Kama ukipata nafasi ya kukutana na kikundi cha mashabiki au wanamichezo duniani kote jaribu kuwauliza je ni mchezo gani unamashabiki wengi zaidi bilashaka watakujibu kuwa ni soka, Mpiganaji maarufu duniani Michael Gerard Tyson yeye kwa upande wake aliulizwa na mmoja wa watangazaji wa kipindi cha michezo huko nchini marekani je unafikiri nimchezo gani mgumu zaidi kucheza kupita michezo yote? akajibu mpira wa miguu ni mchezo mgumu kuliko michezo yote. Kwa upande wake mpiganaji maarufu duniani kwa sasa na nishabiki wa...
BARAZA la Seneti nchini DRC limepiga kura kufanyia marekebisho mswada uliopendekeza sheria za uchaguzi kufanyiwa mabadiliko. Mswada huo ndio uliozua vurugu na ghasia katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kwa wiki moja. Mabadiliko hayo sasa yanafuta kipengee ambacho kingechelewesha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao. ...
CHANJO ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola iko njiani kuelekea nchini Liberia. Hii ni mara ya kwanza kwa chanjo hii kupelekwa kwenye nchi iliyoathiriwa zaidi na Ebola. Lakini Wataalamu wanasema, wakati huu maambukizi ya Ebola yakiwa yanapungua, itakuwa vigumu kubaini kama chanjo hii inatoa kinga dhidi ya Virusi vya ugonjwa huo. Chanjo hiyo ilitengenezwa na Kampuni moja ya Uingereza, na Taasisi ya kitaifa ya afya nchini Marekani GSK imesema ndege iliyo iliyobeba dozi za awali takriban 300 za chanjo...
KATIKA kuhakikisha kuwa kunakuwepo na Ubora na Usalama wa dawa kwa matumizi ya binadamu, Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini-TFDA, imefuta usajili na kuzuia uingizaji, usambazaji na matumizi ya aina tano za dawa za binadamu. Akizungumza na Wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo HIITI SILLO, amesema kuwa uamzi huo uliochukuliwa ni kutokana na matokeo ya mfumo wa ufuatiliaji na kubaini uwepo wa dawa duni kwenye soko. Bwana SILLO amezitaja baadhi ya dawa zilizofungiwa...
UMOJA wa katiba ya wananchi -UKAWA, umesema kuwa hawatashiriki katika mchakato wa kura za maoni kutokana na mapungufu mbalimbali yanayolikabili zoezi hilo ikiwemo mchakato wa kupata katiba pendekezwa haukuzingatia maridhiano ya kitaifa. Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa umoja huo ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha wananchi Cuf Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa kutokana na mapungufu hayo Ukawa walisusia mchakato huo tangu ulipoanza na pia Rais alipuuza makubakubaliano baina ya umoja wa Demokrasia Tanzania ambao unaundwa na vyama...
MATOKEO ya kura za urais nchini Zambia sasa yameanza kukamilika katika ukumbi wa kimataifa wa Mulungushi makao makuu ya kuhesabia kura . Matokeo yaliotolewa na tume ya uchaguzi ya Zambia Usiku wa kuamkia leo yanaonyesha kuwa Edgar Lungu mgombea wa chama tawala cha Patriotic Front mpaka sasa bado anaongoza akiwa na kura laki 670 elfu 397 huku mpinzani wake Hakainde Hachilema wa chama cha United Party for National Development akiwa karibu kwa kura laki 641 efu 343. Hivo Edgar Lungu...
SERIKALI imesema imeandaa mkakati maalumu wa kuwaelimisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura. Mkakati huo utatekelezwa kupitia Halmashauri zote nchini na kwamba, itakuwa ni fulsa kwa wananchi kuona umuhimu wa kupiga kura. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Tamisemi, mheshimiwa Hawa ghasia, wakati akizungumza kwenye kikao cha sita cha shirikisho kati ya Tanzania bara na Zanzibar kinachofanyika mjini Morogoro....
KUFUATIA utafiti uliofanywa na Hakielimu na kutoa Takwimu zinazoonesha kushuka kwa Elimu kwenye baadhi ya Mikoa nchini ikiwemo Mkoa wa Rukwa Kantalamba jimbo la Nkasi ambapo hali ya utekelezaji wa malengo ya Matokeo Makubwa Sasa si ya kuridhisha bado Sekta ya Elimu imeonesha kuwa na changamoto kubwa mkoani humo. Akizungumza na Efm mara baada ya utafiti huo kutolewa mbunge wa jimbo la Nkasi Mheshimiwa Ally Kessy amesema siyo kweli kwamba elimu haijafanikiwa kwenye jimbo hilo kwakuwa Shule zimekuwa nyingi na...
KUNA TAARIFA kuwa mfalme wa Saudia Abdullah bin Abdulaziz amefariki dunia akiwa hospitalini . Tamko la kifo cha mfalme huyo zimetolewa na kaka wa mfalme huyo aitwaye , Salman,ambaye naye aliwahi kuwa mfalme. Kabla ya tamko hilo television ya taifa la Saudia ilikatiza matangazo yake na kuweka nyimbo za quraan ,kama ishara ya kifo cha kiongozi wa juu wa ufalme. Mfalme Abdullah, amefariki dunia akiwa na miaka 90, alilazwa hospitalini kwa wiki kadhaa tangu December mwaka wa jana kutokana na...
TETESI ZA MAGAZETI: Klabu ya Manchester United imeweka mezani kitita cha paundi milioni 61 ili kumsajili kiungo wa klabu ya Juventus PAUL POGBA huku Chelsea nayo ikionekana kumuhitaji mchezaji huyo. (Daily Express) Klabu ya Valencia na Liverpool zimeingia katika kinyanganyiro cha kuisaka saini ya kiungo wa Manchester City JAMES MILNER. (Sky Sports) Klabu ya Arsenal na Manchester United zipo katika kinyanganyiro cha kuisaka saini ya beki wa kati wa klabu ya Villarreal GABRIEL PAULISTA kwa paundi milioni 16. (Daily Mail)...
MAREKANI na Cuba zimeanza mazungumzo ya kihistoria leo kuhusu kurejesha mahusiano ya kidiplomasia baada ya kikao kilichojadili masuala ya uhamiaji kudhihirisha changamoto zilizopo katika kuondokana na uhasama wa nusu karne kati ya nchi hizo. Ujumbe wa ngazi ya juu wa Marekani kuwahi kwenda Cuba katika kipindi cha miaka 35 utakamilisha mazungumzo ya siku mbili leo mjini Havana, huku pande zote mbili zikionya hakuna uwezekano wa kufikia makubaliano ya haraka. Maafisa wa Marekani wanasema wana matumaini Cuba itakubali kuzifungua balozi zake...