Slider

AU: YAKUTANA DAR LEO
Local News

UMOJA WA AFRICA na nchi zake 13 ikiwemo Tanzania zimekutana leo nchini kujadili mpango wa muda mfupi wa kukabiliana kwa haraka na migogoro na majanga yanayojitokeza wakati wowote Africa ACIRC.  Mpango huo wa ACIRC uliounda jeshi la Afrika la kukabiliana kwa haraka na migogoro na majanga yanayojitokeza wakati wowote kupitia zoezi la utulivu, Africa imelenga kutimiza malengo ya nchi za umoja huo kwa kupima uwezo wa kutatua matatizo yake yenyewe   ambapo kwa mwaka huu Tanzania imekuwa mwenyeji wa hafla hiyo....

Like
261
0
Thursday, 27 November 2014
MUHONGO AWASILISHA HOJA YA MKATABA KATI YA IPTL NA TANESCO
Local News

WAZIRI WA NISHATI na Madini Profesa SOSPITER MUHONGO amewasilisha hoja yenye maelezo juu ya mkataba uliowekwa kati ya kampuni ya –IPTL-na shirika la umeme nchini Tanesco ambapo amesema kuwa taarifa iliyotolewa na kamati  ya  hesabu za serikali na mashirika ya umma- PAC- haina ukweli wowote kwa kuwa fedha za –ESCROW– siyo fedha za umma. Akiwasilisha hoja hiyo leo Bungeni mjini Dodoma Profesa MUHONGO amesema kuwa ingawa kiasi hicho cha fedha za –ESCROW- siyo za umma pia hakuna ukweli wowote juu...

Like
243
0
Thursday, 27 November 2014
SHEMEJI WA DESIRE LUZINDA AHUKUMIWA KIFO
Entertanment

Kaka wa aliekuwa boyfriend wa desire luzinda Franklin ambae ni raia wa Nigeria amehukumiwa kifo nchini Malaysia baada ya kukutwa na hatia ya kuingiza dawa za kulevya nchini humo Jamaa huyo mwenye umri wa mika 35 alietambulika kwa jina la Abuchi Ngwoke alihukumiwa kifo siku ya jumanne november 25 na mahakama kuu ya Malaysia baada ya kukamatwa mapema mwaka 2012 katika uwanja wa ndege nchini humo akiwa na kilo 251.66 za methamphetamine, ingawa hukumu hiyo imepita lakini bado siku ya...

Like
364
0
Thursday, 27 November 2014
HOLLANDE RAIS WA KWANZA KUTOKA MAGHARIBI KUTEMBELEA AFRIKA MAGHARIBI
Global News

  RAIS wa Ufaransa Francois Hollande anatarajia kuanza ziara yake nchini Guinea kesho, itakayomfanya kuwa kiongozi wa kwanza wa magharibi kuitembelea nchi iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa hatari wa Ebola. Guinea tayari imewapoteza watu 1,200 kutokana na ugonjwa huo, ambao kufikia sasa umewaua zaidi ya watu 5,600 na kuwaambukiza wengine 16,000 hasa katika eneo la Afrika Magharibi, kwa mujibu wa Shirika la Afya ulimwenguni – WHO. Katika hatua nyingine Watafiti wa chanjo ya Ebola nchini Marekani wamesema kuwa wametiwa...

Like
311
0
Thursday, 27 November 2014
WAZAZI KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA ELIMU
Local News

WAZAZI nchini  wameshauriwa kuwekeza katika sekta ya  elimu  ili kuweza kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo hasa kwa  baadhi ya shule za msingi nchini. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na mtabibu wa tiba mbadala Abdalah Mandai wakati akizungumza na kituo hiki juu ya changamoto mbalimbali za sekta ya elimu nchini. Amesema kuwa baadhi ya shule za msingi zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati pamoja na vyumba vya madasara kitendo kinachochangia wanafunzi kusoma huku wakiwa wamekaa chini na...

Like
252
0
Thursday, 27 November 2014
NANYUMBU WALALAMIKA KUNYANYASWA HOSPITALI MASASI
Local News

WANANCHI wa Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wamemlalamikia Katibu Mkuu wa CCM ABDULRAHMAN KINANA kuwa wagonjwa wanaotoka wilani humo kwenda Hospital ya Wilaya ya Masasi wananyanyaswa. Wananchi hao wameiomba Serikali kutoa kibali cha kupandisha hadhi hospital ya Wilaya ya Nanyumbu ambapo Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imeombwa kibali kwa muda mrefu lakini hadi sasa imeshindwa kutoa na matokeo yake hospital ya Wilaya ya Nanyumbu imebaki kuwa Kituo cha Afya. Wananchi hao wamemwambia Ndugu KINANA kuwa ni vema akawasaidia...

Like
421
0
Thursday, 27 November 2014
PINDA: TANZANIA BILA FOLENI INAWEZEKANA
Local News

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA amesema kuwa serikali imedhamiria kuondoa tatizo la msongamano  wa magari katika miji yote mikubwa ikiwemo Dar es salaam, Mwanza na Arusha kwa kuwashirikisha wananchi pamoja na vyombo husika kupitia sheria na Taratibu zilizowekwa. Waziri PINDA ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Kilwa mheshimiwa MURTAZA MANGUNGU aliyehoji kutaka kujua mikakati ya serikali katika utekelezaji wa suala hilo nchini. Bunge linaendelea tena leo mjini Dodoma ambapo kutakuwa na Tamko la serikali juu ya...

Like
250
0
Thursday, 27 November 2014
FLOYD MAYWEATHER: KUTOA MIMBA NI MAUAJI
Entertanment

  Floyd Mayweather  amedai kuwa hakumkosea aliekuwa mpenzi wake Shantel Jackson hakumkosea kufuatia kitendo cha yeye kulizungumzia swala la Shantel Jackson kutoa mimba kupitia mitandao ya kijamii kwavile hata mahusiano yao yalikuwa ni kutafuta umaarufu kwenye jamii Mapema mwaka huu iliripotiwa kwamba Shantel Jackson amefungua kesi kwa sababu tofautitofauti ikiwa ni pamoja na kushambuliwa, kashfa, uvamizi wa faragha na zaidi. Floyd Mayweather  alifunguka zaidi na kutoa siri kuwa Shantel ndie aliemtafuta yeye na kumuomba amfanye kuwa...

Like
252
0
Thursday, 27 November 2014
PAPA FRANCIS ATAKASERA YA UHAMIAJI ULAYA
Global News

KIONGOZI  wa  Kanisa  Katoliki Papa  Francis  amelitaka bara  la  Ulaya  kutayarisha  sera  moja  na ya haki  katika suala la  uhamiaji. Amesema mamia  kwa  maelfu  ya wahamiaji  wanaowasili  katika  mataifa  hayo kila  mwaka kupitia  baharini  wanahitaji  kukubalika na  msaada, na  sio kuwa  na  sera  zenye  maslahi  binafsi  ambazo zinahatarisha  maisha na  kuchochea  mzozo  wa  kijamii. Papa Francis  ametoa  kauli hiyo  katika  bunge  la Ulaya  wakati  wa  ziara  fupi  iliyokuwa  na  lengo ...

Like
316
0
Wednesday, 26 November 2014
SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA 78 NIGERIA
Global News

WATU 78 wameuawa katika mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyofanywa sokoni, katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria. Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema mlipuko wa kwanza ulitokea wakati washambuliaji hao walipomuwekea mlipuko mwanamke mmoja mwenye matatizo ya akili. Kundi la kiislamu la wapiganaji la Boko Haram ambalo linadhibiti maeneo mengine ya miji ya kaskazini mwa nchi hiyo na vijiji, linadhaniwa kuhusika na shambulio...

Like
397
0
Wednesday, 26 November 2014
ZIMAMOTO KUANZISHA OPARESHENI YA UKAGUZI WA VIFAA
Local News

JESHI la Zimamoto na Uokoaji mkoani Pwani linatarajia kuanza Oparation maalum kwa ajili ukaguzi wa Vifaa vya kung’amua na kuzima moto kwenye shule za Kawaida zenye Mabweni na Vyuo mkoani humo. Kamanda wa Jeshi hilo mkoani Pwani GOODLUCK ZELOTE ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake. Amebainisha kuwa Oparation hiyo inatokana na matukio ya moto kutokea mfululizo mkoani humo ambapo hivi karibuni shule ya Sekondary ya Filbert Bay iliungua moto na kuteketeteza baadhi majengo na maduka sita....

Like
496
0
Wednesday, 26 November 2014