao ni mzima. Hata hivyo amewataka Watanzania, kuacha tabia ya kuvumisha taarifa ambazo siyo za kweli kwani zinachangia upotoshaji kwa watu na badala yake kuwa na ufuatiliaji wa mambo kabla hawajaanza...

Like
433
0
Monday, 09 March 2015
PICHA: UJAUZITO SI KIKWAZO KWA TIWA SAVAGE AFANYA BONGE LA SHOW UGANDA
Entertanment

Tiwa Savage  richa ya kuwa sasa anaujauzito upatao miezi tena ila kwake haikuwa kikwazo kutua nchini Uganda na kuafanya bonge la show kwenye Airtel Inspiring Women Concert na kushiriki pia kwenye tuzo za mitandao ya kijamii nchini humo  ikiwa ni masaa machache baada ya kupokelewa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa nchini humo siku ya jumamosi. Mwimbaji huyo kutoka kwenye kundi la The Marvin hakuwepo katika show ya AMVCA iliyofanyika huko kwao Nigeria amapo mastar kadhaa wa Afrika walihusika jukwaaniakiwemo Diamond...

Like
471
0
Monday, 09 March 2015
JARIBIO LA KWANZA LA NDEGE INAYOTUMIA UMEME WA JUA LIMEFANYIKA LEO
Global News

Ndege hiyo iliruka majira ya saa 12 saa za Afrika Mashiriki ikianzia Abu Dhabi. Ndege hiyo yenye kiti kimoja ina mabawa yenye ukubwa wa jumbo jet huku ndege yenyewe ikiwa na uzito sawa na gari, mabawa yake yamefunikwa na vifaa vya vya kunasia mionzi ya jua yaani solar panels. Betri zake zina uwezo wa kuhifadhi nguvu ya umeme jua kutoka kwenye jua na hivyo kuiweza kusafiri hata nyakati za usiku. Marubani wawili wanaorusha ndege hiyo Bertrand Piccard na Andre Borschberg...

Like
243
0
Monday, 09 March 2015
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI AKEMEA WAZAZI WANAOKATISHA WATOTO MASOMO
Local News

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa ANNE KILANGO MALECELA, amekemea Wazazi wilayani Bagamoyo ambao wanakatisha watoto wao masomo, kwa kisingizio cha kukosa Ada, na badala yake hutumia gharama kubwa kuwafanyia watoto Ngoma za Kimila. Aidha amekemea Familia zinazoombea watoto wao wafeli katika Mitihani yao, ili kuepuka gharama za kusomesha. Mheshimiwa KILANGO ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wazazi, walezi, walimu, wanafunzi, wananchi na Viongozi mbalimbali katika mafahali ya saba ya kidato cha sita katika shule ya...

Like
277
0
Monday, 09 March 2015
BALOZI SEIF ALI IDD ALIA NA VIONGOZI WANAOKWAMISHA KURA YA MAONI KUWA NI KINYUME NA DEMOKRASIA
Local News

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi SEIF ALI IDD, amesema  Viongozi wa kisiasa wanaowakataza wananchi wasishiriki zoezi la kura ya maoni mwezi Aprili mwaka huu ili kuipitisha Katiba inayopendekezwa, wana alama za Udikteta na pia wanakwenda kinyume na matakwa ya Demokrasia. Balozi SEIF ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na kusema jambo hilo ni fedheha katika dunia mpya inayooongozwa kwa kufuata misingi ya Demokrasia na utawala bora. Ameeleza kwamba...

Like
293
0
Monday, 09 March 2015
KOCHA WA ZAMANI WA YANGA, MICHO AJIUNGA NA AL HILAL YA SUDANI
Slider

Kocha wa zamani wa Yanga, Micho ajiunga na klabu ya Al Hilal ya Sudani na kuitosa timu ya Taifa ya Uganda Timu hiyo ya sudani imemtangaza mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic kama kocha mkuu w timu hiyo baada ya kikao cha bodi siku ya jumamosi Al Hilal imemaliza mkataba wake na kocha aliekuwa akikinoa kikosi hicho Patrick Osimes mwezi uliopita. “Bodi imekutana jumamosi katika makao makuu ya klabu huko Omdurman na kufikia maamuzi mengi ikiwemo kumchagua Micho kuwa kocha mkuu” ilitangaza...

Like
509
0
Monday, 09 March 2015
JUHUDI ZA KUTATUA MZOZO SUDANI KUSINI ZAGONGA MWAMBA
Global News

MAZUNGUMZO ya kutatua mzozo unaokumba Sudan Kusini yamegonga mwamba, saa kadhaa kabla ya Umoja wa Mataifa kuwawekea vikwazo wanaohusika. Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir na mpinzani wake ambaye aliwahi kuwa makamu wake, Riek Machar, wamekuwa wakijadili mipango ya kugawanya mamlaka ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha maelfu ya watu kuuawa na zaidi ya watu milioni moja na nusu kupoteza makazi. Umoja wa mataifa umetishia kuwawekea vikwazo watu binafasi wanaojaribu kuzuia makubaliano hayo iwapo makundi hayo mawili...

Like
270
0
Thursday, 05 March 2015