Arsene Wenger amemmwagia sifa za kutosha Olivier Giroud’s kuwa na uwezo mkubwa kiakili na kusisitiza kuwa hakudhamiria kumpumzisha mshambuliaji huyo Giroud amekuwa benchi baada ya kukosa nafasi kadhaa za kushinda magoli kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na kupokea kichapo cha 3-1 walipokutana na Monaco. Meneja huyo wa Arsenal bado anaimani ya kutosha kwa mshambuliaji huyo kufuatia ushindi wa magoli ya 2-0 dhidi ya Everton kwenye uwanja wao wa nyumbani huko Emirates ambapo Giroud kuziona nyavu na kuandika goli...
WAZIRI Mkuu wa Israeli BENJAMIN NETANYAHU amewasili nchini Marekani kupinga dhidi uwezekano wa kufikia makubalino na Iran juu ya mpango wake wa Nyuklia. Bwana NETANYAHU amesema mkataba huo hautoshi kuizuia Iran kumiliki Silaha za Nyuklia. Pia anatarajia kulihutubia Bunge la Congress March 03, hotuba ambayo haikukubaliwa kabla na Utawala wa Rais BARRACK OBAMA na kuiudhi Ikulu ya...
MAKAMU wa Rais wa Sierra Leone SAMUEL SAM-SUMANA amejiweka mwenyewe katika Karantini kwa siku 21 baada ya mlinzi wake mmoja kufa Jumanne iliyopita kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola. SAM-SUMANA anakaimu wadhifa wa Urais baada ya rais Wa nchi hiyo ERNEST KOROMA kuondoka Sierra Leone kwenda Ubelgiji kuhudhuria mkutano kuhusu Ebola utakaofanyika March. SAM-SUMANA anatekeleza majukumu yake kutoka nyumbani kwake na ni Kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu wa Afrika kuwa katika Karantini tangu Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola...
MKUU wa Polisi Wilaya ya Arusha Mrakibu wa Polisi -SP JUMANNE MULIRO amevitaka vikundi vya ulinzi shirikishi pindi wanapokuwa katika kazi za doria kutowabughudhi wananchi badala yake wanatakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria. Amesema utendaji bora wa kazi kwa kuzingatia nidhamu na sheria utaongeza imani kwa wananchi hali ambayo itawafanya wajitolee na kuendelea kuvichangia vikundi hivyo hatimaye kuboresha maslahi yao wenyewe na vikundi hivyo kwa ujumla Hayo yamesemwa wakati wa Uzinduzi wa vikundi viwili vya Ulinzi Shirikishi uliofanyika...
WAKATI Tanzania inatarajia kuingia katika zoezi muhimu la Uchaguzi mkuu wa Udiwani, Ubunge na Urais Oktoba mwaka huu, Wito umetolewa kwa waandishi wa habari kutojihusisha na upande wowote wa Vyama vya Kisiasa na badala yake wafuate maadili ya kazi kwa maslahi ya Taifa. Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama Cha –ADC SAID MIRAJI wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema kuwa Uandishi wa Habari ni Taaluma inayopaswa kutumika bila kuegemea upande wowote. Ameeleza kuwa...
MAHAKAMA moja ya jijini New York, Marekani imemhukumu Khalid al-Fawwaz kwa kuhusika na mashambulizi ya mabomu ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998. Waendesha mashtaka wamemtaja al-Fawwaz kuwa mmoja wa watu waliokuwa karibu zaidi na aliyekuwa kiongozi wa al-Qaida, Osama bin Laden. Baada ya mahakama kumkuta na hatia katika makosa 29, al-Fawwaz mwenye miaka 52 sasa anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha. Raia huyo wa Saudi Arabia alikamatwa jijini London, Uingereza, mwaka 1998 na kukabidhiwa kwa Marekani mwaka...
Maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati waliokimbilia Jamhuri ya Kidmekorasia ya Congo sasa wanakumbwa na balaa la njaa. Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, limesema wakimbizi hao walioko kaskazini mashariki mwa Congo wanakabiliwa na utapiamlo kwani hawapati chakula na maji ya kutosha na wanategemea tu wahisani kuwapatia mahitaji ya msingi. Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, MSF imeshuhudia watoto kumi wakilazwa hospitalini kutokana na utapiamlo....
JUKWAA la sera na mtandao wa asasi za kiraia unaoshughulikia maswala ya utawala bora na uwajibikaji, umeandaa mjadala uliojadili na kuangazia namna uchimbaji wa madini unaofanywa na makampuni na kuangalia jinsi wanavyowajibika kwa jamii, kwa wafanyakazi wanao waajiri na jinsi wanavyotunza mazingira ili kuandaa mazingira bora na kuleta maendeleo endelevu. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mratibu wa jukwaa la sera Senkaye Kilonzo amesema kama asasi za kiraia zinazoangalia maswala hayo wameona kuna haja ya kukaa...
MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake Tanzania-WAMA amekabidhi msaada wa mashine ya kisasa ya upimaji Saratani ya Matiti kwa akinamama katika hospitali kuu ya Jeshi la Ulinzi Tanzania LUGALO ili kuokoa maisha ya wanawake wengi wanaosumbuliwa na Saratani ya matiti nchini. Akizungumza na wadau mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam kwenye makabidhiano ya mashine hiyo Mama SALMA KIKWETE ambaye pia ni mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza kuwa mashine imetolewa na kikundi cha wanawake watanzania waishio Marekani kijulikanacho kama Tano...
Justin Bieber ahamia kwenye mjengo mpya wenye hadhi ya kipekee huko Beverly Hills Calfonia Wadadisi wa mambo huko marekani wanaitaja hatua hiyo ya msanii huyo kuwa ni kama ni sehemu ya kupunguza gharama za maisha kwa kulinganisha kodi ya mwezi aliyokuwa akilipa kwenye kasri ya glass palace ambapo kwa mwezi alikuwa akilipa dola za kimarekani $60,000 ila kwa huu mjengo wa sasa analipia $35,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na punguzo la nusu ya gharama kw kulinganisha na kodi ya...
KATIBU MKUU wa NATO Jens Stoltenberg ameonya kwamba jaribio lolote la kupanua mipaka inayoshikiliwa na wapiganaji wanaotaka kujitenga nchini Ukraine , halitakubalika na kuiambia Urusi kuondoa vifaa 1,000 vya kijeshi kutoka katika ardhi ya nchi jirani ya Ukraine. Akizungumza baada ya mkutano na waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi , katibu mkuu wa NATO ameeleza matumaini ya tahadhari juu ya matarajio ya makubaliano tete ya kusitisha mapigano kati ...