RAIS wa Haiti na Wabunge wa Upinzani wanaendelea na mazungumzo, kujaribu kufikia makubaliano ya dakika za mwisho, kutatua mgogoro unaokwamisha uchaguzi katika taifa hilo linalokabiliwa na matatizo. Rais MICHEL MARTELLY na Maafisa wa upinzani wamekuwa katika mvutano kuhusu uchaguzi wa Bunge uliopaswa kuitishwa mwaka...
MKUU wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara FARIDA MGOMI, ametoa onyo kwa viongozi wa vijiji vya Mwongozo, Mdenga na Nangoo vilivyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi, ambao wanashindwa kuwachukulia hatua za kisheria watu ambao wanahujumu miundombinu katika mradi wa maji wa mamlaka ya maji safi na Mazingira Masasi-Nachingwea -MANAWASA. MGOMI ametoa onyo hilo baada ya Mamlaka hiyo kutangaza kusudio la kusitisha huduma ya Maji kwenye Vijiji hivyo vitatu kutokana na wananchi wake kuhujumu Miundombinu ya maji na kusababisha huduma...
IKULU imesema Rais JAKAYA KIKWETE, hajapiga marufuku, wala kupinga au kusema vifaa vya kupigia kura kwa kutumia mfumo wa kisasa wa –BVR-, havifai kwa matumizi. Ikulu imetoa taarifa hiyo, na kufafanua kuwa katika hafla ambayo Rais aliwaandalia Mabalozi wanaowakilisha nchi na Mashirika ya Kimataifa juzi, kuna baadhi ya vyombo vya habari vilipotosha kuhusu suala...
LEO Wazanzibar wanaadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu yaliyofanyika January 12 mwaka 1964. Pamoja na hali hiyo bado Tanzania kama Taifa linaloundwa na Visiwa vya Zanzibar na Tanganyika wana kila sababu ya kujadili hali na mwenendo wa Taifa hili. Katika siku za hivi karibuni wameshuhudia matukio mabaya yanayoashiria uvunjifu wa Amani Visiwani humo na wakati mwingine hata raia wasiokuwa na hatia kupoteza maisha. ...
Ray J atoa ametoa ofa ya kununua mjengo katika mtaa anaoishi Kim kardashian na mumewe Kanye west. Ray j ambae aliwahi kuwa na mahusiano na Kim na kucheza nae filam ya Ngono hali inayopelekea mara kadhaa Ray j kutishia kuichia video hiyo inayotabiliwa kuja kuuza zaidi nahii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa Kim ni mke wa Kanye west Mwezi mmoja nyuma Kim Kardashian alichapisha picha zake za utupu kwenye moja ya majalida makubwa yanayoandika habari za mastar, wataalamu...
RAIS WA SHIRIKISHO la Jamhuri ya Ujerumani JOACHIM GAUCK amelaani shambulio la kigaidi la Paris na kulitaja kuwa ni shambulio dhidi ya uhuru. Rais GAUCK amesema Demokrasia imezidi kupata nguvu kuushinda ugaidi kabla ya mapokezi ya mwaka mpya ya mabalozi wa nchi za nje katika kasri lake mjini Berlin. Rais JOACHIM GAUCK ameendelea kusema kuwa hawataachia chuki...
Umoja wa Mataifa umekemea wimbi la mashambulizi dhidi ya Watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino, baada ya tukio la kutekwa kwa mtoto wa miaka minne mjini Mwanza. Mwakilishi wa UN nchini ALVARO RODRIGUEZ ameitaka Serikali ya Tanzania kuzidisha juhudi za kupambana na vitendo vya unyanyapaa dhidi ya...
Wajumbe wa kamati ya ufundi ya bodi ya maji Safi na Maji Taka Dar es salaam-DAWASA wamefanya ziara ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo. Ziara ya wajumbe hao wa kamati ya Ufundi imeanza kwa kukagua kazi ya ukarabati wa kituo yalipo matangi ya maji...
KAMATI KUU ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi -CCM inataraji kukutana Zanzibar Januari 13,mwaka huukatika kikao cha kawaida cha siku moja chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais JAKAYA KIKWETE. Kikao cha Kamati Kuu kitatanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kitakachofanyika Januari 10, jijini Dar es...
POLISI WA UWANJA wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere-JNIA wamefanikiwa kumkamata Raia wa Kuwait,HASSAIN AHMED ALLY kwa tuhuma za kukutwa na Viumbe aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Shilingi Milioni 6 nukta kinyume cha sheria . Kamanda wa Polisi wa Uwanjani hapo HAMISI SELEMAN amesema kuwan raia huyo amekamatwa na Kenge hao ambao amewaweka katika mifuko midogo midogo iliyokuwa kwenye begi lake kubwa. Amesema kuwa tukio hilo limetokea wakati HASSAN akijiandaa na safari ya kuelekea nchini Kuwait kupitia Dubai...
WANAMGAMBO wa kundi la Boko Haram wameripotiwa kuwauwa watu kadhaa katika mashambulio kaskazini mashariki mwa Nigeria. Nyumba pia zimechomwa katika wimbi la hivi karibuni la mashambulizi katika jimbo la Borno. Hali hiyo imekuja baada ya kundi hilo lenye Itikadi Kali ya Kiislamu kuuteka mji wa Baga mwishoni mwa Juma....